Nawezaje kuachana na mwenza wa miaka mingi tuliyezaa watoto 5 pamoja?

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
2,349
4,613
Tayari uhusiano huu umezalisha watoto watano.

Wakuu tupeane maujanja ya namna ya kutoka kwenye mahusiano haya na matokeo yake (yote mazuri na mabaya) ya kuachana huko.

**Sitaki ushauri wa kurudiana maana maamuzi ya kuachana tayari yameshafanyika.
 
Mmejaribu kuwaza vile mtakavo wapa shida na msongo wa mawazo hao watoto watano?

Nao mmewahusisha kwenye hayo maamuzi yenu au hayo maamuzi ni kwa ajili yenu tu.?

Ni wakati mgumu sana na inahitajika hekima kubwa sana..

Poleni kwa changamoto zilizo wakuteni.
 
Dingi Wangu Angekuwa humu hili swali angelijibu vizuri sana, maana yeye alitufyatua 11 katika nyumba ya vyumba viwili, baada ya hapo akaukimbia mji na kuoa mwanamke mwingine huko nako kafyatua Saba na maisha yanaendelea. Kwa kweli akina mama wana kazi sana ya kulea watoto na dingi Kwa sasa ni majuto kwa sana kwa kitendo kile cha kukimbia mji…maana sasa siku zimeenda na watoto wote hatujamtenga…lakini kila siku ukikutana naye yeye ni kuomba msamaha tu hadi huruma…
Angalia ndugu yangu, mutawapa watoto wakati mgumu sana, lakini Kama uko vizuri na uendelee kuwapa matunzo pia emotional support - itawasaidia sana…
Kufyatua Ina majukumu mengi sana beyond utamu wa Dakika 3…
Fainali uzeeni… Hilo zingatia sana…
 
Kuna mzee alimuacha mkewe wakiwa na watoto 12, nwingine waliachana wakiwa na watoto 8, hawa ni watu naowajua kwa karibu,

kuliko mchinjane humo ndani heri muachane, kwa watoto ni maumivu lakini sio vyema kuishi na mtu mlieshindwana kwa msukumo wa watatuonaje?
 
Amani ya moyo ni muhimu sana,baba na mama waliachana wakiwa na watoto 7 including me,niliachwa na kulelewa na baba nikiwa na mwaka 1.8 na leo hii nipo,kupitia hali hii sina huruma na mwanamke atayeniletea ujinga ujinga,nikuachana na kuoa tena,hata kama nitaoa mara 100 sitajari.

Mkuu tafuta amani ya moyo wako,usiwaze juu ya watoto,ikiwa mimi nimekuwa toka kuachwa nikiwa na mwaka1.8 sasa hofu yako ni ipi? Mwambie huyo huyo mwanamke humtaki tena ikiwa una sababu kuu ya kufanya hivyo,huhitaji kujiuliza.
 
Dingi Wangu Angekuwa humu hili swali angelijibu vizuri sana, maana yeye alitufyatua 11 katika nyumba ya vyumba viwili, baada ya hapo akaukimbia mji na kuoa mwanamke mwingine huko nako kafyatua Saba na maisha yanaendelea. Kwa kweli akina mama wana kazi sana ya kulea watoto na dingi Kwa sasa ni majuto kwa sana kwa kitendo kile cha kukimbia mji…maana sasa siku zimeenda na watoto wote hatujamtenga…lakini kila siku ukikutana naye yeye ni kuomba msamaha tu hadi huruma…
Angalia ndugu yangu, mutawapa watoto wakati mgumu sana, lakini Kama uko vizuri na uendelee kuwapa matunzo pia emotional support - itawasaidia sana…
Kufyatua Ina majukumu mengi sana beyond utamu wa Dakika 3…
Fainali uzeeni… Hilo zingatia sana…
Majuto ni mjukuu......alijifanya kitombi sasa yanamkuta....na angalau mna mpa miambili miambili vinginevyo angeita maji Umma.

Ukiwa kijana kuwa makini sana na mienendo yako. Imagine mtu anafyatua tu hadi 11 wala uwezo wa kulea au kujenga nyumba hana.

Mtu kama huyu hajali mnalala wapi, mnakula nini yeye anajua tu kuosha rungu na chakula huwa hanunui.

Akaenda huko akazaa tena 7.

Wazungu walishasema Africa tunaweza kuzaa sana, ngono, pombe na kucheza ngoma tu.
 
Nadhani Kama mmeona kuachana ndo Hatua nzuri zaidi Kwa mlipifikia basi ni vyema mkaachana Kwa amani.

Lazima muandae mpango mzuri wa namna ya kulea hao watoto wenu pasipo kuwaumiza. Mnaweza kukubaliana watoto waishi Kwa Nani, ratiba za kuwaona, gharama za mahitaji muhimu ya afya,elimu,chakula na malazi vizingatiwe.

