mzaramo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2006
- 6,371
- 5,183
Mwaka 2015 Nilirudi kutoka kutafuta maisha,sikuwa mbali sana na nyumbani nilikuwa moja kati ya nchi zinazotuzunguka...
Huu ni mwaka uliokuwa na matukio mengi katika maisha yangu ukiacha mkenge tulioingia kama nchi kwa kumchagua Magufuli kuwa Raisi pia kwa mara ya Kwanza niliachwa na mtu niliempenda na kulazimishwa kwenda kwa Mganga kuroga ili anirudie.
Nakuchukia mwaka 2015.
Nilikuwa na Msichana ambae Unaweza kusema ni mchumba wangu japo sikuwa nimemchumbia rasmi ila mapenzi yetu yalikuwa na miaka mingi kiasi ambacho ndugu zake wote walikuwa wananijua huku ndugu zangu wakiwa wanamtambua kama mchumba wangu.
Katika harakati za maisha nikasafiri na kwenda nchi jirani kuweka sawa kidogo maisha yangu...Nikiwa huko nilikuwa nawasiliana bila matatizo na kusema kweli yule Msichana alikuwa mvumilivu na muelewa Mungu amtilie wepesi kwenye Ndoa yake In Sha Allah...
Sikuwa nchini kwa miaka takribani mitatu na siku niliyorudi nikasema nifanye sapraisi nije kimya kimya.....Kweli nikafanya namna hiyo Nilirudi bila kumwambia.
Muda wote huo nilikuwa nawasiliana nae WhatsApp na alikuwa anajua bado sijarudi...Siku ya pili yake toka nirudi nikaona Leo ndio siku muafaka nimstukize mpenzi wangu basi nikatoka na kwenda kumsubiri nje ya ofisi yao.
Nimekaa pale nje kwenye gari huku nachati nae upo wapi anajibu nipo kazini unatoka saa ngapi anajibu saa 12 jioni...Basi kufika saa 12 na nusu jioni anatoka ofisini kwake mm nimetulia tu kwenye gari kimyaaa kabisa kwa macho yangu namuona mpenzi wangu anaingia kwenye gari ya mwanaume mwingine nikajikaza nikawa nawasindikiza wao mbele mimi nyuma ila nikawa nikituma meseji WhatsApp ajibu kitu.
Huku roho ikiwa inanidunda na kuniuma waliongoza pamoja mpaka Mgahawa mmoja hivi huko mitaa ya Ilala wakaingia pale...Walivyoshuka kwenye gari na mimi nikashuka bila wao kuniona wakaagiza chakula pale na vinywaji wakawa wanajichana mimi niliagiza Maji ila hata nguvu ya kuyafungua sikuwa nayo.
Nilitamani niende kufanya vurugu pale maana kwa nilivyomuona yule jamaa nilijua kabisa nikipandisha mori yangu ya kizaramo aniambii kitu nitamchakaza vizuri tu ila niliogopa aibu maana mwanamke anaweza kukukana hakujui mbele za watu mwisho wa siku ukaonekana kibaka raia wenye hasira kali wakajichukulia sheria mkononi nikafa kizembe.
Nikajakaza kaza pale wakalishana pale kama Kinda la ndege na mama ake chakula cha kula dakika 5 wakatumia saa nzima mpaka giza likaingia pale...Wakatoka kwenye pale Hotelini wakaingia kwenye gari hao wakaondoka zao.
Na mimi nikaunga Tela nyuma nyuma na kigari changu....Hao mpaka mitaa ya kwao yule Msichana wakapaki gari pale karibu dakika 15 nzima nami uvumilivu ushanishinda natamani kwenda kufanya balaa langu pale...Alhamdulliah kabla shetani langu alijapanda yule bibie akashuka na kwenda kwao.
Usiku ulikuwa mrefu usingizi ukanigomea kabisa wallah hasa ukizingatia niliweka nia kabisa nakuja kumuona huyu alafu nikashuudia mwenyewe nasalitiwa mchana peupe....basi Kesho yake nikajikaza kaza pale nikachati nae WhatsApp nikamdanganya sikia kuna mzigo nimeutuma na ndugu zangu siwaamini amini wale washenzi Kesho nataka uende sehemu ukachukue huo mzigo akasema poa.
