"Nenda karuke nao pamoja; hata kama hufanani nao"

RIGHT MARKER

Member
Apr 30, 2018
99
360
💼 MHADHARA WA 12

Mwanangu eeh! Mara moja moja ukishika hata shilingi elfu 30 nenda katembelee hoteli ya kifahari au maeneo mengine ya kifahari. Fika hoteli ya kifahari agiza glasi moja ya juice anza kunywa kwa mbwembwe mpaka wakuone "na wewe ni mtu". Wakati unakunywa hiyo Juice punguza speed ya kunywa kwa sababu huenda hela utakayobaki nayo mfukoni isiweze kununua chochote eneo hilo. Hivyo hakikisha unakunywa taratibu mpaka wahudumu waje wakwambie; "Kaka/dada maliza hiyo juice yako uondoke!!"

Usijali sana kuhusu wahenga waliosema; "Ndege wafananao huruka pamoja" - Wewe nenda karuke nao pamoja hata kama hufanani nao. Ukifanya hivyo zaidi ya mara moja unaweza kupata rafiki ambaye atakuonyesha barabara ya kuelekea duniani.

Unajua nini mwanangu!! ngoja nikwambie kwa herufi kubwa; CHATU HANG'AI GIZANI. Kama huamini muweke Chatu kwenye chumba cha giza kamwe hutomwona, lakini akiwa ndani ya chumba chenye mwanga au ukiwasha tochi kwenye chumba alichomo chatu utaona ngozi yake ya mabakabaka inang'aa.

Huo mfano una maana ifuatayo;
(1) CHATU - ni wewe.
(2) CHUMBA CHA GIZA - ni vile unavyojitafuta bila malengo wala mikakati.
(3) CHUMBA CHA MWANGA - ni vile unavyojitafuta kwa kuzingatia nini unafanya, kwa nini unafanya, wapi unafanya, na unafanya na akina nani (watu wanaokuzunguka),

Mwanangu eeh!! hebu tuamke usingizi bila hela unachosha. Wewe na mimi ni kama chatu lakini tupo kwenye chumba chenye giza, unadhani hapa tulipo nani atatuona. Aliwahi kusema ANSEL ADAMS kuwa; "Picha nzuri ni kujua pa kusimama" - Ni kweli kabisa, ukitaka kupiga picha nzuri unapaswa kuchagua sehemu nzuri ya kusimama - CHAGUA MARAFIKI BORA.

By: RIGHT MARKER-TZ
Septemba 21, 2024
Mbezi Louis, Dar es salaam.
 
Weeee usinambie
Ngoja nijaribu
 
Bro,yaani michongo uipate jf,wakati kila siku tumezungukwa na watu kibao ambao ukiwa serious madili kibao unapata.

Sikatai nimejifunza mengi kupitia jf lakini kwenye kupata michongoooo.........hapana na sihitaji partiner yeyote ambaye ni anonymous
namaanisha mtu awe anapost yale anayoona yanaingiza hela huko alipo

hivyo tu kuliko kujaza mashairi humu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom