Natafuta chuo cha kufundisha kujipendekeza na kujikomba, hasa kwenye siasa

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
620
342
Eti tunalalamika kwamba watu wanapanda vyoe kwa kujikomba au kujipendekeza. KWamba msomi mzima alikuwa kipanga darasani lakini akifika kwenye taasisi au serikalini basi anaacha yale mashindano ya ukipanga anaanz amashidano ya ukilaza.

Kama ni mwandishi akiwa kilaza sana kuandika habari zinafurahisha wakubwa basi gazeti lake linapata matangazo mengi.

Kama ni ofisini, ukijipendekeza licha ya kumzidi akili huyo unayejipendekeza kwake basi utapanda vyeo, utanunua gari na kwa hakika utaishi maisha tunayosema ni mazuri.

Nasikia hata huko makanisani ili mtu uwe padri lazima huko seminari ufanye kazi ya ziaza ya kujipendekeza, tena wakati mwingine mtu akikuambiw akwamba "sema hii ni nyeupe" na wewe unasema ni nyeupe hata kama macho yako yanaona ni nyeusi.

Kwenye vyama nasikia utapatana na viongozi ukiwa ni fundi wa kujipendekeza na kujikomba.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kuna jambo hatufundishwi na kila mtu anajifunza kivyake.

Tnafundishwa kwamba kujipendekeza na kujikomba kwa binadamu mwenzio mwenye ubinadamu kama wewe ni kujidhalilisha. Lakini hapohapo unaona kwamba kila kona ya maisha wanaojipendekeza ndiyo wanafaidi maisha.

Ukifika kazini ukajifanya una akili nyingi kama ulivyokuwa chuoni basi sahau maisha mazuri, sahau kupanda cheo chochote. Wenzako waliongia katika mashindano ya kujipendekeza wanaondoka wakikuacha unaona.

Kama ni kwenye chama wenzako watachukua uongozi, watarithishwa uongozi na watoto wao utawaona wanasoma "nje", kwa sababu walijifanya wajinga kujipendekeza, wewe hukujipendekeza, ukaacha principle ya kufaulu kwa kujifanya mjinga, ukang'ang'ania kwamba wewe ni "genious" ukabaki hivyohivyo.

Sasa nahitimisha. Je, ni kipi chuo kinachofundisha kujipendekeza na kujikomba. Maana na mimi sasa ninataka kufaidi maisha kama wanaofaidi wanaojikomba na kijupendekeza.

Wasalaam.
 
Sasa nahitimisha. Je, ni kipi chuo kinachofundisha kujipendekeza na kujikomba. Maana na mimi sasa ninataka kufaidi maisha kama wanaofaidi wanaojikomba na kijupendekeza.

CHADEMA walipewa pesa na SABODO wajenge chuo.Kajikombe kwa MBOWE akuonyeshe walau tu kiwanja cha hicho chuo kilipo kabla hujaomba kazi kwenye hicho chuo chao hewa.
 
Ninakumbuka yule Dr wa sheria aliyepinga hata andiko lake la kitaalamu kuhusu serikali tatu wakati akiwa chuo kikuu. Alilipinga hilo andiko wakati wa mjadala wa katiba mpya. Sasa ni waziri wa sheria---Vilaza huwa wanazaliwa wakiwa vilaza!!
 
sijasoma habari isipokuwa kichwa cha habari,

Hakuna tofauti kubwa kati ya habari na kichwa. Suala ni kujipendekeza, iwe Lumumba au upinzani au taasisi yoyote. Nataka na mimi maisha mazuri yanayoyokana na kujipendekeza, kujfanya mjinga nk.
 
CHADEMA walipewa pesa na SABODO wajenge chuo.Kajikombe kwa MBOWE akuonyeshe walau tu kiwanja cha hicho chuo kilipo kabla hujaomba kazi kwenye hicho chuo chao hewa.

Sitaki chuo hewa,

Nataka kujikomba na kujipendekeza ili na mimi nifaulu maisha maana kufaulu siu hizi kunaendana na kujipendkeza.

Chuo hewa hakitanisaidia. Nataka nifaulu mashindano ya kuonekana lijinga maana huko ndiko kwenye utamu wa maisha.

Nisaidie mwenzi na mimi nifaulu kama wanaofaulu kwa kujipendekeza na kujikomba na kujifanya mambumbumbu.
 
Put in summary... habari za namna hii tumezichoka hata kuzisikia na kizisoma.

Hata ingekuwa mstari mmoja kama ni kilaza huwezi kusoma. Nifundishe jinsi ya kujipendekeza hata kwa kupinga hoja zinazotolewa humu JF.
 
