Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 368
- 952
Mwezi Septemba mwaka jana CEO wa lebo ya WCB na mwimbaji wa Bongofleva, Diamond Platnumz akiongea na DW Africa alithibitisha kununua ndege binafsi (private jet) kwa lengo la kile alichoita ni kuongeza thamani yake.
Baada ya kauli hiyo, Diamond akasifiwa sana na kuelezwa kwamba angekuwa msanii wa kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kumiliki ndege yake.
Tulisikia mengi, sifa kem kem kutoka kwa wapambe wake wakiwemo akina Baba Levo ambao walisema kwamba si tu kwamba bosi wao huyo ana mpango wa kutaka kununua hiyo ndege, bali tayari amekwishainunua ila tu bado kuwasili kwa vile inamaliziwa.
Kuanzia wakati huo tunaona kimya. Tumesubiri kwa mwaka mzima lakini kimya hadi sasa. Hiyo ndege iko wapi jamani au imeishakuja kinyemela?