Ndg Rais Magufuli Yakupasa Ku Subsidize Kilimo

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,143
3,222
Ndugu Rais kama mwananchi ningependa tujadili hili, hasa hili swala la kilimo. Ila kabla ya yote ningependa kukupa pongezi za juhudi zako unazoendeleza ktk ujenzi wa Taifa hili changa, wenda lenye watu wachanga pia.

Kuna msemo unasema, ukitaka kukamua maziwa mengi mlishe ng'ombe wako vizuri. Sasa ng'ombe ktk taifa hili ni wananchi, na kwa vile wananchi wengi wanategemea kilimo, sasa yapaswa kuwalisha vizuri kwa serikali ku subsidize kilimo.

Mfano, Serikali inaweza tenga mikoa 20 na kila mkoa kuupa bilion 10 zijengwe miundo mbinu ya irrigation systems, na kisha kumkabidhi mwendeshaji, kama ilivyo serikali kununua ndege na kuwakabidhi wengine wazi run. ukianza kwa mikoa hiyo 20 kisha awamu inayofuata unakamilika mikoa yote kuwa na atleast kila mkoa una mashamba makubwa yanayozarisha mazao mda wote na kwa wakati wote.

Kuendelea kutegemea mvua ndo kilimo kifanyike nafikiri ndoto zetu zakuwa na maisha ya kati zitakuwa ndoto zakufikirika. Huyu ng'ombe (mwananchi)aliyekonda siku zote atakukuruka ili apate kuishi. Waswahili wanamsemo unasema, hakuna binadamu aliye na ustaarabu mwenye njaa.

Hivyo, nafikiri japo unaendelea na mkakati mingine ya miundo mbinu na viwanda. Lakini kiwanda cha irrigation kilicho rahisi nafikiri tumekisahahu. Hiki nikiwanda murua kabisa ambacho tukizarisha mazao tuta export kwa jirani zetu na kuimport $$$$ na kisha ku stabilize uchumi. Ni maoni yangu.

Sasa hatua ya awali hii swala linawezekana na lipo ndani ya uwezo wa serikali, Mungu katupendelea tuna maziwa na mito mingi wenda kuliko nchi yoyote africa, tuna ardhi arable land nzuri tu. Cha kufanya ili twende ktk uchumi wa kati, ni kumpunguzia pressure mwananchi, kwa kuwezesha kilimo ambacho kinafanya chakula kuwa available ana affordable. Hyo inamuongezea mwananchi purchasing power na namna yakufikiri ktk maendeleo mengine ya kwake na taifa , badala ya kila siku mwananchi kufikiri jioni atakuwa je chakula.
 
Hata nchi mfano za ulaya, ni zime subsidize ktk kilimo na nyaja zingine. Hapa sisemi kuwapa mbolea wananchi tu, hiyo haitoshi kwa sababu wataweka mbolea na mvua hainyeshi.
 
Mkuu kasema hataki kushauriwa, anajua kila kitu. Acha tu utaitwa mchochezi
 
Mkuu kasema hataki kushauriwa, anajua kila kitu. Acha tu utaitwa mchochezi
Ushauri anapenda ila hataki nafikiri kumlazimisha ushauri ama maoni yako ayafanyie kazi.

Kilimo inabidi Rais akiangalie kwa jicho la pekee, ni eneo ambalo halina ushindani kabisa ktk maeneo ya afrika.
 
ngoja kwanza tumalize kupanga na kupangua....Tutakusikiliza
 
Bei ya bombardier moja angejenga bonge la irrigation scheme kule RUBADA angetengeneza bonge Shamba la mpunga na kungekuwa na bonge faida halafu mi angeniajiri kuamia au kufukuza ndege wasile mpunga.
 
Mkuu kasema anachukia mitandao please mwandikie barua ila ukitaka ufanikiwe ipitishe kwa bashite
 
Namimi nainyoosha nchi huku mitandaoni magogon yupo yeye nae anainyoosha kivyake Sasa kwa pamoja ngoja tuivunje halafu tunyooshane atakaepona kati yangu na yeye atalea kizazi atachoacha mwenzie
 
Kwasasa ardhi imeshikiliwa kiholela, wapo speculators, wapo wakulima wadogo wadogo. Bila kuhakiki ardhi na kujuwa nani ni nani, hiyo hela itaishia mifukoni mwa wakulima wajanja tu. Let's know who is who, na nani ana ekri ngapi. Tunahitaji wakulima serious ambao wanamipango ya maendeleo kuliko mtu anajiita mkulima unampa mitambo mwisho wa siku anashindwa kurudisha chochote wala kuonyesha alichokifanya.
 
