Nataka sana kuoa

Boid

Member
Jun 23, 2016
40
62
Wakuu,

Kweli nimeamini kitu ukiwa nacho huwezi ona thamani yake, nakumbuka enzi nasoma nilikuwa nasoma na wasichana wazuri sana, ila sikuwai waza ata siku moja itafika nami niangaike kutafuta mke.

Nilikuwa naona kuoa ni rahisi tu yaani ni kiasi cha kumwaproach mwanamke unayemtaka, ila kwa sasa mambo yamebadilika sana ni tofauti na nilivyodhani natamani siku zirudi nyuma miaka mitano.

Enzi hizo kumwaproach mwanamke unayempenda ilikuwa rahisi ila sa hivi mambo ni magumu maana kila ninayemwona anafaa tayari anamilikiwa, hakuna ata aliye single, enzi zile nilikuwa naogopa kwasababu sikuwa na kipato, sasa hivi umri unakimbia huku nipo single tu nabaki kusema laiti ningejua.

Ni kitu kinauma sana pale unapokosa unachokihitaji katika maisha, nawashauri wale wenye wapenzi wao wenye malengo katika maisha washikamane maana muda utapomkosa utajiona hu mpweke dunia nzima.
 
Unajua hawa viumbe hawajielewi kabisaa! wanakataa watu wa kuwaoa wanakimbilia kwa players wanadungwa mimba waananza kulalama, huwa wanaonga raha kutoka na mabwana za watu, yaani they are very hopeless
 
ila we jamaa nimependa sana hiyo style yako ya kutafuta mwenza..

ila nachosikitika saiv humu watu wanawasiwasi na jinsia zinazosemekana ni za kike..

so, nakupa angalizo,kama unaPlan ya kuopoa jiko humu usije ukaoa mwanaume
 
Acha udomo zege wa bavicha wa kushangilia na kudekia barabara mafisadi.

Wanawake ni Wengi Sana kila siku wanahudhuria maombi wamekosa wachumba.
Hivi karibuni nimeona picha zinazunguka huko mitandaoni, mchungaji mmoja mzee ameoa binti mdogo kabisa sawa an mjukuu wake, sa sielewi huyu bwama anamaanisha nn hapa
 
ndiyo mara yangu ya kwanza kusikia mwanaume akisema amekosa mke wa kuoa,. Njoo Tanga nikutafutie
 
mkuu sijakuelewa... tatizo ni wasichana wachache au tatizo ni kumpata unayempenda... au unazungumzia ugumu wa kumtongoza msichana mzuri... weka bayana upewe mawazo na mafundi usione aibu mkuu..

Tatizo kupata anaefaa kuoa, wanawake wapo wengi ila wenye qualification namba imepungua au kwisha, huezi kuoa yeyote tu wengine unajinunulia ticket ya kifo.
 
Tatizo kupata anaefaa kuoa, wanawake wapo wengi ila wenye qualification namba imepungua au kwisha, huezi kuoa yeyote tu wengine unajinunulia ticket ya kifo.
hatujamshauri aoe yeyote ila swala la kusema waolewaji wameisha huo ni uwongo... wapo tele ila ninachohisi anataka wanawake wazuri kama kim kardashian halaf akijichek mwenyewe ndo hivyo tena!
 
Mkuu panua wigo,

Kama ulikuwa unatafuta huko makazini,sasa anza kwenda kwenye mikutano ya injili,kanisani,warsha mbali mbali za vijana,mziki kama unapenda hata hapa JF

Usikae tu,hawajleti,anza actively kumsaka mwenza wako,
 
duh walivyo wengi hadi wanalazimisha ndoa kila kukicha mkuu haupati?kuna tatizo mahali.
 
duh walivyo wengi hadi wanalazimisha ndoa kila kukicha mkuu haupati?kuna tatizo mahali.

Mkuu kumpata mtu mnaeendana sana,ni ngumu,watu wengi wana compromize vigezo,unasema so long ana hiki,hiki na hiki,then namuweka ndani,sasa kama unataka mtu 100% perfect,utasubiri sana.
 
Tafuta madalali wakusaidie
 
Sio kila mwanaume ama mwanamke unadhani anafaa kuolewa ama kuoa, na katika kuoa uwa inahitaji uangalifu sana maana ndio maisha yenyewe so unapocomment ufikiri kwanza la sivyo nisingepost chochote zaidi ningeenda kwenye madanguro na kutafuta wa kuishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…