Natafuta junior software developers wa backend na frontend na graphic designers tuunde kampuni

kwa-muda

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
2,097
5,364
Wakuu,

Mimi ni mtu ninayependa sana technology na nimekuw nikifuatilia sana masuala ya technology. Kwa upande wangu sijasoma course yoyote officially ambayo iko related na masuala ya IT ila mengi nimejifunza mwenyewe kuanzia programming japo siwezi tengeneza kitu chochote cha maana ila najua how things work na graphics ikiwemo motion graphics kupitia after effects nako huku siwezi jiita mkali.

Ndoto yangu ni kuja kuwa na kampuni ambayo itakuwa inatengeneza products ambazo zitatua changamoto za watanzania. Si product zile sawa na facebook clone, sijui whatsapp ya kitanzania hapa lakini product ambayo mtanzania ataitumia na kufaidi matunda yake kama ilivyo kwa mpesa, ilivyokuwa kwa maxmalipo n.k.

Hivyo basi, naona makampuni mengi yanaanza yakiwa madogo na hata steve jobs hakuwa programmer bali wozniaki ndiye alikuwa programmer, ningependa kuteam up na watu ambao wanaweza kuwa serious tukaanzisha kampuni. Tukafikiria na kuja na products mbalimbali ambazo zinaweza kutatua changamoto za watanzania na pia kutengeneza product za watu wengine wenye mahitaji binafsi ndani na nje ya nchi.
Nini nitaleta mezani?

Ninachoweza kuweka mezani, ni mtaji kidogo maana siwezi kusema nina ela nyingi ya kufund kila kitu, hivyo hivyo kidogo kidogo tunaweza kuelewana na hao mashareholders ambao tunaanza nao what we need. Mfano office space, working stations lakini kwa kiwango cha watu wanaojitafuta then from there labda natumai tunawza kusonga.

Nakaribisha maoni.
 
Nina experience ya kufanya hivyo aisee Kufanya kazi kwenye Tech startup yahitaji moyo wa chuma, Anyway kila La kheri Mkuu ukipenda kazi zangu njoo PM tufanye jambo

 
Nina experience ya kufanya hivyo aisee Kufanya kazi kwenye Tech startup yahitaji moyo wa chuma, Anyway kila La kheri Mkuu ukipenda kazi zangu njoo PM tufanye jambo

Mkuu umefanya kitu kizuri sana kwenye app yako all the best.
Ni kweli startups zina changamoto hasa pia na kudeal na watanzania unaweza kuwekeza halafu watu unaodeal nao wasiwe serious.
Lakini hili ni jambo ambalo ningependa kufanya
 
Back
Top Bottom