Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,782
- 13,541
NEMC Kanda ya Temeke yafanya ukaguzi katika Kampuni ya African Inland Container Depot iliyopo Kata ya Sandali, Mtaa wa Usalama, Wilaya ya Temeke.
Hii ni kufuatia tukio la moto wiki iliyopita ambapo. Sulphur katika ghala hilo ilingua na kusababisha moshi mwingi kusambaa.
Malalamiko ya awali - Wakazi wa TAZARA (Dar) na maeneo jirani tumeathiriwa na moshi wa malighafi zenye sumu zilizolipuka kwenye godauni
Aidha, timu ilifika katika ofisi za Fire na Kata kupata maelezo juu ya tukio hilo na kubaini uwepo wa vumbi la sulphur, wafanyakazi kutokua na vifaa kinga maalumu kwa ajili ya kazi hiyo, umwagikaji hovyo wa sulphur, uhifadhi wa sulphur eneo la wazi ambapo unaweza kuleta athari kipindi cha mvua na uwezekano wa sulphur kuelekea kwenye mifereji ya mvua.
Taarifa za awali zinasema kuwa moshi huo ulisababisha baadhi ya mimea karibu na maeneo hayo kukauka na watu kupata madhara kama macho kuwasha na kupoteza fahamu.
Meneja wa NEMC Kanda ya Temeke, Arnold Mapunduzi aelezea:
Bado hatujachukua hatua kabisa, tunampa nafasi mteja kwa kumpa maelekezo ya nini kifanyike kisha aje tueleweshane kipi anatakiwa kukifanya na kipi hataki kufanya ili kulinda usalama wa Watu na mazingira.
Taarifa za awali kuhusu madhara tumeelezwa kuwa Watu walikohoa na wengine walikuwa wanadondoka, kuhusu Sulphur kuwa na sumu kidogo inanizumbua, lakini Sulphur ni kemikali na Kemikali yoyote nis umu il ani kwa kuwa kiwango gani hilo nalo linajitegemea.
Wafanyakazi wanaofanya sehemu kama hiyo wanatakiwa kujilinda kwa kuwa na vifaa kinga, wanatakiwa kuvaa vitu kama barakoa na gloves kwa kuwa kile wanachodili nacho ni Kemikali.
Kuhusu fidia ya wanaodaiwa kuathirika hilo siyo letu, sisi tunasimamia kanuni za mazingira na kutoa maelekezo ya nini kifanyike ili kujikinga.
Shughuli pale kiwandani zinaendelea kama kawaida kwa kuwa hatujamfungia na lengo letu sio kuwa tunafungia biashara, lengo ni kulinda Watu na viumbe hai vingine.