Basi Kesho yake nikampa namba ya mshkaji wangu akampigia kwa kumzuga kuwa yeye ndio anao huo mzigo wangu akamuelekeza pa kwenda kukutana nae....Basi ile anafika pale anakuta mzigo mwenyewe ndio mimi yule mwanamke kidogo adondoke kwa hofu na wasiwasi...
Nikamwambia Ingia kwenye gari kuingia nikamwambia nipe simu yako....Balaa likaanza pale na nguvu kidogo ikabidi itumike mwishoe nikaichukua simu yake kupekua ni aibu tupu kumbe wale wapenzi karibu miezi 6 nyuma pale pale nikaamua kuachana nae aendelee na huyo jamaa yake japo aliliia lia pale nimsamehe mwanaume nikakaza na pale pale nikawapigia ndugu zake na kuwaambia huyu naachana nae kwa sababu nimegundua ananisaliti.
Basi ndugu zake wa Tanga wakanipigia simu niende tukaongee kufika kule ndio napata habari kumbe yule jamaa kishapeleka mpaka barua anataka kuoa ila mwanamke wangu alishindwa kuniambia ukweli na wao walikuwa pia walishindwa kuniambia kwa sababu walijua mimi najua maana yule bibie aliwadanganya kwao kuwa mimi najua na nimekubalia aolewe sasa wakashangaa kwanini nimewapigia simu kulalamika kuwa nimemfumania wakati mimi nishaachana nae na yule ni mchumba wa mtu?!
Basi kufika Tanga ndio wakanisharauri huyu itakuwa karogwa tu sio bure hapa dawa twende kwa Mganga Pangani huyo Mganga ni kiboko Leo anafanya mambo Kesho wanaachana wale nakwambia mimi nikabaki kushangaa tu wakanilazimisha pale wewe ndio chaguo letu na sio huyo mchumba mpya.
Basi nikakubali hao mpaka kwa Mganga Pangani kufika pale Mganga kabla hata hatujamwambia shida yetu akajua kila kitu dadeki aiseee nilishangaa sana...Basi nikamwambia jina langu na jina la huyo mwanamke akafanya mambo yake pale nikapewa nazi na mayai viza nikavunje njooni pale pale kwa Mganga na nazi nyingine nikavunje makaburini usiku.
Kweli usiku wake huku nikiwa naogopa nikaenda kuvunja nikiwa nimesindikizwa na shemeji yangu tukavunja pale na kurudi kulala huku nikijilaumu haya mambo gani tena nafanya mimi jamani...Basi Mganga alitupa siku 3 mpaka 7 majibu lazima yawe mazuri.
Nikarudi zangu Dar....Kweli baada ya siku 4 hivi mambo yakaanza kujipa nikasikia wamegombana wale na wameachana huku ndugu zake yule bibie wakanisisitizia ni muda wangu wakupeleka barua nioe mimi maana yule jamaa kishaachwa Mganga kafanya mambo yawe.
Kusema kweli mimi nilijisikia vibaya sana kwa kile kitu maana yale yashakuwa mapenzi ya kichawi maana yake baada ya muda dawa za Mganga zitaisha na atataka kurudiana na yule jamaa wake sasa itakuaje kama ikiwa mimi nishamuoa au ndio najiaandaa kumuona si litakuwa balaa na aibu!?
Basi mimi nikaona hapa ishakuwa msala na aibu nikaamua kufanya maamuzi ya kiume nikabadili namba yangu ya simu na kuwa mbali na ile familia maana niliogopa kama unakwenda kuoa kwenye familia ambayo inaamini kwenye uchawi na kurogana si hatari hiyo kwa ustawi wa familia yako?!
Miaka miwili imepita sasa toka lile tukio lipite Leo nimejisikia kusema kuhusu iki kitu....hakuna ndugu yangu yoyote anayejua kwanini niliachana na yule mwanamke na Leo kwa mara ya Kwanza nimesema kitu gani kilichotokea kule Tanga...
Ilinifanya nijue kuwa kwenye mapenzi watu wanatumia uchawi na kurogana ilinishangaza sana ila ilinifunza pia.
Asante kwa kunisoma mkuu.