Ndio maana hupati kazi achana na CV tengeneza Portfolio

Festo Andrews

Senior Member
Apr 1, 2022
103
154
Habari wana JF
Hope mko poa wote, leo nimeandaa hii thread itakayokuelezea umuhimu wa kuwa na portifolio badala ya kuwa na CV kwenye kutafuta kazi mbali mbali
Kwanza kabisa inabidi utambue ya kuwa Ukishaingia kwenye soko la "What You Know" badala ya "Who You Know" kuna baadhi ya concept unakuwa unakutana nazo zinakuwa na changamoto sana mfano neno portfolio binafsi mimi lilikuwa linanichanganya sana kuliko kitu chochote lakini baada ya kufwatilia kwa undani
Nikawa nimegundua Portfolio ni nini na inatofautiana vipi na CV na huwa inatengenezwaje.

Binafsi naamini wengi wetu tumekuwa tukihangaika kuelewa:

✅ Portfolio ni nini hasa?

✅ Inatofautianaje na CV?

✅ Na kwa nini inahitajika sana siku hizi wakati wa kutafuta kazi
20250324_133007.jpg
Leo nakupasulia jipu kimasta!
Nimeelezea tofauti yao kwa undani, nikitoa mifano halisi, na hata kukupatia baadhi ya sites unazoweza kutumia kutengeneza portfolio yako bora kulingana na skill au profession ambayo upo nayo na incase ikitokea haipo utakuwa umepata njia atleast njia ya kujua wapi utaanzia.

Sasa tuanze na CV kwa ufupi Je CV ni nini?

Curricullum Vitae au CV ni kama story au hadithi unayoeleza kuhusu ujuzi na uzoefu wako juu ya kitu fulani ambacho ulikifanyaga kipindi cha nyuma huko.

Ila Portfolio sasa yenyewe ni ushahidi unaoonesha kile unachoweza kufanya juu ya kazi fulani Sijui umenielewa vizuri?

Au ngoja niiweke kwa kutumia huu mfano mdogo hapa chini;

CV ni kama menu ya mgahawa ambayo inaorodhesha kila chakula kinachopatikana na Portfolio ni sahani ya chakula halisi inayoonesha uhalisia wa ladha na muonekano wa kile unachopika.
20250324_133449.jpg
Huu ni mfano wa CV
20250324_133451.jpg
Huu ni mfano wa Portifolio
Hivyo sasa kwa maisha ya sasa hivi na experience niliyoipitia waajiri wengi wanapokagua waombaji wa kazi, hawataki kusoma tu "menu" (CV), bali huwa wanataka kuona na kuonja chakula chenyewe yaani waione Portfolio yako

Sasa Kwa Nini Portfolio Ni Muhimu Kuliko CV?

Kama unatafuta kazi kwa kutegemea CV pekee, basi unakuwa na silaha moja tu kwenye vita vya ajira. Lakini ukiwa na portfolio, unakuwa na ushahidi wa vitendo kwamba unaweza kufanya kazi unayodai unaijua na una sampuli ya vithibitisho.
Na hii ndiyo sababu portfolio ni game changer kwenye ajira za sasa:

✔ Waajiri huwa wanataka kuona kazi yako, siyo kuisikia tu.
✔ Inaongeza nafasi zako za kushindana sokoni.
✔ Inakupa mamlaka zaidi ya kudhibiti first impression yako.
✔ Inapunguza mashaka ya waajiri.

So, Kwa kifupi: CV itakusaidia zaidi kupata interview kwenye kazi uliyoomba ila probability ya kupata kazi inakuwa sio kubwa sana ( sijasema hupati kazi kabisa) , lakini portfolio inaweza kukuhakikishia unapata kazi asilimia zaidi ya 90%

Portfolio mara nyingi huwa inategemea kazi yako sana sana na matokeo yaliyopatikana baada ya kufanya hiyo kazi. Kuwa tu na portfolio haitoshi ila inatakiwa iendane na kazi yako uliypifanya na unayoiomba effectively.
Kwa mfano wewe ni Programmer au Developer
Badala ya kuandika tu "Nina uzoefu wa miaka 3 kwenye Python na JavaScript au CSS",

Onyesha real-world projects zako kwenye site kama GitHub au kwenye website yako mwenyewe pia tengeneza live demos au eleza changamoto ulizotatua kwenye projects zako.
20250324_145024.jpg

Kama unajua mambo ya Graphics design & UI/UX Designers badala ya kusema tu najua kutumia software za Photoshop, Illustrator, Canva na Figma kama unavyoandika kwenye CV huku unatakiwa uoneshe kazi zako kwa kutumia website kama Behance, Dribble, Pinterest au website yako binafsi.
Pia, Hakikisha portfolio yako ina muonekano wa kitaalamu na inaonyesha diversity ya kazi zako
20250324_145343.png

Au unakuta mtu unasema wewe ni "photographer", lakini hakuna hata picha moja uliyowahi post umepiga hapo utakuwa unazingua ikiwezekana hizo picha zipost Instagram, 500px, au Behance utapata wateja tu taasisi zitakutafuta.

Kumbuka " No matter your profession, a strong portfolio makes you stand out! Bro

Nicheki whatsapp wa.me/255765772976 kwa ajili ya tips zaidi
Natumaini umepata kitu haujatoka bure
Uwe na mchana mwema 🙏
 

Attachments

  • 20250324_133449.jpg
    20250324_133449.jpg
    123.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom