Nchi za Saudi Arabia, Bahrain, Sudan na Jumuiya ya Milki za Kiarabu (UAE), zavunja uhusiano na Iran

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,432
8,140
Saudi Arabia imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Iran na huku kukiwa na hali mbaya ya mvutano kufuatia utekelezaji adhabu ya kifo kwa mhubiri maarufu wa dini ya Kiislamu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Saudia, Adel al-Jubeir, ameishutumu serikali ya Iran kwa kusambaza silaha na kuanzisha jela na kuwafunga watu wanaodhaniwa magaidi katika ukanda wake .

Waziri huyo amesema wanadiplomasia wa Iran wanatakiwa kuondoka Saudia ndani ya saa arobaini.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, waandamanaji mjini Tehran waliuvamia ubalozi wa Saudia mjini Tehran, huku wakilaani utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine 46.

Watu hao waliouawa inasadikiwa walikuwa na hatia ya makosa yanayohusiana na ugaidi.
Kiongozi mkuu wa Iran alimweleza Sheikh huyo kama shahidi ambaye alikuwa akitetea amani na kufanya maandamano ya amani.
==============



==============

UPDATE


Washirika kadha wa Saudi Arabia wamejiunga na taifa hilo katika kuvunja uhusiano na Iran huku mvutano ukizidi kuhusu kuuawa kwa mhubiri wa Kishia.

Mataifa hayo ni Bahrain, Sudan na Jumuiya ya Milki za Kiarabu (UAE).

Saudi Arabia ilikuwa imewapa wanabalozi wa Iran siku mbili kuondoka nchini Saudi Arabia kufuatia mvutano uliotokana na kuuawa kwa mhubiri maarufu wa Kishia.

Bahrain, ambayo hutawaliwa na Mfalme Msuni lakini raia wengi ni wa dhehebu la Shia, nayo ilifuata wa kuvunja uhusiano.

Ufalme huo pia uliwapa wanabalozi wa Iran saa 48 wawe wameondoka nchini humo.

Sudan nayo ilimfukuza balozi wa Iran kutoka Khartoum huku UAE nayo ikipunguza idadi ya maafisa wa ubalozi. Waislamu wengi nchini Sudan ni Wasuni.

Taarifa ya wizara ya ammbo ya nje ya Sudan imesema: "Kufuatia mashambulio ya kikatili dhidi ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran na afisi yake ya ubalozi Mashhad... Sudan inatakaza kwamba imevunja uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Mhubiri huyo Sheikh Nimr al-Nimr aliuawa pamoja na watu wengine 46 baada ya kupatikana na makosa yanayohusiana na ugaidi.

Washia walishutumu hatua hiyo na maandamano yalishuhudia maeneo yenye Washia wengi.

Mjini Tehran, waandamanaji waliteketeza majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia.

Saudi Arabia na Iran ndiyo mataifa makuu ya Kisuni na Kishia mtawalia Mashariki ya Kati, na yamekuwa yakiunga mkono pande pinzani katika mizozo inayoendelea Syria na Yemen.

Kuna wasiwasi huenda machafuko yakatokea kanda hiyo.

Jumatatu, misikiti miwili ya Wasuni ilishambuliwa na imam mmoja akauawa.

Saudi Arabia ilitangaza kwamba imekatiza uhusiano wake na Iran baada ya maandamano yaliyotokea ubalozi wake mjini Iran. Ilisema pia kwamba imemwagiza balozi wake arejee nyumbani.

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema Saudi Arabia inaendeleza sera ya kuzidisha chuki na makambiliano katika kanda hiyo.

Msemaji wa wizara hiyo Hossein Jaber Ansari alisema Jumatatu kwamba Saudi Arabia inajaribu kusuluhisha matatizo yake ya kinyumbani kwa “kuyatoa nje kwa mataifa mengine”.