Mkuu huu unakuwa miradi ya serikali na mashamba ya serikali, harafu unawapa watu kuyaendesha kwa niaba ya serikali kwa mkataba maalumu na kugawana faida. Maendeleo yatapatikana kwa dhati wananchi wakiwa wameshiba na kwayo ku create ajira nyingi na za uhakika
 

Mimi nakibalina na wewe kwa 100%, lakini tatizo linakuja hapo kipindi cha nyuma kulitokea wajanja wakajimilikisha ardhi na wengine kuichukia mikopo wakapote na mikopo hiyo. Uhakiki unahitajika, lakini juu ya hayo, tunahitaji wakulima wanaochukulia kilimo kama biashara, sio kama kazi ya kawaida. Wakulima wetu wengi wanachukia kilimo kama shughuli nyingine ya kawaida kama kufagia barabara. Hakuna mkukima anayefuatilia utabiri wa hali ya hewa kujuwa ni mazao gani alime mwakani, wote wanafanya kwa kudra ya Mungu. Ukame tunao ambiwa leo ulitabitia miaka miatu iliyo pita, hakuna aliye sikia wala kulima mazao yanayoendana na ukame. Wakulima wetu hawajuwi kitafuta masoko, wanategema wakala waende mashambabi huku wanapewa bei ya chini. Kwahiyo tunahitaji kuwa na wakulima walionuwia kilimo na wanojifinza mbinu mpya. Vinginevyo ruzuku tutakuwa tunaimwaga baharini.
 

Nakubaliana na wewe 100% hayo ndio matatizo tuliyanyo ktk nyanja ya kilimo. Hivyo matatizo tunayafahamu yani ya kwamba wakulima wetu hawachukulii kilimo ktk mtizamo ambao serikali ingetaka kuwa, na kwamba ni kweli kuwapa ruzuku hawa wakulima unakuwa unaongeza tatizo badala la ya kulisahihisha.

Ninachosema mimi, ni serikali ifanye kuyaendesha hayo mashamba kwa kupitia mawakala. Yani serikali itafute mashamba yake yenyewe kila mkoa, na ijenge miundo mbinu ya umwagiliaji ktk mashamba haya kisha kuwakabidhi mawakala kwa makubaliano maalumu ya kugawana faida, si lazima sana hawa mawakala wa kilimo hiki yani large scale wawe watanzania.

Serikali ni ngumu kuwezesha ruzuku wakulima wafanye large scale farming, badala yake serikali yenyewe iwezeshe miundo mbinu na i run hayo mashamba virtually. Hii ni mbinu ambavyo serikali za kibepari zinafanya kuendesha mambo ya biashara. Kwani kwa upande wa pili serikali ni ngumu kujiendesha kama inategemea kodi tu, yapaswa kufanya biashara kwa kupitia mawakala. Mfano mzuri ni mkongo wa taifa wa mawasiliano, kama serikali ingewapa ruzuku watu wachache wajenge isingewezekana, na ilichofanya ilijenga yenyewe na kuwakabidhi TTCL na faida kama wana make watakuwa wanagawana na serikali.

Serikali inge identify mazao yanayositawi kila mkoa, na kisha kupata mashamba yao watayoyajengea miundo mbinu ya umwagiliaji na kutafuta watu wanaoweza yaendesha hayo mashamba. Hii nafikiri itaongeza tija sana kwa taifa hasa ktk maendeleo, na pia litakuwa taifa lenye uimara sana tofauti na tulivyo wenda sasa.
 
Nimekuelewa, you've a point japo utakumbuka serikali kabla ya kupata hayo mashamba, wameanza na uhakiki wa ardhi kujuwa nani anamiliki nini na kuwaondowa wote wawekezaji uchwara. Mwaka wa kwanza JPM na Mzee Lukuvi wamekuwa busy kukusanya ardhi na mashamba yote ambayo hayaendelezwi na yanayo tumiwa na wajanja, pamoja na wale waliojimilikisha wakidai wao ni watanzania kumbe sio. Huu ni mwaka wa pili, mkakati wa kilimo utatolewa sio muda mrefu walishaahidi hivyo. Sijuwi huo mkakati una nini ndani yake lakini nina wasiwasi kama wanaweza kufanya kama ulivyo shauri wewe maana hapo serikali itakuwa inajiingiza kwenye biashara ambapo wao waloshajitowa na kubaki kama regularity authority tu. Tusubiri tutajuwa yaliyomo kwenye mkakati huo.
 

