Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,702
- 47,176
Kuna watu wamekulia na kulelewa mazingira ambayo wamezoea kuwaona wazaxlzi wao wakiamka na kushinda kwenye bao na kupiga porojo, wakicheka wakati wote na kufurahi. Wakitoka hapo wanaenda kwenye kahawa, na pengine kwenye ngoma.
Na hawa ikatokea bahati mbaya, mzazi akaondoka Duniani, matanga yakiisha tu wanaanza kumtafuta mteja wa kununua nyumba ya marehemu baba yao, mashamva ya marehemu, n.k.. Wakizidiwa watauza mpaka nguo za marehemu.
Hawa ndio wale wakakosa mlo, watauza mpaka kitanda. Wakipata hela ya mauzo ya kitanda watakula pilau na biriani mpaka hela iishe. Ikiisha watatafuta kingine cha kuuza. Kama wana binti, watalazimishe aolewe haraka ili mahari iokoe njaa ya nyumbani. Binti akitoka nyumbani, akashinda kusikoeleweka lakini jioni akarudi na mchele, kuku, mdalasini, pilipili Manga, watamsifia kweli kuwa anawathamini wazazi wake.
Sasa ikatokea bahati, watu waliokulia mazingira ya namna hiyo wakaupata uongozi, cha kwanza wataanza kuangalia nini cha kuuza. Watauza mbuga za wanyama, watauza ardhi na mapori yote, watauza bandari. Na kama kungekuwa na soko la kuuza binadamu, wakiishiwa kabisa, watapenda wauze mpaka binadamu wenzao. Wao fikra zao ni kuwa ili upate fedha ni lazima uuze, uuze kila unachokiona. Wanaamini kuwa waliotangulia hawakuuza kwa savabu walikuwa hawana uwezo wa kuwatafuta wanunuzi. Hawa hawana mawazo ya kuzalisha, kwao maisha ili yawe mazuri wanaamini suluhisho ni kuuza ambavyo hawakuvitengeneza, na kwamba wakati wote havikosekani vya kuuza.
Kwa upande mwingine, wapo wanaoamini kuwa kuishi kwa kusubiria mzazi wako afe ili urithi mali ni laana. Wanawafundisha watoto wao namna ya kutumia vinavyowazunguka katika kuzalisha. Wamekulia katika mazingira ambayo kila aliyepo nyumbani anajivunia kufanya kitu, na ndiyo fahari yake. Ikatokea mwanafamilia kauza shamba, ukoo mzima unamjia na kumhoji kuna nini, maana ameuza sehemu aliyostahili kuzalishia.
Aliyekulia na kuelelwa mazingira ya hivyo, akiupata uongozi lazima kutakuwa na tofauti kubwa. Kwake rasilimali asilia ataziona ni vizalishia mali na siyo bidhaa ya kuiuza. Anayeiuza ataonekana ni adui wa jamii nzima na muuji wa vizazi vijavyo.
Katika mazingira haya mawili tofauti, mwanaJF yumkini una kundi lako unalilona kuwa lipo sahihi, lakini ndivyo jamii yetu ilivyojengeka.