george aloyce
JF-Expert Member
- Aug 22, 2017
- 1,302
- 2,015
MTI WA MBAAZI UNAVYOTUMIKA KWENYE UCHAWI NA TIBA YA MARADHI YA MWANADAMU
MBAAZI- Huu ni mti maarufu sana kwa watu wengi na hutumika kama mboga ama chakula hasa kwa watu wa pwani
🫵Pia kwa upande wa wa waganga,wanga,wachawi na baadhi ya majini na mashetani pia wanautumia mti huu kwenye mambo yao
🫵Mbaazi ndiyo mti pekee wenye mambo mengi kwenye utibabu wa asili na hata uchawi kuanzia Majani,miti,mizizi,na hata udongo ulio chini ya mti wa mbaazi una kazi kubwa sana
UDONGO WA MBAAZI
.udongo wa mbaazi ndiyo unaotumika kuwapaka misukule pindi wanapopelekwa kwenye mashamba ya wchawi au kazi mbalimbali ili wasiweze kuonekana na watu wengine
.Udongo wa mbaazi pia hutumika kwa kuumwaga njia panda zinazoingilia kijiini ili kuwapoteza watu wabaya wasiweze kuingia katika vijiji vyao,udongo huo huchanganywa na vizimba vingine kisha huifadhiwa kwenye chungu ama tunguri kabla ya kwenda kuumwaga njia panda
.udongo huu hutumika kutengeneza chuma ulete,mtu kupendwa na viumbe majini(hii hutumia sana waganga wanaotumia majini au vitabu)kuwatupia watu maradhi ya kichawi,udongo huu pia hutumika kumficha mtu akaweza kuingia sehemu bila kuonekana na macho ya kawaida
MIZIZI YA MBAAZI
Mizizi ya mbaazi inatibu magonjwa zaidi ya 70,yapo baadhi ya magonjwa hutibiwa kwa miziz hiyo pekee na magonjwa mengine mzizi huo huwa kiungo kwenye mchanganyiko wa miti tofauti,mfano mizizi ya mbaazi ni tiba nzuri kwa mtoto mwenye kigugumizi
🫵pia mizizi ya mbaazi hutibu mtoto aliyechelewa sana kuongea
amka alfajiri kabla ya kuchomoza kwa jua,uwe msafi wa mwili na uvae kaniki au kitambaa cheusi
ukifika kwenye mti wa mbaazi ita jina lake mfano ewe mbaazi na uuombe maajabu yake kisha chimba mizizi ukimaliza chana kaniki funga miziz hiyo kisha fukia ulipochimba na unatakiwa uweke sadaka yako hapo chini ya mbaazi kama vile punje za nafaka mtama,mpunga n.k, viwe kiganja kimoja tu,pia unaweza kuweka pesa lkn iwe sarafu
🫵chemsha dawa kwenye chungu cha mfinyanzi na sio sufuria,anywe mtoto kikombe cha kahawa kwa siku9 kigugumizi na kuchelewa kuongea kutaondoka.
MTI WA MBAAZI
🫵mti wa mbaazi kuanzia kwenye shina hadi yanapoanza kuota majani yake ni dawa kali sana kwa anayetaka kupandishwa cheo,mvuto kazini,na kupendwa
🫵kata mti wa mbaazi wenye maua na uchune magamba yake kisha uyakaushe na uyatwange mpaka ziwe unga kama tunavyosaga dawa zingine za miti,wakati wa kukata uwe na kijogoo kidogo chekundu mchinje bila ya kusema Bismillah wala kibla(sababu ni chakula cha majini)
🫵kwenye kuutwanga au kusagwa ufanywe na msichana bikra,au bibi aliyemaliza uzazi,kisha mtu anayetaka kupanda cheo,mvuto kazini au heshima anavaa kitambaa cha rangi ya nyota yake na aoshewe dawa huku anafanyiwa dua njema
🫵huongeza heshima,kuogopwa, na kupewa siri za wabaya wako kwani moja ya matokeo ya dawa ni kuwa wabaya wako mmoja atawasaliti wenzie na kukuletea taarifa ya kila kinachoiri kwenye mipango yao
🫵pia mashetani na wachawi huwafunga wanyama wao kwenye miti ya mbaazi,mfano fisi,mbawala,kenge,nyoka nk
🫵pia wachawi huifadhi mikoba yao kwenye miti ya mbaazi kwa kuwa ina nguvu kubwa za kiroho kuliko mbuyu
🫵pia mbaazi hutumika kama fimbo ambazo hutembea nazo wachawi na wanga,mti wa mbaazi huchomekwa ndani ya ngozi ya mkia wa fisi maji au nyumbu.
🫵pia fimbo ya mbaazi hutumika kuwaamsha misukule,kuwatoa wafu kwenye makaburi yao kwa nguvu za giza na ndiyo maana wachawi wengi wanapokamatwa huwa hawapo tayari kuipoteza fimbo hiyo na wenye kujua huwa wanaing'ang'ania fimbo hiyo na hapo mchawi atakuwa tayari kukupa kitu
chochote hata mali zake zote.
MAJANI YA MBAAZI
majani ya mbaazi makavu hutumika kumpandisha ruhani asiyeweza kusema kwa sasbubu yeyote ile,changanya majani yaliyodondoka yenyewe na udi wowote kisha weka kwenye kaniki mfushe atasema bila shurutwi.
🫵ni huduma ya kwanza kwa mtu aliyepigwa na radi na kutoka damu,wazee hutafuna majani ya mbaazi na kumpaka
🫵mwenye kuweweseka usiku huchukuliwa majani haya na kiota cha ndege aliyekwishaangua vifaranga huchanganywa pamoja yanachemshwa na anaoga mhusika akiwa uchi kabisa kwa siku 9 atakaa sawa.
🫵hutumika kama kinga ya chuma ulete
🫵pia ukitaka kuwaona wachawi kaa chini ya mbaazi usiku wa manane uwe uchi anza kunuia mbaazi ukuonyeshe watembea usiku ghafla utawaona.
🫵MBAAZI ni mti wenye kazi nyingi zisizoisha hata kwenye vitabu vya tiba na uchawi ni mti wenye kurasa nyingi na hadithi ndefu
Kwa maelekezo zaidi nichek dm