Nawazaaa na kuwazua naingia katika sayansi narudi katika Biblia nashindwa kupata Jibu!
Labda nianze na Bible
"Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Natumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu,wakatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani, na wanyama,na nchi yote pia,na kila kitu kitambaacho juu ya nchi"!
- Nataka kujua katika uumbaji waumbaji walikuwa wangapi??(Natumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu) Inamaana kuna mtu walikuwa wakijadiliana naye!
- Adam na Eva walikuwa ni kabila gani au Mweupe au Mweusi ili tujue Mungu ualisia wake kwakuwa kasema katengeneza mtu kwa mfano wake!
- Na uumbaji ulianza lini kwa miaka maana wanasayansi hutwambia kuwa baadhi ya miamba inamiaka milion na milion je uumbaji ulianza lini?
- Na wansayansi wanatwambia binadamu katokana na na masokwe je Mungu alianza kuumba Sokwe si binadamu japo tunaambiwa matabaka yalikuja kutokana na generation je ukweli ni upi??