Ndugu zangu, sisi sote baba yetu mmoja

Nov 28, 2023
9
7
Habari kiongozi unasoma post hii naandika nikiwa na maumivu makali mno ya moyo maana najiuliza baba yetu alikosea kutuachia Mali? maana tunawaua watoto wetu, wadogo zetu na ndugu zetu kisa tunataka Mali waliyonayo hii ni sawa ama ni haki?

Mwaka mmoja sasa tangu nimekuwa na rafiki toka kongo Hasa mji wa goma ameonyesha mengi yanayoendelea huko Mimi mtoto wa kiume ninamoyo mgumu ila sio wa kikatili Kuna picha na video clip nimekuwa naziona zinaniumiza moyo sana jaman Afrika ni ya nani?

Nani aliyelitengeneza bara hili?

Nani aliyeziweka rasilimali zilizoko afrika?

Kila kitu imekuwa mzungu uchumi mzungu aamue, siasa bora na utawala mzungu aamue, amani ya taifa fulani mzungu aamue, mabadiliko yoyote mzungu aamue Kuna haja gani ya kuwa huru kama kila kitu mpaka mzungu aamue?

Nina picha za Kongo zimejaa ukatili kweli kweli kama unahitaji kudhibitisha ninachokisema nakutumia.

Kuhusu Amani ya Kongo simlalamikii mzungu ila na mlalamikia nchi zote za afrika hata kama ubinafsi ila umezindi sana wanaokufa kule si binadamu kama sisi? Kwanini usijisikie uchungu binadamu mwenzio akipoteza uhai?
 
Back
Top Bottom