kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,808
- 20,209
Ndege isiyo na rubani ya Iran yazifukuza ndege za Marekani katika anga ya Iran
Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Iran amesema ndege isiyo na rubani ya Karrar imezionya mara kadhaa ndege za ujasusi za Marekani na ndege nyingine za kigeni na kuzitaka kuwa mbali na anga ya Iran.
Brigedia Jenerali Alireza Elhami alisema jana Jumapili kwamba ndege hiyo isiyo na rubani mara kadhaa imezilazimisha ndege za kigeni zenye watu na zisizo na rubani kubadili mkondo wao kwenye Ghuba ya Uajemi, Mlango Bahari wa Hormuz, na Bahari ya Oman.
Kamanda huyo amesema, baadhi ya ndege za kijeshi za kigeni zilitaka kujaribu uwezo wa ulinzi wa anga wa Iran kwa kubadilisha mwinuko wa safiri zao, bila kujua kwamba Karrar, ambayo imetengenezwa kikamilifu na wataalamu wa ndani, inaweza kuruka juu yao.
Elhami pia amebainisha kuwa Karrar imewekewa mfumo wa kisasa wa rada.
Droni ya Karrar, iliyotengenezwa na Kampuni ya Viwanda ya Kutengeneza Ndege ya Iran (HESA), ni miongoni mwa kizazi kipya cha zana za anga za jeshi la Jamhuri ya Kiislamu iliyoundwa kuzuia vyombo vinavyoruka vya maadui kuingia katika anga ya Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amekuwa akitoa wito wa kufanyika juhudi kubwa za kudumisha na kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa Iran.