Itumie sana Tbc na mawingu tv
 
Hakuna tofauti kubwa kati ya habari na kichwa. Suala ni kujipendekeza, iwe Lumumba au upinzani au taasisi yoyote. Nataka na mimi maisha mazuri yanayoyokana na kujipendekeza, kujfanya mjinga nk.
wewe ni mjinga tayari sio unajifanya
 
Kujikomba ni CHADOMO au CUF. Huko ndo kuna wenyeviti, makatibu na wagombea wa nyazifa mbalimbali wa milele. Hawapingwi na mtu, ukiwapinga wamekufukuza uanachama. Ni lazima ukijikombe kwao ili udumu katika uanachama/nyazifa ndani ya chama.
 
Intelligence haifundishwi.Ukiona mtu anajikomba na kufanikiwa kwa ajili ya hiyo project,ujue ana intelligensia kubwa kuliko wewe.Ukiwajua binadamu na kujua wanataka nini ili wakupe chako,hutapata shida.Leo Rais ndiye watu wanajikomba kwake lakini usidhani kuwa yeye hakuwahi kufanya hivyo kwa wakuu wake.Miti iliyo flexible huhimili upepo mkali tofauti na miti isiyo flexible.Kwa wakristo tumeambiwa wapeni hofu wanaotaka hofu,heshima wanaotaka heshima...
 

Kwa maana hiyo nikijua

1: kama anpenda uongo nisiseme ukweli
2: kama anamtaka mke wangu basi niafiki na nijkombe kwa namna hiyi nisipate shida!!!!
3: Kama mimi ni mwanamke na ananitaka nimkubalie kulala naye kitandani

Hiyo ndiyo inteligence, kama nimekupata.
 

Taabu nyingine kuu ni kwamba unayejipendekeza kwake anakujua ni mwenye shida na hata unayoyachuma kwa kujikomba wewe kwake ni kama ombaomba wa mtaani.

Tofauti ya yule ombaomba kama Matonya na mtu anayejikomba ni kwamba Matonya anatuomba barabarani sh. 1000 tunampa na yeye anasema ana inteligence.

Wewe unapojikomba au kujipendekeza kiwango chako ni kukubwa kuliko Matonya maana wewe utataka kujengewa nyumba Mbezi Juu na kununuliwa Prado basi hicho ndicho kiwango chako cha kujikomba na kujipendekeza.

Usichotambua ni kwamba wote wewe na Matonya hamna inteligence yoyote ni ujinga mtupu. Kama ungekuwa na inteligence ungejua kwamba mali aliyonayo huyo unayejikomba kwake ni mara 100 kuliko aliyokumegea baada ya kujipendekeza.

Mwenzetu hutaji kabisa neno kudhalilishwa unataja kuvuna toka kwa waru kuwa ndiyo akili.

Taabu yangu ni kwamba nimekuwa nikiona uvunaji huo ni ujinga kwa sababu sifa ya mtu unayejikomba kwake hakupi nusu kwa nusu, akikupa mali asilimia 10 basi umehheshimika mno. Kama kwa kujikomba wewe umejenga nyumba Mbezi Beach na na gari ukanunua Prado, yeye ana vituo 50 vya mafuta. Sasa hapo una akili gani.

Kama matokeo ya kujipendekeza na kujikomba yangekuwa kwamba unapata asilimia 40 ya mali anayokupa, kila binadamu angejikomba maana hakuna asiyeweza kujinyenyekeza kama punguwani ili achune asilimia 40 ya unayejipendekeza, na kwa hakika hapo ni ushindi maana umefaulu kumvuna asilimia 40 yeye kabaki na 60.


Lakini kujikomba ninakokuona huku, eti umejengewa nyumba Mbezi, ukanunuliwa Prado kisha watoto wako wakasoma international na wewe ukaona hui ni inteligence na unataka na sisi tusema ni inteligence, huo ni ukuda maana vyote hivyo ulivyovuna havikfiki hata asilimia 2 ya jamaa anayekugawia, yaani yule bwana unayejipendekeza au kujikomba kwake!

Hivyo, kujikomba na kujipendekza ni ukuda na hutakiwi kujisifia hata kidogo kwamba ni inteligence. Mnaojikomba wote tunatakiwa tuwajue na tuwatangaze hivyo.

Ndiyo maana mimi inaniwia vigumu na kama kipo chuo tuonyesheni tuwe wataaalamu wa kujikomba tulambe asilimia 50 ya tutakaojipendekeza kwao na si hivi viperemende vya mnavyopata mnaojipendekeza eti mnaita flexibility!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…