NEMC: Kuchoma gari au shehena yoyote kwa makusudi ni kinyume na Sheria ya Uchafuzi wa Ardhi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,934
13,689
Mjadala ulizuka baada ya muimbaji wa nyimbo za Injili kuchoma moto gari alilopewa kama zawadi na Mchungaji, ambapo baadhi ya watu walisema hilo ni kosa kisheria wengine wakisema siyo kosa kisheria. Wakili Bashir Yakub alilitolea ufafanuzi upande wa kisheria (zaidi soma hapa), lakini je, upande wa utunzaji wa mazingira imekaaje ukizangati kuna juhudi nyingi zinafanyika ili kupunguza athari za tabia nchi?

JamiiForums ilizungumza na Meneja Uzingatiaji wa Sheria wa NEMC, Hamadi Tymuro ambapo alisema;

"Unapochoma gari au shehena yoyote kama unavyosema inamaanisha vifaa au vitu vilivyomo ndani ya hicho inachokichoma kama vile tairi, mafuta vitasababisha moshi kusambaa.

"Unapofanya hivyo unaweza kuchafua hewa, ardhi au maji kama yapo chini ya ardhi ya eneo husika, vyote hivyo vinapingwa na Sheria ya Uchafuzi wa Ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 ambayo inakataza uchafuzi wa mazingira.

"Ndani ya Sheria hiyo category inaeleza hutakiwi kufanya uchafuzi wa mazingira wa aina yoyote.

"Mtu anapofanya kwa makusudi anaweza kuchukuliwa hatua kwa kupigwa faini au kutakiwa kusafisha eneo husika."
 
Mjadala ulizuka baada ya muimbaji wa nyimbo za Injili kuchoma moto gari alilopewa kama zawadi na Mchungaji, ambapo baadhi ya watu walisema hilo ni kosa kisheria wengine wakisema siyo kosa kisheria. Wakili Bshiri Yakub alilitolea ufafanuzi upande wa kisheria (zaidi soma hapa), lakini je, upande wa utunzaji wa mazingira imekaaje ukizangati kuna juhudi nyingi zinafanyika ili kupunguza athari za tabia nchi?

Back
Top Bottom