IAMswaggstatic
Member
- Apr 23, 2012
- 76
- 71
Martin Maranja Masese,
.., nchi nyingi barani Afrika sasa zinakumbwa na ombwe kubwa la uongozi.., tabaka la uongozi halina viongozi.., mataifa yamebaki na watawala.., na watawala waliopo wameamua kutawala kwa misingi ya matakwa yao siyo katiba tena.., mataifa mengi sasa barani Afrika hayana viongozi tena..,
Kuna kauli maarufu sana inasema; 'ukitaka kuongoza chagua kuongoza na watu, ukitaka kutawala, chagua kutawala pekee yako'
Umewahi kujiuliza kwanini watawala wengi wa nchi za Afrika wamekuwa ving'ang'anizi sana kwenye kuachia madaraka.., wamekuwa siyo waumini wa demokrasia, ingawa wanajificha kwenye kivuli cha uchaguzi ambao siyo huru na haki!!?
Hebu tazama watawala hawa baadhi, wa nchi za Afrika, walivyoamua kufanya ikulu za nchi hizo kama mali yao na urithi wao..
Teodoro Obiang Nguema (Equatorial Guinea) ametawala miaka 36, Jose Eduardo dos Santos (Angola) ametawala miaka 36, Robert Mugabe (Zimbabwe) ametawala miaka 35, Paul Biya (Cameroon) ametawala miaka 32, Yoweri Museveni (Uganda) ametawala miaka 29, King Mswati III (Swaziland) ametawala miaka 29, Omar al-Bashir (Sudan) ametawala miaka 26, Idriss Deby (Chad) ametawala miaka 25...
Hapo haujataja wale ambao kwa sasa wengi wao ni Marehemu, wakikwisha kufariki mfano mfalme Haile Selassie (miaka 44), Muammar Gaddafi (miaka 42), Omar Bongo Ondimba (miaka 41)
Je, katika mataifa yao hakuna watu wengine wenye kariba ya kuwa watawala kama wao!!? Au wanahofu kwamba watakuja viongozi na siyo watawala ambao wataishi katika mioyo na nafsi za wananchi kuliko wao!!? Hofu yao ni ipi haswaa!!?
.., migogoro na maandamano yanayoshuhudiwa hivi sasa kwenye mataifa mengi duniani haswaa Afrika, imetokana na hali mbaya ya uchumi pamoja na kukosekana kwa utashi wa kisiasa wa watawala kutatua matatizo yanayowakabili wananchi wao..., wameamua kuchagua kujikimbikizia mali na siyo kutatua vikwazo lukuki kwa wananchi..
.., utawala mbaya na kuendeleo kuporomoka kwa uchumi wa dunia, ndiko kunakosababisha wananchi kuchoka na kukosa uvumilivu dhidi ya Serikali zao, na hasa vijana ambao wameendelea kujiunga na makundi ya kijihadi na yenye misimamo mikali kutokana na kukosa usaidizi na utatuzi wa kero zinazowakabili..
.., ni jukumu la kila kiongozi duniani kuhakikisha wanakabiliana na hali mbaya ya kiuchumi na kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na dunia yenye maendeleo endelevu kama malengo ya umoja wa Mataifa yanayovyoelekeza ifikapo mwaka 2030.
.., nina uhakika kwamba watawala katika nchi hizi za Afrika, wanayaona na kuyasikia yale ambayo yanayotokea sasa katika nchi zao..., lakini hawajali tena; na wanajua chanzo chake..., lakini kiburi na jeuri yao, ndiyo msingi wa mizozo hii..
Naamini hakuna kiongozi yeyote wa serikali katika nchi hizi za Afrika atakayesimama na kutamka hadharani, kwamba serikali ambayo anaitumikia haitekelezi yale yaliyo sawa kwa wananchi wake.., haiwezekani hata siki moja.., hiyo imebaki kuwa kazi ya wapinzani.., na hata wapinzani wa dola pia wengi sasa wamekuwa watu waliopandikizwa kumaliza nguvu ya upinzani dhidi ya dola...
Watawala wa Afrika sasa wanaogopa kesho yako kuliko hata kifo chao.., watawala wa nchi za Afrika sasa wameamua kujifunika katika mwamvuli wenye matundu madogo.., wanapigwa na Jua hafifu, wananyeshewa na mvua laini..., hawafahamu kwamba wanalowana kwa matone hafifu hayo.., hebu tazama mambo machache sana yafuatayo ;
DRC ; Rais _Joseph Kabila Kabange_, ameamua kutumia mamlaka yake na kusogeza mbele uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu (2016), sasa uchaguzi utafanyika mwaka 2018.., miaka miwili zaidi.