Binafsi naunga mkono nyie kuachana, kuliko kuishi na mtu ambaye Hauna Imani nae Wala upendo nae Tena.

Zaidi ni kumuomba Tu Mungu uwe na mwanzo mzuri wa kuishi maisha mapya.
 
Tayari uhusiano huu umezalisha watoto watano.

Wakuu tupeane maujanja ya namna ya kutoka kwenye mahusiano haya na matokeo yake (yote mazuri na mabaya) ya kuachana huko.

**Sitaki ushauri wa kurudiana maana maamuzi ya kuachana tayari yameshafanyika.
Daah haya maisha bwana.......umemchakata mwenzio hadi umefikia watoto 5.

Ndio kusema hadi unafikisha uzao wa tano kulikuwa hakuna mapenzi?

Bado naamini kuna sababu nyingi za kuwaunganisha na kuendelea kuliko sababu kiduchu za kuwatenganisha.
 
Amani ya moyo ni muhimu sana,baba na mama waliachana wakiwa na watoto 7 including me,niliachwa na kulelewa na baba nikiwa na mwaka 1.8 na leo hii nipo,kupitia hali hii sina huruma na mwanamke atayeniletea ujinga ujinga,nikuachana na kuoa tena,hata kama nitaoa mara 100 sitajari
Wewe tayari ni Mwathrika wa Ndoa na talaka, ona umesha deviate from normal. Ushaona Mwanamke kwako hana thamani. Haya ni matokeo ya Wazazi wako kujali hisia zao na kusahau hisia za watoto.
Tayari tumeshampoteza Kijana mzuri kama wewe. Hujali tena kuzaa na kuacha. Wala hujui hao unaotelekeza ndio Machangudoa, vibaka, majambazi na mashoga. You seem to not care at all.

All in All pole sana. Tuwe makini na Mahusiano tunayoanzisha kwa aababu yanabeba mstakabali wa maisha yetu ya baadae na vizazi vetu.
 
Kuna mzee alimuacha mkewe wakiwa na watoto 12, nwingine waliachana wakiwa na watoto 8, hawa ni watu naowajua kwa karibu,

kuliko mchinjane humo ndani heri muachane, kwa watoto ni maumivu lakini sio vyema kuishi na mtu mlieshindwana kwa msukumo wa watatuonaje?
Hivi hii inakuwaje kuwaje? Umemchakata mtu hadi umeipanua mara 12😅😅😅
 
Cha msingi hudumia watoto, tena kwa wakati. Mapenzi yakiisha na mkiwa na watoto inahitajika zaidi ya hekima juu ya malezi ya watoto.

Hao watoto hawana la kufanya na mapenzi yenu, ila wanahitaji matunzo na elimu bora.
 
Majuto ni mjukuu......alijifanya kitombi sasa yanamkuta....na angalau mna mpa miambili miambili vinginevyo angeita maji Umma.

Ukiwa kijana kuwa makini sana na mienendo yako. Imagine mtu anafyatua tu hadi 11 wala uwezo wa kulea au kujenga nyumba hana.

Mtu kama huyu hajali mnalala wapi, mnakula nini yeye anajua tu kuosha rungu na chakula huwa hanunui.

Akaenda huko akazaa tena 7.

Wazungu walishasema Africa tunaweza kuzaa sana, ngono, pombe na kucheza ngoma tu.
Na amefyatua zaidi ya hao Saba Kwa michepuko mingine… dingi alikuwa mtu fulani muhimu Sana huko serikalini na wanawake walimzonga sana Kutaka maokoto… sasa umri umeenda anakimbilia almost 95 na ndio anakumbuka majuto…
Mtoa Mada awe makini sana na maisha ya ujanani… Binafsi nimejifunza Kwa machungu niliyopitia toka dingi akimbie nyumbani, Ila kuna donda kubwa sana kila nikikimbuka alivyotuacha bila huruma… ni donda haswa la maumivi na sipendi Kabisa hayo mambo ya mtoa Mada…watoto watapata taabu…Ni Mungu tu aliyenipitisha kwenye tanuru lile na kufika hapa kutoa ushuhuda- ashukuriwe Muumba Kwa kweli…ilikuwa ni taabu sana- saa 9 usiku wa mbalamwezi shambani hadi saa 1 asubuhi, baada ya hapo unakimbia kuchota maji round 2 na kujaza mtungi, saa2 asubihi darasani ukiwa umechoka sana hata aeiou hazipandi…saa 6 mchana unawaza hivi Leo tutakula nini, ukienda nyumbani ni Mwenda wa male da wa Magadi na dagaa saa 7 darasani, saa 9 ni either kuuza Vitumbua vya mwalimu mkuu au vibaragara vya ndizi ili nipate fedha za tuition na uniform…
Siku dingi Akirudi kalewa ni mtafutano humo ndani- fimbo hadi basi bila sababu yeyote na anazikomba fedha zote za vibaragara… yaani ni maisha yalikuwa magumu Sana miaka hiyo ya 85’s…Halafu Leo tuko miaka ya 24, bado mtu aNaomba ushauri wa kuachana na watoto/ wife…
Kazi kweli kweli… mtoa Mada dish linaelekea kuyumba…Kwa kweli simshauri aendelee na Wazo lake… huko mbele ni giza totoro…
 
