Nataka kusomea kozi ya Operation of Harbour (Mobile Harbour Crane and STS)

Isaya wa njombe

Senior Member
Apr 2, 2023
191
385
Kwema?

Niende kwenye mada.

Mimi kazi yangu nalipwa mshahara laki tatu 300k nipo DSM lengo la kuandika juu Uzi nataka nikasomee hiyo kozi hapo juu kuendesha mitambo ya bandari. Nimepata chuo kipo pale Kijitonyama(Ihet)

Lengo la juu Uzi naombeni ushauri NSSF nina m5 na chuo ada nimeambiwa 2350000 nataka niache kazi ili nichukue pesa kiasi niende shule, hofu yangu naombeni uzoefu.

Je, hii kozi soko la ajira likoje au ni mtambo? Ipi nikisomea angalau kuna upepo wa hata kupata deiwaka?

Nimefanya maamuzi hayo baada ya kuona mshahara wangu haukidhi mahtaji.

Pia sioni future kwenye maisha yangu, watu mnaopitapita bandarini ushauri wenu tafadhali

Ahsanteni.
 
Asante mkuu unanishauri VIP mi sina connection yoyote ila nataka nisomee na Nina last coin kwenye mfuko wangu ushaur wako tafadhar
 
Hallo hizo hela za Nssf sio za kutegemea kwani kuzipata mpaka utapofikia 60yrs.... So komaa na kazi ila jaribu kuanzisha biashara, ishi kwa bajeti ndugu! punguza wamama na matumizi yasikuwa ya lazima!
 
Nssf unachukua mkuu ukienda na barua ya kuachishwa kazi mkuu
ikiwa kama ajira yako ilikuwa ya ujuzi hawakupi wanahisi unaweza pata kazi muda wowote,ila kama ajira yako haihitaji ujuzi ndio wanakupa hela yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…