Hoja yako ipo sawa sana nakubaliana nayo. Pia nafikiri hilo swala la serikali kujitoa ktk biashara, nikweli walijitoa lakini nafikiri ilikuwa ujanja wa nchi za kibepari kuwalaghai kuwe na serikali legelege. Hata wao mabepari, wame subsidize kwenye makampuni mengi na mawakala wanayo endesha mashirika ya serikali kwa niaba ya serikali. Mfano lile shirika lilotuuzia radar nk.

Kinachotakiwa hapa, si serikali wao wa run haya mashamba directly bali wawezeshe mazingira infrastructures. Kama wanavyojenga barabra na kuwakabidh mawakala tanroads, bila hivyo tanroads wasingeweza kitu. Hii ni miundo mbinu ya umwagiliaji na mashamba. Ni eneo rahisi sana kushindana kikanda na kimataifa na bado tukawa wababe ktk maeneo haya.

Hii nchi tukifanya hivi tena kwa mtaji mdogo sana itakuwa bread basket kwa nchi zote za africa. Bila hivyo nafikiri tukiendelea kuwategemea wakulima traditional farmers, hii nchi tunakoenda itakuwa basket case by itself. Mvua hamna na hazitabiriki , hata ukimpa ruzuku unatafuta kumfunga tu mkulima
 
Sina uhakika kama serikali kujitoa ni kweli ikikuwa ni nguvu ya ubepari, maybe you right lakini hiyo ni nje ya mada.

Sijakataa kama ruzuku (subsidies) ni kitu muhimu, na ni kweli wenzetu wa Ulaya na Marekani wanawapa sana hela wakulima wao, mfano ni nchi za Ulaya ambapo mkulima anazalisha mazao lakini nusu ya gharama zake analipiwa na serikali kwa njia ya punguzo kubwa la kodi. Ndio maana tulikataa kusain EPA na wenzetu wa EAC kutokana wakulima wa Ulaya watatuletea chakula cha bei nafuu sana ambapo kitawanyima wakulima wetu nafasi ya ushindani.

Pamoja na hayo yote, ndio maana nikasema lazima kuwe na utaratibu na mpangilio mzima wa ardhi, JPM na team yake wameanza na uhakiki wa ardhi, kinacho fuata ni kujuwa nani mkulima wa kweli na nani mbabaishaji. Kama wanawasaidia, basi msaada unakwenda kwa watu wanaojuwa wanafanya nini. Sisi tunamatumizi mabaya ya ardhi, wenzetu walioendlea wana weza kutumia ekari kumi wakazalisha mazao ambayo sisi tutazalisha kutumia ekari mia moja kuzalisha kiwano hicho hicho. Kilimo ni sayansi, kilimo ni masoko, kilimo ni ajira. Kama vile hatumpi mtu yoyote asiyejiamini kufunguwa kiwanda au hospitali na kilimo ni hivyo hivyo.
 

Hapo umenena vyema kwenye mpangilio wa ardhi, na matumizi ya ardhi ambayo yenye tija zaidi. Lakini hapa ya kwamba kuwapa wakulima waendeleze kilimo nafikiri ndo logic yangu ina diverge kidogo, kwa sababu hawa wakulima hawajazoea hiki kilimo nachotamani na kukikongelea. Hata hivyo bado ni jambo la buheri kuwapa wakulima wenye nia ya dhati kabisa ktk kulima kibiashara.

Mimi ambacho ningependa, ni serikali kuonyesha njia kwa mfano ulio dhahiri kwa kujenga miundo mbinu hii angalau mmoja ktk mikoa yenye maji ya uhakika, palipo na maziwa kama nyasa,tanganyika, victoria na mito ya uhakika. Kisha wananchi na wakulima wengine watafuata kwa kuwazesha zaidi. Natamani serikali ifanye harafu, mwendeshaji wake apewe wakala wenda kwa usimamizi wa mkuu wa mkoa na wilaya.
 
Ndio maana nikasema tunasuburi muelekezo wa serikali, they promise mageuzi ya kilimo. I hope watachomeka kitu kama hicho unachokisema. Mwanzoni mwa mwezi huu wa March walikuwa na workshop to discuss the policy and also to get some experience from Tanzanian farmers. Lots was discussed na waka ahidi watakuja na sera mpya ya kilimo.

http://www.kilimo.go.tz/index.php/e...agricultural-policy-conference-march-1-3-2017

http://foodsecuritypolicy.msu.edu/n...ural_policy_conference_march_13_dar_es_salaam
 
Wewe ndiye uliyemchukulia form? Wewe ndiye uliyempa urais ?
hako ka KURA kako kimoja Ndio uwe mshauri wa RAIS?
Hujui Kama yeye hashauriwi? Unajua hakushauriwa kuchukua form Na akashinda uchaguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…