Ndoa ya CCM na Polisi inatuharibia nchi

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
25,253
36,508
Nimekuwa naipinga sana CHADEMA kwa sababu ya uCCM wangu.

Lakini kwa hizi pilika zinazofanywa na serikali kukandamiza wapinzani kwa sababu ya kulinda uozo wetu zinanipa mashaka kuwa CCM ndo imekuwa inashika dola na siyo kuongoza dola.

1. Ukikosana na kipngozi wa CCM jiandae kupambana na polisi

2. Ukimkosoa kiongozi wa CCM jiandae kupambana na polisi

3. CCM tunalindwa kwenye joggings zetu lakini wewe mpinzani thubutu yako uone cha moto

4. CCM tunafanya mikutano ya ndani na nje tukiwa na bonus ya ulinzi. Lakini upinzani hata bango la kikao cha ndani ni ugaidi

5. CCM inaajiri watu wa dola kwa kazi za ndani ya chama. Lakini ole wao watakaoenda kuajiriwa upinzani wataitwa magaidi

6. Sheria ya vyama vingi imekataza waajiriwa wote wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya ama kushiriki siasa, lakini tuna mabrigedia, majenerali na watu wengi wa usalama kwenye political apointees kama wakuu wa wilaya na mikoa na hata wengine kupata vyeo ndani ya chama.

7. Kwenye michakato yetu CCM ya kura za uteuzi wa wagombea, nimeshuhudia kila kitu kinaratibiwa na wavaa viatu, lakini upinzani hawapati msaada wowote kutoka huko kwenye teuzi zao.

Haya ni machache kati ya mengi yanayohusu ndoa kati ya vyombo vyetu vya usalama na CCM.

Hii ndoa inapoelekea ni kwenye MAPENZI UPOFU. Hii ni hatari sana kwa Usalama na ustawi wa Taifa. Hivyo tumefikia mahali kwamba

1. CCM tumezalisha ukoloni mpya

2. CCM imeleta nchini ubaguzi baina ya raia wa nchi hii

3. CCM imegeumaa kuwa kichaka cha majambazi ya mali za umma na wabadhirifu

4. CCM imegeuka kuwa kichaka cha wahalifu kwa sababu haichukui hatua zozote dhidi ya watu hao na sana sana wanapewa vyeo.

Ni vizuri sana endapo chama hiki kikongwe kitabadilika au kiondolewe madarakani kupitia sanduku la kura.

Screenshot_20211004-223734_Drive.jpg
 
Mmmmmh, wakusema hayo leo? Kuanzia uchaguzi wa mwaka 1995 hali ni hiyo hiyo, uchaguzi wa 2010 na 2015 ndo kabisaa mapenzi ya CCM na POLISI yalikuwa yameshika kasi, na mimba nyingi walitoa, uchaguzi wa 2020 wamezaa na mtoto kabisa, mbona hukuwahi kusema hayo na yalikuwa wazi kabisa?

Au wewe maslahi yako kwenye serikali ya SSH yameshikiliwa ndo maana umekumbuka kupaza sauti?
 
Mmmmmh, wakusema hayo leo? Kuanzia uchaguzi wa mwaka 1995 hali ni hiyo hiyo, uchaguzi wa 2010 na 2015 ndo kabisaa mapenzi ya CCM na POLISI yalikuwa yameshika kasi, na mimba nyingi walitoa, uchaguzi wa 2020 wamezaa na mtoto kabisa, mbona hukuwahi kusema hayo na yalikuwa wazi kabisa? Au wewe maslahi yako kwenye serikali ya SSH yameshikiliwa ndo maana umekumbuka kupaza sauti?
Fuatilia posts zangu za miaka hiyo.

Mojawapo ya kanuni za MwanaCCM ni kusema kweli daima. Au kuna fitina kwenye bandiko langu?

Neno matumaini halikuwekwa bahati mbaya, bali kama hayaelekei kuwepo basi hatua zingine hufuatwa.
 
Tatizo kubwa ni wanaCCM wenzangu waliojazana vyama vya upinzani wakiwa na lengo la kudhoofisha vyama hivyo.

Hawa wanaorudi siyo kwamba wameona sera za CCM zimebadilika bali wanarudi nyumbani.

Siyo dhambi endapo upinzani utaamua kupeleka vijana wao CCM kwa lengo lile lile tunalolifanya sisi
 
Ukoloni mambo chama tawala(CCM), huu tafsiri yake iwe mfumo wa utawala wa chama dola ambao mapolisi wako hadi uvunguni
 
Fuatilia posts zangu za miaka hiyo.

Mojawapo ya kanuni za MwanaCCM ni kusema kweli daima. Au kuna fitina kwenye bandiko langu?

Neno matumaini halikuwekwa bahati mbaya, bali kama hayaelekei kuwepo basi hatua zingine hufuatwa.
Sawa mkuu, pengine nimejichanganya, ila kama nakumbuka vyema mijadala moto wakati wa nguruvi Kichuguu Mag3 na wadau wengine ulikuwa mtetezi mkubwa wa CCM.
 
