NECTA yaelemewa na Rufaa za vyeti vyeki, yasimamisha shughuli nyingine zote!

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limeamua kusimamisha shughuli nyingine zote barazani hapo ili kushughulikia rufaa za watumishi waliotangazwa na serikali kwamba walifoji vyeti.

Leo katika viunga vya baraza hilo nimeshuhudia umati mkubwa wa watumishi, wengi kutoka mikoani wakiwa wamefurika hapo wengi wakilalamika waliingizwa kwenye orodha ya wenye vyeti feki kimakosa.

Kutokana na Necta kuelemewa na idadi kubwa ya wakata rufaa hao, uongozi ukatangaxia wananchi wengine waliofika kwa shughuli nyingine kwamba kwa sasa hakuna mtu mwingine yeyote atakayehudumiwa zaidi ya hao watumishi wenye malalamiko ya kuingizwa kimakosa katika orodha ya wenye vyeti vyeki!

Hata hivyo wateja wengine wa Baraza la Mitihani wamelaumu uongozo wa Baraza kwa uamuzi huo. Wamedai kwamba nao pia wanahaki ya kuhudumiwa. Na pia wameshangazwa na bodi kusimamisha huduma nyingine badala ya kujipanga kuwahudumia wateja wao wote kwa utaratibu maalum badala ya kuahirisha huduma kwa muda usiojulikana!

Source: Mimi mwenyewe!
 
Ndio maana waziri mwenye dhamana alisema 'kwa yeyote anayedhani ameonewa ruhusa kukata rufaa, ila ikabainika haikuwa kimakosa adhabu kali itatolewa' watu ndio hivyoo wanatumia fursa. Wengine hapo ndio mwanya wa kutoa rushwa vyeti viwe original.
 
Na wewe ni kati ya wenye vyeti fake??
 
Wamefika elfu 10. Acheni dhihaka. Hili ni jambo jema mno kwa taifa letu . Wangeweka kituo cha polisi hapo
 
"...umakini sio sifa wala tabia ya watu wenye papara... "
Thabo Mbeki

Kulikuwa na haraka gani kuja na listi ya majina pasipo kujiridhisha na kuhoji wahusika ili walete vielelezo ambavyo vingepelekwa NECTA kwa verification
Inashangaza sana Mkuu!
 
Reactions: BAK
Janga kubwa la Taifa huyu, mwenyewe anadai anainyoosha nchi!!!!!

"...umakini sio sifa wala tabia ya watu wenye papara... "
Thabo Mbeki

Kulikuwa na haraka gani kuja na listi ya majina pasipo kujiridhisha na kuhoji wahusika ili walete vielelezo ambavyo vingepelekwa NECTA kwa verification
 
Hiyo itawakumbusha kwamba umakini unahitajika kwenye kushughulikia mambo yanayogusa maisha ya watu
Kweli kabisa, kama kuna watu wameensa na orijino halaf wapo kwenye list ya 9000, sijui watawabebaje?
Nadhan serikali ilipaswa kuhakikisha watu wanahakiki tena taarifa zao ndo watoe majina
 
Ndio maana waziri mwenye dhamana alisema 'kwa yeyote anayedhani ameonewa ruhusa kukata rufaa, ila ikabainika haikuwa kimakosa adhabu kali itatolewa' watu ndio hivyoo wanatumia fursa. Wengine hapo ndio mwanya wa kutoa rushwa vyeti viwe original.

Kwani Bashite alitumia mbinu hii ndiyo maana haguswi?
 
Reactions: SDG
Kweli kabisa, kama kuna watu wameensa na orijino halaf wapo kwenye list ya 9000, sijui watawabebaje?
Nadhan serikali ilipaswa kuhakikisha watu wanahakiki tena taarifa zao ndo watoe majina
Kinachoonekana wazi ni kwamba waliharakisha kutoa majina na kukabidhi ripoti kwa Mh ili waiwahi Meimosi! Labda lilikuwa ni shinikizo kutoka kwa Mh Mtukufu!
 
Uongo mi Niko hapa toka asubuhi mpaka dakika hii hakuna kama hicho. Hii messages ametunga lisu ili kuwapa tension watu mana yeye analenga kuichafua serikali tu kwa mwavuli wa TLS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…