Revolution
JF-Expert Member
- Feb 28, 2008
- 902
- 827
Nikiwa kama mwananchi ninapenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa hawa Waheshimiwa wawili. Kwa kweli wamekuwa ni viongozi wa mfano ambao kwa kiasi kikubwa wanashughulikia matatizo ya watanzania maskini na wenye uhitaji. Hivi ndivyo viongozi wote wanapaswa kuwa na ili kuweza kumsaidia Mhe. Rais katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo kwa kuwapa huduma bora.
Ninamshauri sana Mhe. aachane na viongozi mizigo ambao kazi yao ni kujilimbikizia mimali na kutoka mavitambi, achague watu kama Mh. Jerry Slaa na Mh. Makonda.
Mh. Makonda kama binaadamu anazo changamoto chache za kiuongozi ambazo akiendelea kupikwa , kufundwa na kuelekezwa atakuwa kiongozi bora kabisa.
Sisi vijana tunajivunia sana kuwa na hawa viongozi wanaoonesha mfano kwamba vijana tukipewa dhamana ya kuwaongoza Watanzania tunaweza. Hivi Mawaziri wengine na Wakuu wa Mikoa wanajisikiaje wenzao wanapokuwa wanachapa kazi kwa kuwasaidia wanyonge wa nchi hii na wao wapo tu!!? Ingekuwa ni mimi ningeiga wanayofanya sio vibaya au aibu kuiga mambo mazuri kutoka kwa mwenzako.
Kama kuna namna Mh. Rais anaweza kuona post hii tafadhali na aione.