Chanzo: BBC Swahili
 
Last edited by a moderator:
Sheria za saudia nazipenda sana kama mtu akifanya ujinga unaadhibiwa kijinga safi sana saudia ugaidi siyo wa kuchekea hata kidogo.
 
ugaidi hautaisha mpaka pale ufalme wa saudia utakapodondoka,na ni kazi ngumu kwelikweli!

saudia arabia ni nchi ya tatu kwa?matumizi ya kijeshi duniani,baada ya marekani,na china kama sikosei!


bado wana mkataba wa ulinzi na marekani,ukiigusa saud unastukia marekani huyu hapa
 
Na bila kusahau Saudia ndio iliyofadhili mradi mzima wa Bomu la Nuclear wa Pakistan kwa makubaliano kuwa Saudi atapatiwa Bomu kwa ajili ya kulitumia pale atakapozidiwa kijeshi kwenye vita.
 
vita kati ya saud na iran inazidi kunukia,hasa baada ya iran kuzuia njama za saud na washirika wake kumtoa assad wa syria!
marekani atakua upande wa saud,huku Russia akiwa upande wa iran,itakua noumer sana
 
pakistan imekua ikijaribu kujinasua toka katika makucha ya saud arabia,ila saud wana hela inakua ngumu sana
 

We nilishakutsukia ni SHIA
 
mimi sunni bana,ila penye haki ukweli usemwe,saud wanajidanganya kama uislam ni mali yao,na wanataka dunia yote wawe wahabiya kwa lazima
 
Shiite brother wanaungana mkono hata kama kama mtu ni criminal....

Waliouwawa pale na makosa ya Ugaidi ni 47 na 46 kati yao ni SUNNI lakini huyo Shia mmoja tu basi Ulimwengu wa Shia MACHOZI yanavyowatoka na MAPOVU sasa kama halikuwa na makosa ya kuwa Excuted aachwe kisa ni Shia?

Iran kwa mwaka inauwa watu wangapi Raia wake kule?? kwa makosa mbali mbali Mbona Hakuna anayekuja na kulialia?

Ukifanya ushenzi unakula Panga tu..
.
 
mimi sunni bana,ila penye haki ukweli usemwe,saud wanajidanganya kama uislam ni mali yao,na wanataka dunia yote wawe wahabiya kwa lazima

Huu mjadala wa Uwahabi ni mzito sijui kama unaweza kuukabili.....na JF watafuta Thread ikiwa tutaenda huko

maana uwahabi ni Myth japokuwa imeshapachikwa kuwa watu kadhaa wa kadhaa ni wahabi....

Kuna vijana wanaweka Exlposives katika misikiti ya Shia huko Saudi Arabia ( vijana wa kundi la Isis) na wote wamo mbaroni walidakwa karibu 300 na mitambo na mabomu ya kujilipua....

Watu kama hawa Wakiuwawa ni Makosa? na hao Shia je hawaoni kama kuwaondoa hawa vijana wenye fikra za Takfiri juu yao ni usalama wao?

Maana tuangalie mbali UHASAMA WA SAUDI NA IRAN ni zaidi ya Hizi saisa wako katika Suala la Kiimani zaidi....
 
Hawa Saudi na Iran mpaka sasa wanapigana proxy war Syria na Yemen..


Yemen Iran anawapa support Houthi rebels huku Saudi anaipa support serekali iliyopo madarakani

Tukirudi Syria tunaona Saudi inawapa support waasi huku Iran ikishirikiana na Hezbollah' na Russia wanampa support raisi wa Syria

Hapa wanao umia kaatika huu ugomvi wa hawa middle east giants ni wananchi wanaopata madhara ya vita syria na yemen

Lakini hivi sunni na shia wanamatatizo gani mpaka hawapendani kiasi hiki??au ndo kama mdau hapo juu alivyosema huu in ugomvi wa ki historia.
 

Shia na Sunni hawawezi kuelewana ni Historical Thing....ni suala la Itikadi

Na nikwambie kitu...katika watu wako very against Itikadi za kishia ni Sunni (Ahlu sunnah) wengine wanawaita Wahabi, wengine Salafi

hili gogoro ni changa la macho kuna SUALA LA ITIKADI ZA KIDINI NYUMA YAKE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…