I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,900
- 10,667
Muasisi wa nchi yetu mwalimu Nyerere aliwahi kugusia jambo kwenye moja ya hotuba zake wakati akielezea ni jambo gani kubwa inaweza kupelekea nchi kupata maendeleo, alisisitiza sana swala la demokrasia; lakini kwa bahati mbaya hata ndani tu ya chama cha CCM sasa miaka hii hakuna hiyo demokrasia.
nanukuu
"Maendeleo makubwa ya nchi ni kuendeleza demokrasia na si mfumo unaoiendesha"
-Je, hii demokrasia ipo kweli ndani ya chama, au anachoamua mwenyekiti ndicho hichohicho kimeshapitishwa?, kuna wa kupinga au kutoa maoni mbadala? Au mmekubaliana tu kutunga zaburi kwa ajili ya kumtukuza boss kwa yote heri?
Miaka ya hivi karibuni ni kama wanaccm wanapimana nguvu wao kwa wao ndani ya chama, na katiba yao haina nguvu sana kwa sasa. Ni jambo zuri.
"Upinzani wa kweli na mpinzani wa kweli atatoka ndani ya CCM na kwamba bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba."- Nyerere
Yaani fukuto tu. Yeyote atakayejitokeza kuhoji chochote kilichoamuliwa na system, anashughulikiwa mapema tu.
Sasa kama katiba yao wenyewe wanaibinya kulingana na matakwa na faida ya watu wachache itakuweje katiba ya nchi?
"Ni demokrasia gani inayozuia wananchi wake kuihoji katiba yake au sheria nyingine yoyote ya nchi?." Aliuliza Nyerere na kuongezea;
"Demokrasia ikichukua sura ya udikteta, udikteta wenyewe utakuwa na sura gani?
Kama nchi tunahitaji mageuzi makubwa sana ili tuendelee. Vinginevyo, hatufiki kokote zaidi ya kutoleana sifa za uongo.
"Kila mageuzi makubwa huhitaji kiongozi mwenye uwezo na anayekubalika na kuaminiwa na wananchi"- Nyerere
::Sasa swali kwenu wawakilishi wa wananchi wengine nje ya JAMIIFORUM Je, mnamkubali na kumuamini kiongozi wenu anayewaongoza kuelekea mageuzi ya kimaendeleo kwenye nchi yenu?