Nchi za Afrika zimehimizwa kujifunza toka kwa China ili ziweze kupata maendeleo ya kasi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,099
1,095
1724914020083.png

Maendeleo ya kasi ya kiuchumi na kijamii ya China, yamekuwa ni mambo yanayojadiliwa kwa kina na wasomi wengi duniani, ikiwa ni pamoja na wale wa nchi za Afrika. Moja kati ya mambo ya msingi yanayotajwa kuwa ni kiini cha maendeleo hayo ni njia ya China ya kujiletea maendeleo, ambayo wataalam wa mambo ya uchumi wanasema kama nchi za Afrika zikiiga uzoefu wa China zinaweza kujiletea maendeleo ya haraka.

Watu wengi wanaofuatilia siasa za kimataifa watakuwa wanajua kuwa China ni nchi iliyofanya muujiza wa kiuchumi duniani, kwanza kwa kujitoa kwenye lindi la umaskini la miaka ya 70 na kuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani, na pili ni kutoka jamii iliyokuwa nyuma kimaendeleo na kuwa jamii ya kisasa ambayo msingi wake mkubwa ni sayansi na teknolojia.

Kwa nchi za Afrika ambazo kwenye miaka ya 60 kiwango chake cha maendeleo hakikuwa mbali sana na kile cha China kwa wakati ule, China sasa imekuwa na mfano hai wa jinsi ya kuondokana na umaskini. Wataalamu na wasomi mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu mambo ambayo nchi za Afrika zinaweza kuiga kwa China ili ziweze kujiletea mabadiliko ya haraka. Profesa Waithaka Niraki wa Chuo Kikuu Cha Nairobi amesema, ameitaja njia ya maendeleo ya China kwa ni njia ambayo kama nchi za Afrika zitafuata baadhi ya mambo yake ya kimsingi zinaweza kupata maendeleo ya haraka.

Njia ya maendeleo ya China ina mambo mengi, lakini kilichopewa mkazo na Profesa Waithaka ni uongozi imara wa nchi, ambao unatoa kipaumbele kwa maslahi ya umma na kuweka msukumo kwenye mambo yote ya maendeleo ya nchi. China chini ya uongozi wa chama cha kikomunisti, imetoa kipaumbele katika kuendeleza miundo mbinu, teknolojia na hata viwanda. Usimamizi mkali wa chama kwenye mambo hayo matatu, umetoa msukumo mkubwa kwa maendeleo yaliyopo sasa kwa China.

hasa kwenye maswala ya uongozi.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Kenya Profesa Becky Ndeto, yeye anaona kuwa sera zilizotekelezwa na China baada ya kuanza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, zimekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Tofauti kubwa iliyopo kati ya China na nchi za Afrika, ni kuwa China ilianza kufanya mageuzi tangu mwishoni mwa miaka ya 70, na mpaka sasa mageuzi yanaendelea hatua kwa hatua. Nchi za Afrika zimekuwa zinasita kufanya mageuzi au zinakosa msingi na ujasiri wa kufanya mageuzi ili kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hali hii imesababisha kukosa uwiano kwenye maendeleo ya uchumi na kijamii, au hata kukosa maendeleo kabisa na wakati mwingine kurudi nyuma.

Profesa Ndeto amesema uzoefu wa China unatoa somo muhimu kwa nchi za Afrika kuhusu kutumia uwekezaji wa kigeni, maendeleo ya miundombinu na kuendeleza viwanda. Ni wazi kuwa China imekuwa ni moja ya nchi zilizovutia vya uwekezaji mwingi kutoka nchi za nje, hii ni changamoto ambayo nchi nyingi za Afrika zinakabiliana nayo kwa sasa. Uvutiaji wa uwekezaji kutoka nje umekuwa na mchango mkubwa katika kuifanya China iwe moja ya nchi zenye maendeleo makubwa ya teknolojia na viwanda duniani.

China imekuwa ikisema mara nyingi kuwa maendeleo yake yana manufaa kwa watu wote duniani, kwa upande wa Afrika kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha kuwa China ina dhamira ya dhati ya kuhimiza maendeleo katika nchi za Afrika. Eneo la ujenzi wa miundo mbinu ni moja ya maeneo ambayo karibu yamegusa nchi zote za Afrika, na teknolojia kutoka China inaendelea kuingia polepole barani Afrika. Bila shaka nia ya kujifunza kutoka kwa China inaonekana katika nchi nyingi za Afrika, hata hivyo safari ni ndefu.
 
View attachment 3081869

Ni kweli lakini tumeshachelewa
 
China na nchi nyingine zote zilizoendelea wanasimamia sheria, sisi huku tunambembelezana na kulindana sana

Magufuri alisimamia sheria tukaanza kulia lia, akafa tukashangiria tunapaswa tuombe msamaha sana, tulikosea

Hiyo ndio ilikuwa njia pekee ya kutuinua kiuchumi

Huyu Mama anatupoteza, ni mlaini na mpole mnoooo hamuwezi kupata maendeleo namna hii
 
Back
Top Bottom