Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,626
- 13,852
Waziri mkuu wa Israel hapana shaka ataingia kwenye rekodi za dunia kama mtu aliyeleta mateso makubwa si kwa wapalestina peke yao bali kwa dunia yote.Tayari ameshampiku Hitler na wengine waliotajwa kwenye historia ukimuondoa Fir'aun.
Wapalestina wameuliwa wengi sana kwa kupigwa kwenye majumba yao,mahospitalini mpaka kwenye makambi walikokimbilia kujificha.
Wananchi wa Israel kuanzia waliotekewa ndugu zao, wakulima na wengine raia wa kawaida wamelia sana wakitaka vita visimame na hawajaweza kumshawishi Netanyahu kufanya wanachokitaka.
Baraza la vita la Israel pamoja na kila siku kutishia kujiondoa kwa baadhi yao lakini wameshindwa kumshawishi kinyume Netanyahu afanye kinyume na matakwa yake. Wamebaki wanateseka tu.
Marekani nayo kila ikijaribu kusimamia makubaliano ya kusitisha vita ili angalau kwa maslahi ya uchaguzi ujao wameshindwa kumbadilisha Netanyahu.
Kila matumaini yakikaribia ya kufikiwa mwisho wa vita.Benjamini Netanyahu hua anatoa kauli ya kurudisha matumaini mpaka sifuri akisisitiza matakwa yake ambayo tayari ameambiwa hayatotimia,yaani kuifuta Hamas na kuwaokoa mateka.
Mateso ya Netanyahu kwa Marekani yamelifanya taifa hilo lizidi kupoteza heshima yake kwa ulimwengu kwani limejionesha wazi kuwa liko chini ya Israel.
Kwa upande mwengine uchumi wa Marekani umeathirika sana ktuokana na kushirikiana na Israel.
Mahakama za kimataifa na wale wanaoshitaki wamekuwa wakiteseka bure. Hakuna walichoweza kupata kwani Netanyahu ameongoza kuzidharau mamlaka hizo na kulazimisha anachotaka kwa kupinga mbele ya watu wote kilichoamuliwa.
Nchi kadhaa ambazo zimeibembeleza Israel chini ya Netanyahu isitishe mauwaji na nyengine kufanya maamuzi ya kuitambua Palestina nazo zinateseka bure kwani kila kukicha Netanyahu anazitishia nchi hizo kwa maamuzi yao hayo na kuahidi kuwa atawazuia kufanya kazi kwa utulivu chini ya serikali yake.
Kwa upande wa dunia kwa ujumla maamuzi ya Netanyahu yamepelekea kupanda kwa gharama za maisha mara nyingi sana kwani bei za mafuta na chakula vimebadilika sana kutokana na kuvurugika kwa misafara ya meli za mizigo baharini.
Muhimu ni kuwa mtu huyu,Benjamin Netanyahu atakuwa amevutwa afanye kibri ambapo mwisho wake utakuwa ushahidi kwa dunia nzima kuwa hakuna kiumbe anayeweza kuitesa dunia daima bila kutiwa mkononi.
Angalia hapo chini jinsi Netanyahu alivyomdharau Joe Biden,raisi wa Marekani baada ya kupokea ratiba yake ya kumaliza vita.