Nchi 5 ambazo Askari hawaruhusiwi kubeba silaha za moto kwenye doria

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Mauaji ya raia imekua topic kubwa kwenye media mbalimbali duniani kwa siku chache zilizopita na hiyo ni baada ya Polisi ‘Wazungu’ kuua Wamarekani weusi huku mauaji hayo yakinaswa na camera za simu za mashuhuda. Vifo hivyo vilipelekea mpaka Mwanajeshi mmoja wa zamani mwenye utaalamu wa kulenga shabaha kwenye mji wa Dallas Marekani, kujitoa muhanga na kuua askari watano na kujeruhi wengine kadhaa kwa hasira za kulipiza kisasi cha Weusi wenzake kuuawa.

Inawezekana visa vyote hivi visingetokea kama Askari wa Marekani wasingekua na silaha za moto na badala yake wakimkamata Muhalifu wanamfunga pingu na kumpeleka kituoni ila kwa sababu wote walifanya mauaji hayo kwa kutumia bastola, visa vya kulipiza visasi ndio vikaibuka kwenye miji zaidi ya mitatu baada ya video zilizonaswa kuonyesha uonevu.

Kuna nchi ambazo zinaweza kuepuka balaa kama hilo sababu askari wao hawaruhusiwi kisheria kuwa na silaha za moto kwenye doria ambapo nchi hizo ni Ireland, Norway, Iceland, New Zealand na Britain. Askari wa hizo nchi tano huruhusiwa kubeba silaha za moto pale tu kunapokua na matukio maalumu au kwenye ishu nzito nzito, pia kwa upande wa Marekani mpaka sasa ni zaidi ya watu 512 wameuwawa na Polisi toka mwaka 2016 uanze wakati mwaka 2015 ni watu 990.
 
Huwezi kuzuia hao jamaa kutembea na silaha wakati nchi bado haijajitosheleza! Hao wabeba silaha tu wenyewe wakizidiwa hula majani na kusahau sheria za viapo za kazi zao. Wanajichanganya na vibaka.....
 
Nchi ya Vatican ndiyo nchi pekee duniani ambayo haina polisi wala jeshi lo lote na hakuna uhalifu wo wote. Haina mahakama wala bunge. Mkuu wa nchi hiyo anaitwa Pope ambaye hupatikana kwa moshi mweupe na siyo kwa kura. Nchi hiyo huongozwa kwa canon laws tu na hakuna figisufigisu za demokrasia wala nini.
 

Umekosea mzee, wana askari tena wenye mafunzo ya kijeshi
 
Kwan polis wana dhibiti raia wema no vbaka ndo watatumia huo mwanya
Uh, basi tuseme kwa hii nchi yetu nadhani bado sana kuutumia mfumo huo na hata nchi za africa kwa ujumla
 
Inawezekana yapo mengi tu makubwa yanayotokea huko, lakini ndo vile yanakuwa yanazimwa yasitoke nje ya nchi yao
 
Akili ndogo, moshi unaweza kuchaguwa binadamu? Kama hujui kitu kaa kimya.
 
Akili ndogo, Pope anapigiwa kura na makadinari, moshi ni signal tu kama kura zimetosha au zinapigwa tena.
 
Umekosea mzee, wana askari tena wenye mafunzo ya kijeshi
Hawaitwi askari na kazi yao ni kumzunguka (nyie mnaita kumlinda) Pope hasa anapokuwa nje ya nchi yake.

Hivyo sijakosea. Katiba ya nchi ya Vatican ni zile Ten Commandments.
 
Akili ndogo, Pope anapigiwa kura na makadinari, moshi ni signal tu kama kura zimetosha au zinapigwa tena.
Siyo makadirinari bali ni Mitume. Huko hakuna vyama vya siasa wala ilani za uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…