Ndoto ya usiku wa leo imenitisha, msaada kwa anayejua tafsiri au maana

kiredio Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2024
1,068
1,975
Usiku wa leo nimeota ndoto ya ajabu sana, nimeota kuna mtu ninaye mfahamu ananikimbiza na kutaka kunidhuru.

Nikaanza kumkemea kwa maombi huku namnyooshea kidole, ghafla nikaanza kupaa angani mpaka nikafika kilele cha juu mawinguni, chini nikawa naona mazingira tofauti kabisa ambayo sijawahi kuyaona.

Wajuzi wa mambo ya ndoto naombeni mnijuze ndoto hii itakuwa na maana au tafsiri gani kwasababu imenitisha sana kwakweli.
 
Uko juu mawinguni 🔥🔥🔥
1000030407.jpg
 
Bwana Yesu Asifiwe Mtumishi wa Mungu .!?
 
Kuna changamoto utakutananayo siku za usoni lakini hatima yake ni kwamba utaibuka shujaa...

Labda hayo mazingira yalionekanaje unaweza ukaelezea?
 
Huyo anayekukimbiza alikuwa anataka kula kisamvu chako, uliposhtuka na kukemea na kupaa juu angani maana yake ulinusurika kuliwa kimsavu usiku huo. Hongera sana kwa kuendelea kuulinda ubingwa wako.
Kumbe wewe ushawahi kuliwa kisamvu ndotoni? Aisee pole sana mkuu. Tupe stori ilikuwaje maana mpka umesema ni kwamba tayari uliliwa.
 
Back
Top Bottom