The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,897
- 2,866
Watanzania ni watu wa ajabu sana yaani wizara ya michezo naambiwa imepeleka wanamichezo 7 kwenye michezo ya Olympic ufaransa ambao nao hawana uhakika wa medali kutokana na mazingira duni ya namna wanavyoandaliwa.
Badala waziri aumize kichwa na kuangalia ni namna gani atapeleka wachezaji wa kutosha badala yake yeye anakwenda huko kuzurura na kula padiem za serikali Bure.
Yaani hata kama ingekuwa tuko vizuri basi ni heri nafasi ya waziri angeachia wanaocheza ili aongeze timu ya washindanaji. Nina uhakika gharama za waziri kwenda ufaransa zingeweza kugharamia wanamichezo hata 20 ni heri angepanua hata wigo wa ushindani na kuwajengea uzoefu kuliko yeye kwenda na timu isiyoweza kushinda kivyovyote.
Taifa hili lina watu million 60 lakini hatutoi ushindani unaoreflect hiyo namba hata tu kwa hawa jirani zetu.
Mimi binafsi jambo hili nalionea aibu ndipo najiuliza inakuwaje waziri haoni aibu ya kukaa huko ufaransa alafu watu anaowasapoti wako 7 nao waneandaliwa kiyatimayatima.
Kwa mwendo huu sioni kama kuna hatua tutapiga kuelekea maendeleo ya kweli katika secta ya michezo.