Wana JF,
Katika kupitia nukuu za Viongozi maarufu duniani tulio wahi kuwa nao akiwemo Nelson Mandela(Mungu amlaze mahali pema peponi) nimekutana na hii inayosema ''Fools multiply when wisemen are silent''. Naomba tutafakari nukuu hii kwa pamoja kwa kuilinganisha na siasa za CCM kwa nchi yetu Tanzania.
Bila shaka Marehemu Nelson Mandela aliona mbali sana kwa kutoa tamshi kama hili. Kwamba watu wenye busara wakinyamaza basi wapumbavu au wajinga wataongezeka! Serikali ya CCM kwa vipindi vyote imekuwa haitaki kukosolewa na watu wenye busara ili iruhusu WAJINGA KUONGEZEKA NA HIVYO IWEZE KUWATAWALA KIULAINI.
Ukiangalia hata sasa huu utawala wa A5 hautaki kukosolewa wala kusahihishwa na watu wenye busara walioko ndani au nje ya CCM. Tunachoshuhudia kwa sasa ni JUHUDI KUBWA ZA KIMABAVU KUJARIBU KUWANYAMAZISHA WATU WENYE BUSARA ZAO ILI WASIJE WAKASIKIKA NA KUWAFANYA WAPUMBAVU WAEREVUKE!!! Hiyo ndiyo sera tunayoiona kwa sasa kutoka kwa Rais JPM.
Kila mahali sasa tunaona WAPINZANI(wenye busara) wakilazimishwa kukaa kimya kwa kufunguliwa mashtaka yasiyo kichwa wala miguu na kuewa vifungo vya miezi 6,8 na pengine tunakoelekea ni kwenda KUZALISHA WAFUNGWA WA KISIASA kama ilivyokuwa enzi za mkolone.
Hii ni aibu kubwa kwa nchi inayojidai iko huru lakini inaendelea kuzalisha wafungwa wa kisiasa. Nafikiri ni wakti mwafaka sasa kwa jumuia za kimataifa kuiangalia Tanzania kwa jicho la tatu hatimaye kuikemea na kuionya kuwa inachofanya kwa wanasiasa wa Upinzani siyo sahihi na hakikubaliki hata kidogo.