BURUNDI ; Rais _Pierre Nkurunzinza_, alibadili vifungu vya katiba ya nchi hiyo, ili apate fursa ya kupata nafasi ya kugombea urais wa nchi hiyo kwa awamu ya 3, kinyume na katiba ya nchi hiyo ambayo Rais anatakiwa kugombea kwa awamu 2 tu na siyo zaidi.
RWANDA ; Rais _Paul Kagame_, kupitia serikali yake, amepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria katika bunge la nchi hiyo ili aweze kupata fursa ya kuendelea kuwa Rais wa nchi hiyo, wakati uchaguzi ukirefushwa kumpisha Kagame katika wakati huo..
SUDANI KUSINI; Ugomvi wa maslahi kati ya Rais wa Sudani Kusini, _Salvar Kiir_ na kiongozi wa waasi _Riek Machaar_ umeondoka na nafsi za watu wasiokuwa na hatia wengi sana.., wanawake na Watoto wamekuwa wahanga wakubwa wa vita hiyo isiyokuwa na maslahi kwa wananchi ya moja kwa moja..
SOMALIA ; Taifa hili limeharibiwa na vita kubwa ya wenyewe kwa wenyewe.., Somalia limekuwa taifa amabalo sasa ni kitovu cha kuzalisha magaidi katika ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi na hata ukanda wa maziwa makuu.., hii ni kutokana na watawala wa Afrika na taasisi zake kutokufanya kitu cha kuokoa hali hii.., iko wapi AU!!?
AFRIKA KUSINI ; nchi hiyo imegubikwa na rushwa, ufisadi, Ubadhirifu, hadi viongozi wakubwa sana katika taifa hilo hususani Rais Jacob Zuma anatuhumiwa kwa kiasi kikubwa kuhujumu uchumi wa nchi hiyo kww kujilimbikizia mali za umma.., nchi hiyo sasa inaanda muswada kupeleka bungeni ili ijitoe katika Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC).
TANZANIA ; kwa muda mfupi sana ndani ya miaka 15, nchi hiyo imepita katika kipindi chenye kashfa nyingi sana.., kashfa kubwa za ufisadi, Ubadhirifu na Rushwa.., ( RICHMOND, ESCROW, TANGOLD, EPA, MEREMETA, RADA, LUGUMI, KIGODA, Tanzania iliwahi kutajwa nyakato fulani kama nchi ambayo ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa sana la Rushwa katika jamii yake.. Lakini watawala wamaondoka katika nafasi zao bila kushughulikia matatizo hayo hata chembe..
Matendo hayo ya watawala ndiyo hushusha morali ya uwajibikaji kwa wananchi, huondoa tunu ya wananchi kuwa watiifu kwa taifa lao.., na pia ndiyo chanzo kikubwa cha macahfuko yasiyokuwa na mwisho ya mara kwa mara kwa mataifa mengi sana.., Raia au Mwananchi wa kawaida anapotimiza wajibu wake anahitaji kurejeshewa haki yake kama sehemu ya malipo yake rasmi..., haki yake ikiminywa kwa namna yoyote ndiyo chanzo kikubwa cha watu kupiga kelele...
Utawala bora na wenye kufuata sheria kwa watawala wengi eneo hili kwao ni gumu sana.., hawataki kuona wanapingwa, wanakosolewa na hata kuthubutu kutofautiana mawazo na fikra kati yao na wale wanaotawaliwa..
Hili pia ni eneo ambalo watawala wa kiafrika wameshindwa kabisa kulimudu, watawala wengi wa Afrika wamekuwa ni wenye kufuata matakwa yao wenyewe na haswaa yenye kufurahisha nafsi zao, wengi hawapendi kukosolewa, hawapendi kutofautiana mawazo na wengi wamesimika tawala zao kuwa za kiimla katika mwamvuli wa demokrasia tena ya vyama vingi vya siasa isiyokuwa huru na haki...
Tazama mifano Ifuatayo;
ZIMBABWE kumekuwepo na malalamiko ya mara kwa mara kila ifikapo nyakati za uchaguzi, pia nchi ya GABON imetajwa kuwa na vurugu za mara kwa mara katika chaguzi zake mbili zilizopita.., pia nchi ya ZANZIBAR iliwahi kukumbwa na machafuko katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, nchi ya KENYA pia iliwahi kuingia katika machafuko ya baada ya uchaguzi mwaka 2008, nchi ya IVORY COAST pia imewahi kutumbukia katika ghasia za baada ya uchaguzi.., JAMHURI YA AFRIKA YA KATI pia iliwahi kuingia kwenye machafuko ya kisiasa ambayo yaliingia hadi katika imani za kidini., JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO pia imekuwa na matukio yenye machafuko ya mara kwa mara.., Hiyo ni mifano michache sana..