Siku polisi na tume ya uchaguzi wakiacha kwa makusudi kabisa kuisaidia CCM, hakika kitakacho tokea baada ya hapo ni anguko kubwa na la kihistoria nchini.
 
Sawa mkuu, pengine nimejichanganya, ila kama nakumbuka vyema mijadala moto wakati wa nguruvi Kichuguu Mag3 na wadau wengine ulikuwa mtetezi mkubwa wa CCM.
Siyo uongo hata kidogo.

Nimeitetea CCM wakati wote nikiwa na matumaini makubwa yenye tija kwa Taifa.

Nimesimama kwenye kuikampeinia CCM miaka yote hata nimewahi kuwa wakala wake kwenye chaguzi mbalimbali.

Lakini sikuacha kupitia vikao vya ndani kutoa maoni yangu kama haya ya leo.

Sidhani kama napaswa kuwa mpinzani ili kuikosoa CCM.

Kama chama hakitajisahihisha basi ni vyema wapigakura wakaiokoa nchi isiendelee kuzama zaidi.

Wapinzani ni Watanzania na wapo kisheria, tupambane nao kisera na siyo ugaidi wanaofanyiwa na dola kila kukicha
 
Wapinzani ni Watanzania na wapo kisheria, tupambane nao kisera na siyo ugaidi wanaofanyiwa na dola kila
Aina ya upigaji wa kura ambao kwenye vituo vya kupigia kura unakutana na watu waliobeba mabegi yaliyo jaa
 
Nimekuwa naipinga sana CHADEMA kwa sababu ya uCCM wangu.

Lakini kwa hizi pilika zinazofanywa na serikali kukandamiza wapinzani kwa sababu ya kulinda uozo wetu zinanipa mashaka kuwa CCM ndo imekuwa inashika dola na siyo kuongoza dola.

1.
Ukikosana na kipngozi wa CCM jiandae kupambana na polisi

2.
Ukimkosoa kiongozi wa CCM jiandae kupambana na polisi

3.
CCM tunalindwa kwenye joggings zetu lakini wewe mpinzani thubutu yako uone cha moto

4.
CCM tunafanya mikutano ya ndani na nje tukiwa na bonus ya ulinzi. Lakini upinzani hata bango la kikao cha ndani ni ugaidi

5.
CCM inaajiri watu wa dola kwa kazi za ndani ya chama. Lakini ole wao watakaoenda kuajiriwa upinzani wataitwa magaidi

6.
Sheria ya vyama vingi imekataza waajiriwa wote wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya ama kushiriki siasa, lakini tuna mabrigedia, majenerali na watu wengi wa usalama kwenye political apointees kama wakuu wa wilaya na mikoa na hata wengine kupata vyeo ndani ya chama...

7.
Kwenye michakato yetu CCM ya kura za uteuzi wa wagombea, nimeshuhudia kila kitu kinaratibiwa na wavaa viatu, lakini upinzani hawapati msaada wowote kutoka huko kwenye teuzi zao.

Haya ni machache kati ya mengi yanayohusu ndoa kati ya vyombo vyetu vya usalama na CCM.

Hii ndoa inapoelekea ni kwenye MAPENZI UPOFU. Hii ni hatari sana kwa Usalama na ustawi wa Taifa. Hivyo tumefikia mahali kwamba

1.
CCM tumezalisha ukoloni mpya

2.
CCM imeleta nchini ubaguzi baina ya raia wa nchi hii

3.
CCM imegeumaa kuwa kichaka cha majambazi ya mali za umma na wabadhirifu

4.
CCM imegeuka kuwa kichaka cha wahalifu kwa sababu haichukui hatua zozote dhidi ya watu hao na sana sana wanapewa vyeo.

Ni vizuri sana endapo chama hiki kikongwe kitabadilika au kiondolewe madarakani kupitia sanduku la kura.
View attachment 1964784
Cc YEHODAYA, USSR, magonjwa mtambuka, Crimea njoen huku.
 
Siyo uongo hata kidogo.

Nimeitetea CCM wakati wote nikiwa na matumaini makubwa yenye tija kwa Taifa.

Nimesimama kwenye kuikampeinia CCM miaka yote hata nimewahi kuwa wakala wake kwenye chaguzi mbalimbali.

Lakini sikuacha kupitia vikao vya ndani kutoa maoni yangu kama haya ya leo.

Sidhani kama napaswa kuwa mpinzani ili kuikosoa CCM.

Kama chama hakitajisahihisha basi ni vyema wapigakura wakaiokoa nchi isiendelee kuzama zaidi.

Wapinzani ni Watanzania na wapo kisheria, tupambane nao kisera na siyo ugaidi wanaofanyiwa na dola kila kukicha
Miaka 30 bado ulikuwa una matumaini na CCM?
 
Tatizo kubwa ni wanaCCM wenzangu waliojazana vyama vya upinzani wakiwa na lengo la kudhoofisha vyama hivyo.

Hawa wanaorudi siyo kwamba wameona sera za CCM zimebadilika bali wanarudi nyumbani.

Siyo dhambi endapo upinzani utaamua kupeleka vijana wao CCM kwa lengo lile lile tunalolifanya sisi
Wewe una unasaba na CCM?
 
Back
Top Bottom