wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 249
- 701
Sabato ama ka neno lake asili la kiyahudi shabbāth ni neno lenye kumaanisha mapumziko
Mwenyezi Mungu kaweka amri ya kuitakasa siku ya Sabato ndani ya zile amri 10, ni jambo kubwa sana kwetu, Ni kibali kitakatifu kinachotupa ruhusa ya kupumzika siku moja kila wiki ya siku 7. Utaratibu wa kuiabudu siku hii ulianza tangu enzi za Musa alieaminiwa na Mungu kwenye mambo mengi ikiwemo kumkabidhi amri zake kumi, Yesu aliisifu sabato na bado mpaka leo inaabudiwa Israel na madhebu machache ya kikristo kama waadventista wasabato.
Ni ishara ya Upendo Mungu katupa siku hii tupuzike, Nasi pia turuhusu wafanyakazi wetu tuliowaajiri wapumzike, mifugo yetu tunayotumia kwenye shughuli zetu nayo ipumzike.
Katika mapumziko haya tusisahau kurudisha fadhila hii kwa kumuabudu alietupa siku hii, tukutane sehemu za kumuabudu tumuimbie nyimbo za kumsifu, kusali, n.k. kisha kurudi makwetu kuendelea na mapumziko
Yesu alizitii amri 10 na aliisifu siku ya sabato na kutusihi zaidi tuwe na upendo, hivyo hatuna budi tufuate njia zake