Nastaafu kuuza wake za watu (Ijue biashara ya wake za watu in and out)

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,160
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nimefanya biashara ya wake za watu kitambo sanaa. Nina uzoefu wa miaka si chini ya 5 katika fani hii, na mwaka huu 2016 nimekata shauri to retire for good. Kama biashara zote haramu kuacha sio rahisi kabisaaa, nishasema naachaa, naacha siachi wala nini. Ikitokea tenda najikuta nishauza mtu.

Kikubwa kinachonifanya niachane na ufirauni huu ni kumrudia Mungu, nimechoshwa na Adakadebra za shetani. Unapata hela ila zinafanya kupita tu mikononi mwako, hamna lolote la maana unalofanikiwa. Nikiwa alosto 2015 mwanzoni nilivokuwa nawomba vocha humu mpaka yule mdau akanitumia 200,000 sitoka nisahau maishani wakati nishashikaga mamilioni mara kibao ila nilimuona Mungu wa 3 siku hio. Ubarikiwe baba, nilimuomba Mola alie hai, kama kweli yupo, na ni mwema, aniponyeeee, nisiumwe tenaaa, he should give me back whatever was robbed from me by fate, my former career in Multinational companies, a cute, humble to die for BF, My previous body, Graduation and a legit fashion business by 2016 and i will serve thy Lord. Hayakuwa maombi ya mara moja, ilikuwa months and months of begging, Kwaresma niliizingatia ni balaaa. Tb Joshua You tube alinikoma.

Mungu hakawii wala hachelewi, nikaanza kupewa kimoja kimoja. Hello 2016, nimepata vyooote! God is POWERFUL than anything i have ever seen. Kama ilivo ada ukiwa omba omba huachi kuomba. Sasa najiandaa na Kwaresma ya 2016, maombi yako standby. Ndo nataka kutimiza nadhiri za mwaka jana kabla ya huo mwezi. Kwa uzito wa dhambi hii imenilazimu kuiungama hadharani, na nimeamua kutia kabisaa kibiriti na petroli hii biashara. Nauza CD yooooooooote kiasi kwamba hakuna ataeibiwa mke, wla ataekuwadia mke wa mtu. Na nitatoa internal controlsza kufa mtu leo. (Who am i kidding? Najua mtachepuka tu ila mtatumia akili sanaaa zaidi ya leo)

THE BEGINNING!
Hii fani sikuamka asubuhi nikaianza, walaaaa. Siwahi hata kufikiri nitakuja kuifanya. Kazi yoyote ya shetani inaanzaga na shetani mwenyewe. Kama shetani tu siku hio tumeenda sherehe za kifamilia nikamkuta aunt yangu ambae nilivokuwa mdogo nilikuwa nampenda hatari. Kachoka, kakongorokaaa, kazeeka. Nikamwambia nitakuja kwako, akaniambia usije. Tobaaaa! Nitakufa nyumbani niwasalimie.

Nikamwambia maza yule ana problem mi naenda huko huko kwake, maza akawa anasita ila umbea anautaka maana yule wifi yake alimnyanyasa sanaa bi mkubwa alivokuwa ndo kaolewa olewa na dada zake. Akaniambia nenda ila uwe makini. Nimefika kule kajitahidi kunifukuza wapiiii, nikamwambia hapa mi nalala wiki nzima. Akawa hana amani ka anaoga nje. Akaja mumewe, kalewa hatari. Usiku nasikia kelele anabondwa, nikataka kutoka, msichana wa kazi akaniambia utabondwa wewe, tulale tu dada. Masa 3 anapigwa tu. Kesho anajishuku kuniuliza unaondoka? Nikamwambia siondoki. Usiku ulisikia kitu? Nikamwambia sijasikia nililala na headphones.

