mmmuhumba
JF-Expert Member
- Nov 8, 2017
- 493
- 478
Familia nyingi za sasa na walezi wengi wa sasa, wamekuwa ni sehemu ya kusababisha mengi mabaya ya jamii hii ya leo hususani katika malezi na makuzi ya watoto wa kike na wa kiume. Neno kusema hili ni tusi na kuacha kuzungumza ama kumuelekeza mtoto husika imefanya watoto kukutana nayo wenyewe na kuishi nayo kwa uwelewa wao.
Tunaona watoto wengi wa kike na kiume kushindwa kuhimiri mihemko yao ya ukuaji, uigaji na kushindwa kusimama katika ndoto zao kwa kukosa maarifa ya awali kutoka kwa familia zao ama walezi wao.
Jamii zetu watanzania wengi wazazi/walezi hatuwezi kuzungumza na watoto wetu kuhusu ngono, ndoto, jinsia, weledi, ukweli wa mambo ya sayansi na teknolojia na matumizi sahihi ya vifaa husika.
Ngono imekuwa ni sehemu ya kwanza ya kubomoa maisha ya watoto wetu, lakini wazazi na walezi hatunao ujasiri wa kuzungumza na watoto wetu ukweli kuhusu ngono na matokeo yake. Wazazi wengi ufikiri kuzungumza na mtoto juu ya ngono ni matusi. Mwisho watoto ushiriki na bila kujua ngono salama na matokeo ya kushiriki ngono ujenga kichwa ngono (sexual mentality) na bila kujali muda sahihi wa kushikiri ngono na kujitenga na mazingira hatarishi ya vishawishi ya kumuingiza kwenye uraibu wa ngono.
Ndoto, hakuna mzazi ama mlezi mwenye kutaka kuijua ndoto ya mwanaye na kuikuza ama kumpa wosia na motisha. Hili ni tusi, wengi wazazi na walezi uona ni kujidhalilisha na uchuro (nuksi na mzigo) maana wao wenyewe ni wa kwanza kufeli ndoto zao, hivyo kumuelekeza mwanaye ni tusi kubwa.
Jinsia, vijana wetu wa kike na kiume wanapaswa kufunzwa na wazazi wao kutambua umuhimu wa yeye kuwa wa kiume na wa kuwa wa kike. Lakini hili huwa halipo kwa wengi, familia nyingi hakuna mwenye kutoa muongozo wa umuhimu wa jinsia zetu katika jamii na familia zenye nafuu nazo, watoto wa jinsia zote ulelewa na mama muda mwingi na hivyo jinsia ya kike ubeba wingi weledi kwa mama. Ni aibu kukuta mtoto wa kiume kuiga mambo ya jinsia ya kike, siyo kwa kusudi baya bali ndio anachokiona kwa mama/mlezi wa kike. Familia zetu baba anapaswa amjenge mtoto wake wa kiume aone umuhimu wa kuwa mwanaume na mama naye afanye hivyo.
Weledi, ni ukweli mchungu ila kwasasa vijana wengi tuna uthubutu mdogo na uoga mwingi, wengi tumekuwa wazito kuanza jambo mpaka tuvutwe kwa nguvu kubwa. Vijana wengi katika makuzi yetu hatujafunzwa umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, umuhimu wa kuoa na kuolewa , kutafuta fursa wenyewe (utegemezi ni mwingi) na kutokuogopa kukubiliana na maisha. Leo wapo watoto wa kike na kiume wanakubali kuishi maisha yasiyo ya maadili kwa kukosa hili somo toka kwa wazazi/walezi. Watoto wa kiume wa leo ni waoga wa majukumu ya familia.
Sayansi na teknolojia athari zake katika vifaa vya habari, mawasiliano na matumizi sahihi na nufaishi. Wengi wazazi uona fahari watoto wao kuonekana ni wa kileo ila hawawapi ukweli juu ya matumizi sahihi. Siyo ajabu kukuta watoto wadogo wanasimu (vidogoli /janja), kompyuta na nk. Lakini zikawa ni sehemu ya kuwavuruga ubongo badala ya kuwajenga. Na makatazo mengi ya matumizi hayaanishi hasara na faida zake.
Neno tusi, tunapaswa kuliacha katika malezi na makuzi ya watoto wetu, kujenga jamii bora yenye ndoto zitazoishi, watao tambua ngono, watao tambua umuhimu wa jinsia zao na kuzitunza, watao tambua utamaduni wetu na kuurithi, watao tambua umuhimu wa kujituma kufanya kazi na wenye kujua kutambua kila wanacho kifanya kulingana na umri wao na jinsia zao.
Nini kifanyike?
1. Iwepo kampeni ya "neno tusi ni anguko la mtoto wa kike na wa kiume, wazazi tuseme na watoto wetu" (wizara husika ama taasisi husika zifanye kwa wazazi/walezi nchini).
2. Elimu shirikishi ya makuzi kwa darasa la juu la msingi iwepo juu ya masuala yanayo vuruga fikra na maadili kulingana na rika na walimu wahimizwe kualika wataalam wa afya na elimu ya mahusiano na ujasiriamali katika mada hizo hata mara chache kuongeza utambuzi, hamasa na uhalisia wa kitaaluma.
3. Maonyesho (video za maigizo) ya kufunza ya juu ya ngono, matokeo ya ngono ikiwa kama vipindi katika madarasa ya ukuaji iwe kama ni funzo la kuelekeza usahihi wa ngono, mbinu za kuzuia mimba, zinaa, wakati sahihi wa ngono na mahusiano na majukumu ya kijinsia.
Zamani tukiwa shule tulionyeshwa video za elimu juu ya magonjwa ya zinaa, ili tusaidia sana kujitenga na ngono. (Uwazi ni muhimu kwa watoto wa sasa maana ni wadadisi mno na dunia ina utandawazi mkubwa).
4. Maelekezo ya matumizi sahihi ya vifaa vya teknolojia yatolewe kwa watoto wa madarasa ya rika badala ya kuwepo kwa makatazo mengi yasiyo onyesha athari na faida ya vitu hivyo (wizara ya elimu na wazazi/walezi) kama simu, tablet, kompyuta nk.
Mukusudi ni yapi?
1. Kujenga watoto wenye kutambua thamani za jinsia zao na kuzitunza jinsia zao.
2. Kujenga vijana wenye wingi uthubutu na ujasiri wa kuyabeba majukumu yao na ya kijamii.
3. Kujenga jamii itayoitambua teknolojia kama siyo adui bali ni fursa.
4. Kuimarisha umuhimu wa wazazi/walezi kusimamia ndoto za watoto wa kike na kiume.
5. Kujenga jamii jumuishi katika malezi na makuzi ya kijinsi ya watoto, vijana , utamaduni na kufungua uchumi zaidi tegemezi kwa vijana.
Tuweke akilini " usipomtumia mwanao, mwingine awezaye kumtumia atamtumia kuwa kifaa kibaya" hivyo kuliacha neno tusi ni kuwakomboa kifikra watoto wetu, maendeleo na matumizi ya teknolojia kitaaluma, ubunifu biashara na biashara.
Na: mmmuhumba