.., machafuko makubwa ya baada ya uchaguzi katika mataifa hayo ndiyo sehemu kubwa na chanzo cha makundi makubwa na madogo ya waasi.., mfano waasi LRA , M23, Séléka, NFL, NLF, Al shabaab, ISIS, Al-Qaeda, Boko Haram, CDF, Kamajors, AFRC, SPLM, Rasta Militia na makundi mengine mengi....
Pia Afrika imeshuhudia watawala waliopata kutawala kwa muda mrefu sana katika nchi zao na kufikia nyakati kufikiri zile nchi ni máli zao walivyofurushwa na wananchi waliowachoka..
MUAMMAR MOHAMMED ABU MINYAR GADDAFI, alikuwa Rais wa muda mrefu wa Libya, aliuwawa oktoba 20, 2011 huko Sirte, Libya na vikosi vya waasi vya nchi hiyo alipokuwa akitoroka kuelekea nchi ya Chad... Alitawala kwa miaka 42..
MUHAMMAD HOSNI EL SAYED MUBARAK, kiongozi wa zamani wa muda mrefu wa kijeshi na Rais wa taifa la Misri, alitawala kwa miaka 30, baada ya Mapinduzi ya mwaka 2011, alishtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, na mauaji ya waandamanaji katika maandamano ya kumpinga.., Siku 18 pekee zilitosha kumuondoa Mubarak madarakani, baada ya maandamano yasiyokuwa na mwisho katika viunga vya Tahrir square.., amehukumiwa kifungo cha maisha jela!
ZINE EL ABIDINE BEN ALI, alikuwa Rais wa pili wa Tunisia.., katika vuguvugu la mapinduzi katika nchi za kiarabu mwaka 2011.., alifanikiwa kung'oka.., alitawala nchi hiyo kwa miaka 24, tarehe 14-01-2011 baada ya waandamanaji kupamba moto wakitaka ajiuzuru, yeye pamoja na mkewe Laila Ben Ali na watoto wao watatu walikimbilia Saudi Arabia. Baadae serikali ya muda ya Tunisia kupitia polisi wa kimataifa walimkamata Ben Ali na akafunguliwa mashtaka ya utakatishaji fedha, biashara ya dawa za kulevya na akahukumiwa miaka 35 jela.. Pia alikutwa na hatia ya mauaji na kusababisha vurugu katika nchi hiyo na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani..
.., tawala nyingi sana za Afrika zinatumia nguvu za ulaghai., zinatumia mapandikizi katika sehemu mbalimbali na mashushu pia... Nguvu ya mashushu wanaojipendekeza kwa serikali nyingi za watawala zimepwaya kwa sababu nao ni binadamu pia; wanafika mahali wanaona ukweli... Kwamba hali ya Maisha ni ngumu.., maisha ni magumu na yanawaathiri wao na ndugu zao vile vile.
Pesa za wizi na halali zilizo mikononi mwa vyombo vya dola na vyama tawala katika tawala nyingi za Afrika zina kikomo. Haziwezi kununua kila kitu kwa wakati wote. Walau hadi sasa, zimeshindwa kununua mapenzi ya wananchi kwa serikali na ndiyo maana unaona machafuko kila uchwao..
Haziondoi chuki yao dhidi ya watawala walioahidi maisha bora ambayo hayajapatikana, na dalili hazionyeshi kama yatapatikana wakiwa madarakani wakati watawala hao wakiendelea kunufaika wao na familia zao..
Vitisho dhidi ya wakosoaji wa serikali havifajua dafu kwa sababu serikali za kiafrika hazina nidhamu tena; mambo ya kukosoa yanaongezeka kila siku.., wakati watawala wakiendelea kuleta sheria kila siku za kuwabana wakosoaji.
Uoga wa wananchi kwa watawala wa aina hii umepungua kwa kiasi kikubwa, na uelewa wao wa masuala ya kisiasa umeongezeka na hii ni sumu kwa serikali nyingi za kiafrika..
Kuna somo la kujifunza hapo.., kwamba hakuna tawala za kidikteta, kifashisti ambazo zinaweza kuishi milele.., ingawa zinaweza kuishi kwa muda mrefu lakini siyo wakati wote.., hivyo watawala hawapaswi kuwa watawala katika kuongoza watu.., lakini wanapaswa kuwa viongozi ili wapate fursa ya kuongoza watu katika mataifa yao...
Martin Maranja Masese,
Mwananchi wa kawaida,
martinchizzle@gmail.com