Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,204
- 3,277
Ukisoma maoni ya watu mitandaoni hapa Tanzania , na mitandao ya kimataifa, hasa vyombo vya habari vya kimataifa, utaona watu kadhaa wanalaumu kwanini nchi za Kiarabu/Kiislam haziingilii vita ya Palestina na Izrael kijeshi ,kwanini viongozi wa Kiarabu hawaingilii mgogoro wa Izrael kijeshi.
Mimi binafsi naunga mkono nchi za Kiarabu/Kiislam kutoingilia kijeshi , kwanza tufahamu kuwa Izrael ni jimbo la 53 la Marekani kwa kuwa Wayahudi wengi wana Uraia wa Marekani na Uingereza, hivyo ukiwagusa umegusa wananchi wa Marekani. Ukimpiga Izrael, utapigwa na Marekani, utapigwa na Uingereza. Ndio maana baada ya shambulizi la Hamas lililoua Wayahudi 1200, manowari na Zana za kivita za Marekani zilisogea bahari ya Mediterania zikiwa tayari kulinda jimbo la 53 la Marekani
Kwanini Waarabu wanatakiwa kutoishambulia kijeshi Izrael?
Changamoto kubwa ya nchi za Kiislam, ukiongelea kitabu chao cha dini, umeongelea Siasa,hivyo huwa inakuwa changamoto kubwa kwao kuingia vitani pale ambapo utawala ukilega kwa sababu ya kivita, tayari makundi ya kidini yanaibuka. Mfano, leo hii Iran au Misri ikiingia vitani na Izrael, kwa vyovyote vile Marekani na Izrael wataishambulia Irani au Misri. Ikitokea serikali ya Iran imepigwa na kukosa nguvu, tayari makundi ya Kiislam yataingia kati na kutaka utawala wa Sharia, wataanza kuuwana wao kwa wao, imani kali zitaingia kati, Sunni atavaa bomu atalipua Shia msikitini, Makundi ya hitikadi kali a. k. a Mujahidin yataingia hapo. Hii tumeona Talban huko Afghanistan , ISIS Syria, Iraq, Libya. Al Shaabab Somalia, Boko haram huko Nigeria, na Makundi kadhaa West Africa
Hivyo, ili kulinda mataifa ya kiarabu/Kiislam yasisambaratike, kuivamia Izrael kijeshi sio option