Nchi ya Tanzania itafanikiwa endapo 90% ya Wananchi watakuwa wamepata elimu na kujifunza nidhamu ya kufuata sheria

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,854
3,532
Ndugu zangu Watanzania napenda kuwaeleza kuwa matatizo ya Tanzania yanasababishwa na ukosefu wa elimu (ujinga) na sio umasikini. Utajiri unapatikana hata kwa kuuza mboga endapo nidhamu ya pesa itazingatiwa

Wananchi wanapokosa elimu matokeo yake ujinga unatawala katika fikra zao na mwisho wake huleta madhara ndani ya Taifa zima

Baadhi ya madhara yanayosababishwa na ujinga ni umaskini, wivu, chuki, uchoyo, unyang’anyi, wizi, ukosefu wa utu na mengineyo mengi

Katika nchi ya Tanzania umasikini unaweza kuondoka kabisa kuliko tunavyofikiri, naweza kusema hivi kwasababu watu wengi wanaweza kufanikiwa lakini ujinga kati yao ukawa ukuta wa mafanikio yao

Naweza kutoa mfano kidogo katika familia anaweza kuwepo mtu mwenye uwezo mkubwa wa fedha lakini wivu ndani yake ukamzuia kuwasaidia ndugu zake ama ndugu zake wasiokuwa na uwezo wakawa na wivu juu yake kwamba kwanini amefanikiwa kwahiyo katika case kama hii tayari ukosefu wa elimu (ujinga) unatawala ndani ya hii familia kwahiyo matokeo yake familia nzima inaishia kuwa masikini wa kutupa

Ujinga mwingine unaosababisha umasikini ndani ya nchii hii ni utomvu wa nidhamu kwa watu wanaosaidiwa, maana kwamba mtu anasaidiwa lakini matokeo yake anaharibu msaada aliopewa pamoja na kumkosea aliyemsaidia,
Katika case hii watu wanasaidiwa pengine kwa kupewa kazi lakini mwisho wanaharibu kazi wanazopewa aidha kwasababu ya uzembe, wivu, chuki, wizi, dhuluma bila kujua madhara ya kazi kuharibika ni kuzidi kukumbatia umaskini ndani ya maisha ya waliosaidiwa badala ya kuondoka

Ujinga unaotafuna inchi ya Tanzania ni kuajiri viongozi wajinga wasiokuwa na sifa za kuwa viongozi bora ambao wanatumia madaraka yao kuharibu nchi badala ya kujenga, baadhi ya viongozi hao wanaharibu nchi ya Tanzania kwa kutokuwajibika kwa hiyari pasipo amri ya raisi, kula fedha za miradi mbalimbali, kutokuwa makini katika kukagua ujenzi wa miundombinu, kutokupangilia nchi katika muonekano wa kueleweka hasa uzembe katika mipango miji nchi kuwa katika mpangilio mbovu pasipokujulikana tofauti kati ya barabara za vyombo vya moto na watembea kwa miguu, kutokuadhibu wananchi wanaoharibu miundombinu,

Ili inchi hii ifanikiwe wananchi wake wanapaswa kupata elimu (kusoma) ili wafungue upeo wa kufikiri ambao utawasaidia kuondokana na matatizo yote yanayosababishwa na ujinga

Kufanikiwa kwa nchi ya Tanzania ni ndani ya miaka 20 tu endapo itafanikiwa kutokomeza kabisa ujinga uliopo kwa baadhi ya wananchi wake. Ili kufanikisha hili elimu inahitajika, kila mwananchi akisoma au kusomesha kizazi chake matokeo yake kitakuja kizazi cha wananchi wenye uelewa wa akili
 
Kufanikiwa ni mchakato, Wala siyo tukio la mara Moja tu.
 
Hapo kwenye kupata viongozi wajinga ndipo palipoifikisha Tanzania tulipo.wewe fikiria tu mzee kibao alitekwa mchana kweupe na rais kujifanya kuunda tume uchwara ambayo hajatupa majibu Hadi Sasa miezi zaidi ya mitatu.Hii inaonesha namna tulivyo na viongozi wajinga ambao hawakustahili kupewa ofisi za umma
 
Hapa tutachelewa sana kufanikiwa
 
Back
Top Bottom