Ndo akapata amani. Usiku huo hakupigwa ila matusiii yake balaa. Mchana anafarijika niko pale nacheza na watoto wale, ana mtu wa kuongea ambae sio hausigelo. Kumbe hataki wageni kwake sababu ya kuficha huo ufirauni wa mumewe. Hana rafiki, hana shoga, hana mtu yeyote kakumbatia ndoa. Ilivofika ijumaa ikamwambia mi ndo naenda kesho. Akaniita uwanjani kabisaa mbali tusisikike. Akaniambia tunaweza tusionane tena, nashukuru umekuja, watoto wamekujua, nisipokuwepo ongea na braza aniangalizie. Mmmmmh! Nikasema tobaaaa. Nikamuuliza unaenda wapi aunt bila wanao. Mi nahisi nitakufa siku si nyingi. Ndo kunisimuli mambo mazitoooo hayaandikikiii.

Mume si mume. Afu akamfrustrate ajione help less, hana msaada, ndo amekwisha. Hapo ashakuwa sucidal. Alimpiga mimba 3 zikatoka. Na mambo mengine mengi ya kifirauni tu. Mi nikaondoka nilivofika nikamwambia mzee mambo kule sio mazuri, kasema anajiua mwenzenu. Baba nae sijui tuite kikao cha ukoo, tuwakalishe, maza akasema tunaenda mda huu mguu kwa mguu unaenda kumfata au naenda mwenyewe na Lara. Basi tu akaona ujinga ilikuwa usiku, kachukua panga mpaka kule. Nimewafata hawa dada yangu na watoto.

Panga mkononi. Aunt anatetemeka, jasho linamtoka. Kuona panga ikabidi awe mpole. Akawachukua. Basi ndo kukaa nao home, mwili ukamrudi na kisura kikarudi. Mara napewa vibarua zawadi, ect pelekee shangazi yako, na comission napata aaaah! Shangazi nae alikuwa mwingi si kidogo. Tukawa tunakula ni balaaaaaa! Ndani ya mda mfupi alijaza kabati nguo mpyaa, simu kali, nywele za maana. Ungemjuaaaaa! Huku na huku mumewe akaenda kuombewa, alizimia masaa 11.

Pepo aliokuwa nao sio wadogo. Ila alipona, siku hizi hanywiii kabisaa, akiona pombe anatapika mpaka nyongo. Akarudi kwake, ndoa inaendelea, na anamtunza fresh afu bado mume hana amani alivomfanyiaga nyuma, roho inamsuta. Akanipa maelekeza ikija kazi ya msingi nimstue, wizara ya mambo ya nje kama kawaida. Yeye sio boya yule wa zamani. Mpaka 2014 kuna ishu ya rubani mstaafu nimemuunganishia.

THE MONSTER IN THE MAKING!
Aunt kaondoka, maisha hayasongiii kabisaaa. Kula vizuri hamna tenaaa. Daaaah! Ikawa problemoooo. Kama shetani tena, siku haina jina wala saa nikaongea na mtu tu shule, akaniambi His dad is very lonely. Mama yao alifariki so mzee akawa anawalea mwenyewe mpaka wamekua wako High school, wengine chuo, afu sio mtu mzimaaa wala nini huyo mzee, alizaaga mdogo tu. Mpunga upo wa kumwagaa, afu mstaarabu vibaya mnooo. Anawaambia feel free to enjoy the alcohol kwenye min bar yake home, hata ukienda kwenye bar yake unaandika tu jina la mwanae.

Ndo kuniambia inatakiwa apatiwe companion, manake yuko very bored asije jifia bureee. Nikashauri binti mdogo mdogo, akasema no, hawezani nao kabisaaa, ahsajaribu sanaaa, hamna kitu. Kila binti anaempata majangaaa, siku mbili anadai ana mimba wakati mdingi kafanya vasectomy. Sasa ikawa kasusa kaamua kuishi mwenyewe.Nikamwambia sikia huyu inatakiwa apate Single mom umri wake. Akasema nao vile vile, siku mbili wanaulizia urithi wa hao watoto waliokuw nao, au kutaka wale watoto wapendwe sawa na hawa wa ndani, na kutaka kutake over. Mzee hawezi hio. Nikampa msimamo kwa mantiki hio anatakiwa mke wa mtu mwenye shida shida, hawa waume zao waliopotea home au ambao hawaeleweki ila awe anajielewa, ana upendo wa kweli na yupo tayari pendeka maana anajua maisha ni nini.

