NAUZA KIWANJA BEI YA KUTUPA

Chambuso2017

Member
Feb 14, 2017
50
22
Kipo Madale kwa Kawawa, kilometer moja kutoka Barabara ya Madale ilipo nyumba ya Mzee Kawawa.

Kina ukubwa wa hatua 25x25. Kipo kwenye makazi ya watu na kina nafasi za kutanuka kulia na kushoto mana ni ndogo sio rahisi mtu kuja kununua hizo ni mimi ndo ninayetakiwa kuzichukua tatizo fedha. Kinafikika kirahisi kwa gari na umeme umefika. Nahitaji pesa haraka.

Bei Shilingi Milioni saba, mimi mwenyewe ndiyo mmiliki lakini sijakikatia hati bado. Kwa maelezo zaidi nicheki PM nikupe namba tuwasiliane.
 
Metric dimensions ndio kipimo halisi hizo hatua is unknown na hazifanani na milioni 7. Hapa unatakiwa utambue ujazo wa square mita moja ni bei gani na wewe kiwanja chako ni square mita ngapi za mraba ili kurejesha uhalisia wa milioni 7 unazotaka.
 
Metric dimensions ndio kipimo halisi hizo hatua is unknown na hazifanani na milioni 7
Uwe mrefu kama Hasheem Thabit au uwe mfupi kama mzee Small, ukubwa wa hatua ni ule ule. Na hatua moja ni sawa na mita moja... Sasa wewe unataka vipimo gani vya metric hapo?
 
Uwe mrefu kama Hasheem Thabit au uwe mfupi kama mzee Small, ukubwa wa hatua ni ule ule. Na hatua moja ni sawa na mita moja... Sasa wewe unataka vipimo gani vya metric hapo?
Sio kweli kwamba hatua moja ni mita moja la hasha napinga kabisa.
 
Sio kweli kwamba hatua moja ni mita moja la hasha napinga kabisa.
Baci wewe miguu yako itakuwa na matatizo makubwa ya matege... Ukiwa na mguu uliopinda kama upinde huwezi kutoa hatua moja ikawa sawa na meter~
 
Baci wewe miguu yako itakuwa na matatizo makubwa ya matege... Ukiwa na mguu uliopinda kama upinde huwezi kutoa hatua moja ikawa sawa na meter~
Acha ubishi mkuu, me nilishawahi kupima kiwanja cha miguu 20x20 nikaishia kupata mita 16x16
 
Uwe mrefu kama Hasheem Thabit au uwe mfupi kama mzee Small, ukubwa wa hatua ni ule ule. Na hatua moja ni sawa na mita moja... Sasa wewe unataka vipimo gani vya metric hapo?
Ebu Acha uzembe hatua ya Tashimu Thabiti huwezi kulinganisha na hatua ya mzee Small na hatua za watu hazilingani kuna mtu hatua yake ni mita moja mwingine ni 0.8m na mwingine ni 0.5 etc etc inategemea na urefu wa miguu ya mtu, kama unabisha pima hatua zake na za mkeo uone kama zinalingana au pima za kwako na za mwanao
 
Tape measure ya mita 5 ni Tsh 5000/= umeshindwa kununua ili upime vizuri, alafu unataka milioni 7 kwa kipimo cha hatua, hivi hapa shida nini ni kwamba huelewi vipimo vya ardhi viko kwenye unit zipi pale unapoibadili ardhi kwa fedha!? Hivi kweli umeshindwa hata kipimo cha GPRS au google earth ukachop hilo eneo lilivyo! Hata kama ardhi ni yako lakini kwa uelewa wa vipimo hapo bado kuna walakini. Ila alie mwelewa atakuja na tape measure ili ajue ananunua nini kwa milioni 7.
 
Kimeshanunuliwa broo..
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…