NEC yaiazima NIDA baadhi ya mitambo ya TEHAMA kutekeleza utoaji wa vitambulisho vya taifa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,296
Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC imeridhia kuiazima Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA sehemu ya mitambo ya TEHAMA kwa muda wa siku 90 kwa ajili ya kuchakata taarifa wakati wa utekelezaji wa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya taifa.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha tume hiyo kilichofanyika hapo jana katika ofisi za NEC jijini Dar es salaam ambapo wajumbe wamekubaliana kwa kauli moja ya kuhamishwa kwa muda mitambo hiyo kutoka ofisi zao na kwenda NIDA kwa gharama za mamlaka hiyo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguziJaji Lubuva amesema kwamba taratibu za makabidhiano hayo zitaandaliwa ili kuwezesha mitambo hiyo ya TEHAMA kuhamishiwa NIDA kwa muda na kufafanua kwamba kutokuwepo kwa miudombinu ya mawasiliano ambayo ingeunganisha mitambo ya NEC kwenda NIDA ndiyo sababu ya kuhamisha mitambo mahali uchakataji unapofanyika.

Aidha akiwasilisha taarifa ya wataalamu iliyopitia maombi ya NIDA Mkurugenzi wa uchaguzi Ndg, Kailima Ramadhan amesema tume ya taifa ya uchaguzi ilinunua mitambo hiyo ya TEHAMA kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uandikishaji wapiga kura na uchaguzi mkuu wa 2015.

Hata hivyo ameeleza kuwa mitambo hiyo ina uwezo mkubwa wa kuchakata taarifa hususani uchakataji wa alama za vidole (finger prints).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…