Ndege yatua Uhispania na abiria kamili bila mizigo yao

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
8,626
13,847
Usafiri wa ndege ni usafiri wa raha na wa haraka zaidi. Pamoja na hivyo ni moja ya usafiri wenye vituko vingi zaidi.

Wiki mbili zilizopita ndege moja huko Marekani ilibidi irudi ilikotoka baada ya abiria mmoja kuchafukwa na tumbo na kuichafua ndege nzima.

Juzi tena tarehe 11 ndege ya shirika la ndege la Switzerland iliruka kutoka uwanja wa Zurich nchini humo mpaka Bilbao nchini Australia na abiria 161 kamili lakini bila ya mzigo wowote wa abiria. Zaidi ya hayo shirika hilo la ndege lilipiga kimya bila kuwaambia abiria wao juu ya kilichotokea hivyo wakabaki wakisubiri kwenye mkanda wa kupokelea mizigo kwa saa moja na nusu kabla wafanyakazi wa shirika la ndege la Iberia la Spain walipowatobolea siri hiyo kuwa mizigo yao iliachwa walikotoka.

Shirika hilo la ndege lilikuwa likiendesha ndege za wenzao wa shirika la Edelweiss airlines. Kwa mujibu wa rubani wa ndege hiyo ambaye baadae ilibidi awaombe radhi abiria wake, alisema walibaki uwanjani Zurich kwa zaidi ya saa moja na robo kusubiri wafanyakazi wa Edelweiss airlines, wapandishe mizigo hiyo bila mafanikio. Kwa maelezo ya rubani huyo walipoona hali imekuwa hivyo ndipo ikabidi awahi kuruka kwenda Spain kwani walitakiwa wawe wameshafika huko kuchukua ndege nyingine kabla kiza hakijaingia.

1694634147309.png
 
View attachment 2748420
Hongera sana
 
unajua hiyo juzi nikijiuliza sana mbona wametuweka sana...mpk baadae kbs ndio nakuja kuzinduka na kupigwa na butwaa pale bwana rubani alipotuchana live kiukiweli nilikasirika sana ukizingatia kulikuwa na documement zangu kibao ambazo nilitakiwa kuwa nazo kwenye kikao muhimu cha Tokyo
 
Document muhimu siku nyengine usiweke kwenye mabegi ya shehena .Panda nayo ndani ya ndege.Huo ni ushamba.
Watu kama nyinyi mnaokwenda kwenye vikao wala hamchukui mabegi.Unaingia na begi dogo la mkononi mpaka kilo 8 na laptop kwenye mfuko mwengine wala huzuiliwi kuingia navyo.
 
Back
Top Bottom