Akasema iukifanikisha kuna 100,000! Yeluwiiiiii! Advance ilikuwa hela ya maana. Nikaenda kwa aunt, anatakiwa mtu huyu, aunt akataka aingie front hio kazi aifanye mwenyewe. Tobaaaa. Nikamgomea hana vigezooo, mzee anatakiwa mtu classic, mzee mwenyewe Elite, kakaa sana nje. Akaniunga na shoga zake 3 wote mashangingi.

Nikaona sasa hii hela naikosa. Kama shetani tu, nikamkumbuka binti mmoja anaitwa C wa olevel alikuwa na kamama classic, kama dada yake, maza mzungu ni balaa, afu ana binti huyo mmoja tu. Afu babake alikuwa haeleweki, hafanyagi kazi yoyote, yupo tu kijiweni, kama mzigo. Mkewe alikuwa airhostss mstaafu, sahivi secretary ndo anaibeba familia. Pamoja na hayo huyo baba yao kufumaniwa ni kawaida.Nikamsaka nikampata na kumpa mchongo, it is time for your mom to move on, nilimtia sumu za hatariii, mbele ya 100,000 mchaga namwaga verse. Akawa anasita, damu nzito. Nikamwambia your mom deserves better than him. 20yrs for this shit, akapumzike. Uvumilivu wa ndoa hauna tuzo. Akaelewa somo.

Yul mama mzungu tukamwambia kuna mtu anataka mtu kama yeye. Basi akapagawa kama ndoto, navomtajia mali za huyo baba, yuko Lara japo sikukuzaa ila nilikuwa nakupenda tuuu, nilijua utaniletea fursa. Sasa asiponipendaa, ngoja nianze diet, mama mwenye size 8 hapo, i need to be a size 0 kabla hajaniona. Hahahahaaa! Inabidi niagize anti aging creams. Nikaenda kumwambia mtu keshapatikana ila ana mume, akaanza kusita, muone kwanza mtu mwenywe. Nenda ofisi flani secretary ndo yeye. Kumuonaaa alalaaaaaaa! Akanikabidhi 100,000 cash. Ikafanyika party ya wazazi yule mama kaja nae. Mzee alidataaaa.

Walimalizana wenyewe kiutu uzimaa. Ila yule mama sahivi anaishi na yule pedeshee. Na mpaka kesho nikiwa na shida ananisaidia fastaaaa. Sema roho tu inanisutaaa, yule baba mume wa zamani mke alivoondoka, stress alikuwaga mlevii, mbwaaaaa, hadi alilewa akagongwa na gari akafariki. Najua mtalani sanaa ila ndo maisha.

THE MONSTER HERSELF!
Nilislow down kidogo hii business sababu yule baba aliniuma mnoooo. Nikasema naach haya mambo. Nikaacha kabisaa, and i was happy and blassed. Nikawa napata madanga ya maana hatari. Kimbembe chuo kuisha nikaanza kazi ya Sales kukutana na watu ndo ikawa balaaa. Siku hio kuna mwarabu mteja wangu mkubwa mnooo, ananifanikishia mambo yangu ya bonus hatariii. Namwambia tu mwarabu nunua kreti kadhaa nifike target ananunua. Mimi na yeye hatudhuriani.

Akaniambia nina maongezi na wewe. Tobaaaa! Nikajua ananitongoza, na sifa yao ile ya 0713 nikasema nimekwishaaa. Nikaenda kumsikiza uzuri. Akaniambia nimekuona una busaraaa afu msiri, mie natafuta nchepukooo. Awe nke ya ntu lakini. Vicheche hivi sivitaki. Hata akiwa binti awe ameolewa na anaishi na nme. Mie ntu wa dini mnooo, afu ntu mwenye pesa nyingi, na nke wangu nnmetoka nae mbalii sina kitu na muheshimu mnooo. Binti wasiolewa wanakuwa na fujo nyingiii, tamaa nyingiii, atakufata hapa, azushe zogo, mara ampigie nke wangu, sitakiiii.

