John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 68
- 117
Neno Yesu na neno Kristo Inamaanisha Nini
Neno Yesu
YESU ni jina la kiuanadamu la Bwana, alilopewa na Mariamu na malaika Gabrieli (Luka 1:31). “Yesu” maana yake ni “Mungu anaokoa”. Hili ndilo neno la Kigiriki linalofanana na neno la Kiebrania “Mashiak”au "Masihi."
Kuna vifungu vingi vya kinabii katika Agano la Kale ambavyo vinalenga kuja kwa Masihi ambaye atakomboa watu wake (Isaya 61:1; Danieli 9:26).
Hili lilikuwa jina la kawaida, na Yesu alizaliwa katika hali duni, mwanadamu, Mwana wa Adamu. Na ilikuwa kwa njia yake kwamba ulimwengu ungeokolewa! Dhambi ilikuwa imekuja ulimwenguni kupitia kutotii na kiburi cha mwanadamu wa kwanza, Adamu. Lakini ndani ya Mwanadamu Yesu, dhambi ilishindwa kupitia unyenyekevu na utii wake kwa Mungu. Kwa kutokubali kamwe kutenda dhambi alipojaribiwa, alishinda nguvu za mauti. Sasa tunaweza kuokolewa kutoka kwa dhambi kupitia kifo cha Yesu msalabani na kupata matunda ya Roho kwa kufuata maisha yake.
Israeli ya kale ilidhani Masihi wao angekuja na nguvu za kijeshi ili kuwaokoa kutoka utumwa wa miongo mingi na wafalme mbalimbali wa dunia hii (ikiwa ni pamoja na wafalme wa Kirumi). Lakini, Agano Jipya linaonyesha ukombozi bora zaidi anaoutoa Kristo Masihi, ni ukombozi kutoka kwa nguvu na adhabu ya dhambi (Luka 4:18; Warumi 6:23).
Wayahudi wa wakati wa Yesu walitarajia Masihi kukomboa Israeli kwa kupindua utawala wa Warumi na kuanzisha ufalme wa kidunia (Matendo ya Mitume 1:6). Baada ya kufufuka kwa Yesu, ndipo hatimaye wanafunzi wake walianza kuelewa ambacho unabii katika Agano la Kale ulimaanisha Masihi angefanya (Luka 24:25-27). Masihi "aliwekwa wakfu" kwanza kuwaokoa watu wake kiroho; kuwakomboa kutoka kwenye dhambi (Yohana 8:31-36). Alikamilisha wokovu huu kupitia kifo na kufufuka kwake (Yohana 3:16, Yohana 12:32).
Agano la Kale lilitabiri kuhusu Mkombozi ajaye, aliyechaguliwa na Mungu kukomboa Israeli (Isaya 42:1; 61:1-3). Mkombozi huyu alijulikana na Wayahudi kama Masihi. Yesu wa Nazareti alikuwa ndiye Masihi aliyetabiriwa (Luka 4:17-21; Yohana 4:25-26).
Neno Kristo
KRISTO ni jina la cheo chake, likiashiria kuwa Yesu alitumwa kutoka kwa Mungu kuwa Mfalme na Mkombozi (Danieli 9:25; Isaya 32:1).
Kristo siyo jina la mwisho (la ukoo) la Yesu, la hasha. Kristo linatoka kwenye neno la Kigiriki Kristos, maana yake "mtiwa mafuta", au "aliyetiwa wakfu" au "mteule".
Katika Israeli ya kale, wakati mtu alipopewa nafsi ya mamlaka, mafuta yalimiminwa kichwani mwake, ikiwa ni ishara kuwa ametiwa wakfu kwa kazi ya Mungu, yaani ni mteule wa Mungu. Wafalme, makuhani, na manabii walitiwa wakfu namna hiyo. Kutiwa mafuta lilikuwa ni tendo la ishara kuonyesha chaguo la Mungu (1Samwel 10:1, 1Samwel 24:6).
Katika Agano la Kale, watu walitiwa wakfu kwa majukumu ya nabii, kuhani na mfalme. Mungu alimwambia Eliya amtie mafuta Elisha ili awe nabii wa Israeli (1Wafalme 19:16). Haruni aliwekwa wakfu kama kuhani mkuu wa kwanza wa Israeli (Walawi 8:12). Samwel aliweka wakfu Sauli na Daudi kuwa wafalme wa Israeli (1Samweli 10:1; 16:12-13). Wanaume hawa wote walikuwa na majukumu "yaliyotiwa wakfu".
Katika Agano Jipya tunaona thibitisho kwamba Yesu ndiye Mteule: "Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake" (Yohana 20:31). Tunasikia ushuhuda kwamba Yesu ni "Masihi, Mwana wa Mungu aliye hai" (Mathayo 16:16).
Biblia inasema kuwa Yesu alitiwa wakfu kwa mafuta katika matukio mawili tofauti, na wanawake wawili tofauti (Mathayo 26:6-7; Luka 7:37-38). Lakini wakfu muhimu ulikuja wa Roho Mtakatifu (Matendo 10:38). "Kristo" kuwa jina la Yesu inamaanisha Yeye Yesu mwokozi, ndiye Mtiwa Mafuta wa Mungu, yule mmoja aliyetimiza nabii za Agano la Kale, Mwokozi mteule ambaye alikuja kukomboa wenye dhambi (1Timotheo 1:15).
Hii ndiyo sababu Yesu pia alipewa jina la cheo “Kristo”, linalomaanisha “Mtiwa-Mafuta” au “Mteule” au “Masihi”, aliyetumwa na Mungu Baba Yake kwa kazi kubwa ya kuokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi na mauti.
Yesu ni jina linalomaanisha "Mungu anaokoa", na Kristo ni cheo (status) cha Yesu linalomaanisha kuwa ni Mteule au Mtiwa Mafuta wa Mungu.
Hivyo, jina YESU KRISTO linamaanisha Yesu Masihi au Yesu Mtiwa Mafuta au Yesu Mteule wa Mungu.