Mtoa Taarifa
Senior Member
- Sep 21, 2024
- 178
- 569
MABADILIKO YA RATIBA YA NDEGE
YA MUMBAI-DAR ES SALAAM
04 Novemba 2024, Dar es Salaam
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inapenda kuutaarifu umma kuwa ratiba ya leo ya safari ya kutoka Mumbai kwenda Dar es Salaam imebadilishwa kutokana na hitilafu ya kiufundi.
Kwa kuzingatia kipaumbele chetu cha usalama, abiria wote waliokumbwa na mabadiliko haya wameshapatiwa huduma stahiki na wanatarajiwa kurejea nchini kesho.
Ndege hiyo inatarajia kuendelea na ratiba zake za Mumbai kwenda Dar es salaam kuanzia tarehe 6 Novemba, 2024.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma
Air Tanzania
+255 748 773 900 | www.airtanzania.co.tz
The Wings of Kilimanjaro