Na amefyatua zaidi ya hao Saba Kwa michepuko mingine… dingi alikuwa mtu fulani muhimu Sana huko serikalini na wanawake walimzonga sana Kutaka maokoto… sasa umri umeenda anakimbilia almost 95 na ndio anakumbuka majuto…
Kumbe alikuwa na maokoto ya kutosha sana. Sasa ilikuwaje pamoja na kuwa mtu wa Mapene hajujenga Nyumba ya familia?

Imagine mtu aliyekuwa na kipato kikubwa alishindwa kujenga hadi nyumba je sisi tunaojitafuta hali si mbaya zaidi?
 
Mtoa Mada awe makini sana na maisha ya ujanani…
Kinachowasumbua wengi vijana wakiume na wakike ni ile kujiona kuwa naweza kufanya chochote anasahau kuwa after 50s kila kitu kinarudi mwanzo.

Atleast kama una uwezo wa fedha lakini kama una unga unga aisee kuwa makini sana na ujana. Utakuja kujuta hadi uchukie dunia unaanza kuona binadamu sio wema kumbe wewe ndio uliharibu unapata malipo
 
Binafsi nimejifunza Kwa machungu niliyopitia toka dingi akimbie nyumbani, Ila kuna donda kubwa sana kila nikikimbuka alivyotuacha bila huruma… ni donda haswa la maumivi na sipendi Kabisa hayo mambo ya mtoa Mada…watoto watapata taabu…Ni Mungu tu aliyenipitisha kwenye tanuru lile na kufika hapa kutoa ushuhuda
Mkuu unachosema uko sahihi Moja ya Ndugu zangu ameathirika kama hivi.

Watu wasio mjua wanamuona ana roho mbaya sana.

Ni Bahati mbaya kwamba tumempoteza na sisi Kaka yangu hayuko normal tena kutokana na kashi kashi za wazazi wasiojali hisia za watoto na kujali starehe zao tu.

Watu wananiuliza mbona kaka yako yuko hivyo nawambia ni maumbile tu kila mtu Mungu kamuumba huku najua fika Kaka yangu aliathirika na zile shurba. Hana upendo tena kwa sababu hajaonja upendo kwenye maisha yake.

Ni kwa neema tu wengine tunasalimika.

Vitendo vya kikatiriz ulawitiz mauaji na mengine kama hayo ni matokeo ya maumivu ya watoto ktk makuzi yao.
Irresponsible parents wanatuharibia Dunia ya Mwenyezi Mungu
 
Kumbe alikuwa na maokoto ya kutosha sana. Sasa ilikuwaje pamoja na kuwa mtu wa Mapene hajujenga Nyumba ya familia?

Imagine mtu aliyekuwa na kipato kikubwa alishindwa kujenga hadi nyumba je sisi tunaojitafuta hali si mbaya zaidi?
Jibu lake ni rahisi sana, yeye aliwasaudia kaka na dada zake Kama 16 hivi na sisi pia Tusaidiane ili hali hata abc za maisha hatuna… yeye alikuwa mtu wa bata tu… Mzee wangu nimesamehe ili sisahau alipo niacha… na hata msamaha wake sijui huwa anaomba wa nini maana ni kunimwagia chumvi kwenye donda Langu… all in all mtoa Mada arudi Kwa wenye busara wampe skill set aitunze familia. Kukimbia yaweza kuwa kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi… changamoto haziishi maishani…
Ndio maana siku ya kuzaliwa watoto wote hulia na siku ya kifo ni kinyume chake…
 
Siku dingi Akirudi kalewa ni mtafutano humo ndani- fimbo hadi basi bila sababu yeyote na anazikomba fedha zote za vibaragara… yaani ni maisha yalikuwa magumu Sana miaka hiyo ya 85’s…Halafu Leo tuko miaka ya 24, bado mtu aNaomba ushauri wa kuachana na watoto/ wife…
Kazi kweli kweli… mtoa Mada dish linaelekea kuyumba…Kwa kweli simshauri aendelee na Wazo lake… huko mbele ni giza totoro
Daa imeniuma kweli kweli, wazaI wengi hawana hela au wamepinda kimaisha sio kwa sababu hawakuwa na fursa ya kuwa na maisha bora bali walihendekeza starehe na ujana.

Sasa wanalauma watoto hawawasaidii. Imagine kama huyu alikuwa na kipato kizuri lakini anaishi kama chokoraa?
 
Back
Top Bottom