Wapendwa
Najitokeza tena kwenye jukwaa hili, kuchukua hii fursa ya kujitafutia mwenza aliyeko tayari kuanza maisha;
sifa zangu;
- Nina umri wa miaka 39
- Sijawahi kuolewa wala sina mtoto
- Naishi Dar na ninajitegemea
- Ni mjasiriamali mdogo
- Nimelelewa kwenye familia ya Kiislam
- Elimu yangu ni kidato cha nne
- Nina mwili wa kawaida, rangi ya maji ya kunde/mweusi
Napendelea Mume ninaye muhitaji awe na sifa hizi;
- Awe na umri wa 45 na kuendelea (Sifa za umri na dini ni Muhimu kwangu)
- Akiwa na mtoto ni sawa; nipo tayari kumlea kama mwanangu
- Asiwe kwenye Ndoa ila kama alisha wahi kuoa haina tatizo
- Awe na kipato (mjasiriamali au ameajiriwa)
- Awe tayari kuoa na sio kuchezeana au kupotezeana muda
Kwa aliye tayari karibu pm tuchati