Natamani viongozi wote wa mataifa ya Afrika waiunge mkono kauli ya Nana Akufo Ado

kaligopelelo

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,812
4,035
Ifike wakati Sasa Afrika tuungane Katika kutetea masilahi yetu. Linapokuja suala la Afrika lisiachwe liwe la mtu mmoja,au taifa moja.
Afrika tuoneshe kujitambua.
4b4b21bfa8a5320cc25a5ede0f032658.png
 
Mi naona wawalipe hao wengine,sisi wasubirie kwanza,kwasababu hata zikija,sintafaidika nazo,zitaingia mifukoni mwa watu walewale wanaokula keki ya taifa,huku tukishuhudia,na bahasha zao zinazoandikwa SIRI.
😄😄 Hatari sana,hili taifa linahitaji maombi sana
 
... katika vyote ameona kulipwa "fidia" ndiko kutaikwamua Afrika? Kwa zaidi ya miaka 60 ya uhuru wa Afrika, bara hili limepokea mabilioni mangapi ya dola? Yameifikisha Afrika wapi? Badala ya ku-hit kiini cha tatizo, anajizungushazungusha tu kama kawaida ya viongozi wa Afrika.

Mwl. Nyerere alituasa, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne tu - ardhi, watu, siasa safi, na uongozi bora - fedha (fidia) sio miongoni mwa mahitaji hayo. By the way, wasingekuja wazungu (na waarabu) Afrika ingekuwa na hali mbaya sana kuliko iliyo nayo sasa.
 
😄😄 Hatari sana,hili taifa linahitaji maombi sana
Kabisa,yaani maisha yananipelekesha,nafanya kazi kwa bidii kutafuta mtaji lakini wapi,kwasababu dependants ni wengi na suwezi nikasema nisiwasaidie,maana ni ndugu zangu,naomba ajira TAMISEMI,wanachukua wa 2020,2021,wananiacha mimi,naomba sensa,wanapeana kimchongo,sasa hizo pesa eti zije,si zitaliwa tu.....?

Wao wawape nchi nyingine,ila huku,hapana kwakweli,mi sintafaidika kivyovyote vile,this country is corrupt,hata viongozi wake ni corrupt.... wanaila sana hii nchi,nilipofikia hata leo waseme ni mwisho wa dunia,niko tayari,tufe wooote.... labda tukiumbwa upya,kutakua usawa.
 
Ifike wakati Sasa Afrika tuungane Katika kutetea masilahi yetu. Linapokuja suala la Afrika lisiachwe liwe la mtu mmoja,au taifa moja.
Afrika tuoneshe kujitambua.View attachment 2325477
Naunga mkono hoja hii, ni muhimu Sana Afrika nchi za Ulaya kuilipa Afrika fidia walau kila mtu milioni 50 , kwa kuwafuta waafrika machozi ju ya uharibifu walio ufanya ndani ya Afrika.

(1) Kusombelea maliasili madini,pembe za ndovu malundo kwa malundo ndani ya Afrika na kuzipeleka Ulaya.
(2) Kuwafanyisha kazi ngumu mashambani , migidini na zisizo na ujira au heshima.
(3) Kuwa teka utumwani waafrika na kuwaoeleka uzunguni kwa biashara
(4) Kuwaua mababu zetu
Nk
(3)
 
... katika vyote ameona kulipwa "fidia" ndiko kutaikwamua Afrika? Kwa zaidi ya miaka 60 ya uhuru wa Afrika, bara hili limepokea mabilioni mangapi ya dola? Yameifikisha Afrika wapi? Badala ya ku-hit kiini cha tatizo, anajizungushazungusha tu kama kawaida ya viongozi wa Afrika.

Mwl. Nyerere alituasa, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne tu - ardhi, watu, siasa safi, na uongozi bora - fedha (fidia) sio miongoni mwa mahitaji hayo. By the way, wasingekuja wazungu (na waarabu) Afrika ingekuwa na hali mbaya sana kuliko iliyo nayo sasa.
Mi nadhani lengo sio kutajirika,kikubwa hapo ni kurejesha fidia ya uharibifu na wizi walioufanya. Haiwezi kulipia machungu na maumivu waliuopitia waafrika ila ni inasaidia kuwajulisha watesi wetu kuwa walichokifanya hakikuwa sawa.
 
Back
Top Bottom