Natafuta mama wa hiari, baada ya mama kufariki

paluz

Member
Feb 9, 2016
53
9
Kama kichwa kijielezavyo.

Mimi ni kijana wa kitanzania nina miaka 23 sasa hivi nipo mwaka wa mwisho chuo kikuu UDSM -undergraduate.

Baada ya mama kufariki, nimeishi bila mama hivyo basi natafuta mama wa hiari atakayenipa malezi nikamhisi ame- replace nafasi ya mama yangu, nipo serious kwa hili.

Contacts:webasweba@gmail.com au ni PM
 
Pole sana kwa kuondokewa mama mkuu
Mama yako atabaki Kua mama hakuna wa kuziba nafasi yake.... Baba yako Yuko Wapi akutafutie mama wa kambo? Kuliko wewe kujitafutia
 
Pole sana kwa kuondokewa mama mkuu
Mama yako atabaki Kua mama hakuna wa kuziba nafasi yake.... Baba yako Yuko Wapi akutafutie mama wa kambo? Kuliko wewe kujitafutia
nimemaua kutafuta mwenyewe,kama yupo ajitokeze kikubwa anionyeshe upendo kama watoto wake alionao
 
pole mkuu. But huna mama mdogo? huna shangazi? huna marafiki wa mama yako waliokuwa karibu nae?

Una miaka 23 ni mtu mzima tena mwanachuo inamaana sio mhitaji wa malezi kama vile upo 8yrs.

Unahitaji washauri tuu. Kupatama mama mlezi wa kutoka mitandaoni sio vibaya but kuna mambo lazima uwe makin nayo mfano cultural difference.... na tofauti nyingine nyingi mkuuu

umri wako ni mkubwa Jiamin jiongoze. Tumia ndugu zako wa karibu wanaokufaham kwa msaada. pia wasio ndugu zako ambao wanakufahamu.
 
Kabla mama hajafariki aliota soon atafariki. Akamuuliza Malaika, umekuja kunichukua na wananangu flani na fulani mbona bado wadogo itakuwaje?

Yule mtu akamjibu usiwe na wasiwasi wanatakuwa vizuri tu. Baada ya siku tatu mama alifariki. Ndio tukaanza kushangaa kumbe alikuwa serious na ile story. We cried weee but ndo ivo hadi leo maisha yanasonga Mungu ndie anaetusaidia.

Ushauri: Wazo lako ni zuri, lakini kaa ukijua Mungu anakujua kama upo, anajua kama mama yako hayupo na anajua kama unahitaji faraja na upendo wa mama. Kwahiyo ishi kana kwamba una mama na maisha yatasonga tu kwa msaada wa Mungu.

Jitahidi kumuomba Mungu atakusaidia tu. Mwanadamu ni mwanadamu, unaweza pata mama watoto wake wakawa tatizo then ikakuongezea maumivu moyoni.
 
pole ila angalizo, usije lelewa tofaut maana wa mama wa mujin wapo wanaohitaj vijana wa kuwalea.
 

Pole sana kwa kuondokewa na mama.
Hakuna binadamu atakayeweza kuchukua nafasi ya mwingine, hususani mama.
Ni sehemu ya maisha wapendwa kufa. Ndio maisha yanasonga.
Kazana sana katika masomo yako. Achana na hizo habari za kutafuta mama wa hiari, bali umshukuru Mungu umefika hadi chuo kikuu. Wengine mama zao anafariki baada ya kuwazaa tu.
Mshukuru Mungu kwa kila jambo. Songa mbele.
 
Huna baba, mama wadogo na je ndugu wengine wa karibu huna? We jipendekeze tu uangukie kwa kina mama washirikina na wachawi ndo akili itakukaa vizur...23 yrs unataka kulelewa bado...
 
Mmmmmhh huu Umagharibi endeleeni nao nyie wasomi. Mtu wa ku replace mama!!!!? NB: Msinitukane mimi simo na sifahamu kama anaweza tokea mtu wa kumfananisha na mama. Weekend njema
 
Mmmmmhh huu Umagharibi endeleeni nao nyie wasomi. Mtu wa ku replace mama!!!!? NB: Msinitukane mimi simo na sifahamu kama anaweza tokea mtu wa kumfananisha na mama. Weekend njema
wewe unae,mimi sina mwambie mama ako akikubali nije kwenu
 
Duh!Pole sana najua uchungu unaoupata.
Kupata mzazi wa hiyari sio kitu rahisi hasa pale ambapo wewe ndo mhitaji.Mimi sina mama ila nawaheshimu wamama wote hadi wao wanatamani ningekuwa mtoto wao japo nshakuwa mtu mzima.Ila sasa kuna changamoto kubwa kwani utamheshimu mtu kama mzazi she will never be like your mama hakika nakuambia.Muombe Mungu na uwe mtu wa ibada.Mungu alisema yeye ni baba wa Yatima kwa hiyo mtegemee yeye utavuta watu wanaomtegemea katika maisha yako.
Usijepata mama wa hiyari akakufanyia jambo ambalo litakufanya uchukie wamama wote hata ambao hawajakukosea.
 
Pole sana kwakufiwa na Mama naelewa unavyo jisikia lakini kumbuka kua Mama ni mmoja tuu,hayupo na hatokuwepo wakuchukua nafasi yake,kama kweli ulikua nae karibu na unataka uendelee kua nae karibu basi muombe sana dua na pendelea sana kufika kaburini kwake na umuombe dua, yoyote yule atakae kwambia nakupenda basi hajamfikia hata ROBO ya anavyokupenda Mama,soma kwa bidii pata kazi mtolee sadaka kwa jina lake kwa kadri ya uwezo wako unavyoweza..
na mwenyezi mungu atakupa subra na uvumilivu Inshallah..............
 
Pole sana kwa kuondokewa na mama, lakini ssuala LA kutafuta mama wa hiar huku siafikiani nalo mama alikuwa na ndugu wanaomzunguka alikuwa anashirikiana nao tena wengine wanakufahamu vizur udhaifu wako hata mazuri yako kupitia kwa mama yako, huna ndugu upande wa mama? na kwa umri huo huitaj kulelewa unahitaj muongozo tu ambao hauhitaj mama ndo akupe MTU yoyote mtu mzima anakupa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…