Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,013
- 6,755
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imelitangaza Jimbo la Konde huko Pemba kuwa wazi baada ya mbunge mteule, Sheha Mpemba Faki kutangaza kujiuzulu kabla ya kuapishwa na taratibu za kujaza nafasi hiyo zitatangazwa hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk Wilson Mahera imeeleza kuwa tume imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Agosti 2 ikitoa taarifa kuwa mbunge huyo mteule aliandika barua kwa chama chake kukitaarifu kuwa hayupo tayari kuwawakilisha wananchi wa Konde katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na changamoto za kifamilia.
Mbunge mteule ajiuzulu, CCM yasikitika
“Kutokana na hatua hiyo, Tume inatoa taarifa kwa umma kuwa Jimbo la Konde lipo wazi na taratibu za kujaza nafasi hiyo zitatangazwa hivi karibuni. Tume imefanya hivyo kwa kuwa ilikuwa bado haijamjulisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusu kukamilika kwa uchaguzi katika Jimbo la Konde na kuchaguliwa kwa mbunge huyo. Aidha, tume ilikuwa haijamtangaza kwenye Gazeti la Serikali kama inavyoelekezwa na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,” amesema Dk Mahera.
Awali, amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka kwa Spika kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge katika Jimbo la Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba –Zanzibar kutokana na kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Khatibu Saidi Haji wa chama cha ACT - Wazalendo.
“Kutokana na taarifa hiyo ya Spika, Tume ya Uchaguzi iliitisha uchaguzi uliofanyika Julai 18,” amefafanua.
Faki amejiuzulu siku 14 tangu achaguliwe na kutangazwa kushinda ubunge wa jimbo hilo katikauchaguzi ambao ACT Wazalengo wamelalamikia kuchezewa mchezo mchafu uliofanya washindwe kutetea kiti hicho walichoshinda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.