Nimeona clip, (nitajaribu kui-upload) Waziri Muhongo akimkaripia Mkurugenzi wa NDC kwa kutotumia kichwa chake vizuri.
Inasikitisha, jamaa anshindwa hata kujieleza vizuri, mradi wa makaa unaendaje .
Halafu jamaa amejifutika masuti na matai, waziri imebidi amwambie hayo masuti na tai havina maana sana kama hutumii akili kutatua matatizo ya kikazi.
NDAC lilikuwa shirika lililokuwa mbele sana katika kubuni, kujenga na kuwekeza kwenye miradi kwa niaba ya serikali.
Kwa watu walioonyeshwa kwenye clip hiyo, watu hao inaelekea hakuna tena, wamebaki magharasha walio tengenezewa ajira kiulaini.
Huu ni uozo, mbaya Zaidi ya jipu.