Nke wa mtu, tunakuwa wote kiutu uzima, mie nanztunza uzuriii tu. Na mpa hela ya kula, kuvaa, atavaa atakacho, hata gari namnunulia mie kwani nna shida basi. Awe na adabu tunaliwaza kiutu uzima, anakungoja njiani ukmpa elfu 2 anashukuru ukimpa 200,000 anashukuru. Mmmmmh! Dau lako 700,000 cash mi nakugea. Looooh! Na awe dini yangu, ntu wa pwani pia, mianamke ya bara haijui mahaba.

Tobaaaa! Nikawa nishakata tamaa. Masharti magumuuu, mtu gani na shungi utamvaa umuuze? Acha kulogwa na waume zao. Mmmmmh! Nikiwa nimekata tamaa kabisaaa, siku hio junior staff mmoja mtoto wa Tanga jicho halikosi wanja, kicwa hakikosi kilemba akaanza kuniambia, mumewe haelewekiii, hatafuti kazi, anamtegea majukumu, anataka kuwapeleka wanae Almuntazir ila mishahara yenyewe ile, na ndo baba ndo mama yao nyumbani roho inamuuma wa kwanza kamuanzisha Kyumba l kwanza. Hako ka kike ndo balaaa, akifikiria Kayumba anashikwa tumbo la kuhara. Nikwambia njia ipooo, ila yataka roho ngumu kama jambazi. Jifikirie kweli Alimtazir unaitaka wewe mwanamke wa kibondei, ulifundwa unyagoni ukafundika? Jifikirie wiki nzima, ukiwa tayari kuingia vitani kutetea future ya wanao nambie, ila ujue jambo lenyewe sio jemaaa, yaani halina hata ujema robo. Kesho kanifata asubuhi nipo tayari.

Nimekuta yule mtoto wa kiume ana bonge na donda usoni kapigwa jiwe shuleni. Na shuleni nimewaachisha wote tunavoongea, we nipe hata namba ya chumba naenda sasa hivi, nakata mauno ya kufa mtu. HAHAHAHAAAA! (It is not a laughing matter you should be ashamed of your selves) Nikampa namba ya mwarabu. Nikampa A to Z, nikamwambia ulijamba hili vizuri nini Almuntazir, utatembea na matako mjini hapa kama kina fudenge. Mmmmmh! Akamtumia sms. Huku na huku kukutana nae kapewa 500,000. Kanigea 100,000. Mwarabu kanirushia 900,000 akaniambia wewe kibokoooo yao, si kwa mtoto huyu anaejielewa. Oooooh! Ndani ya miezi 3 watoto wote Almutazir, mmoj STD 1, kengine Nursery, school bus kila kitu.

Mume kaambiwa nimekuwa meneja kazini tulia boya wee, ulelewe watoto. Kazi imekushinda unasaidiwa. Heeeeee! Siku hio mke wa mtu mwingine hatuna mazoea kaniwahi getini, shoga nipo chini ya miguu yako nistiri mieee. Naaibika, navuliwa nguo dada yako, niko tayari kama A, niko tayari sasa hivi. Shemeji yako kastopishwa kazi watoto wako nyumbani ada, na kodi inaisha mwisho wa mwezi. Tobaaaaa! Majaribu gani hayaaa? Nikamwambia ngoja tucheki rada, manake bado unalipa, watoto 4 namba 8 iko gado.

THE PIMP!

IMEENDELEA UZI MPYAAAAA! Pt 2 ni hatari zaidiii
 
Last edited:
Daaah umeisha nitia hasara,yaani nikafungua kachupa kangu ka lager, halafu umepotea,nime kumaind,@#%¥§!!!!.
 
Hahahah.... story ya kufikirika hiyo. Toka lini wake za watu wananunuliwa wakati wao ndio wanatafuta wanaume
 
Wake za watu wanavyopatikana bure hivi kuna watu wanawapata kwa kununua?

Najua unaweza kua na nyota ya kunguni ya kukataliwa na mabinti lakini ukikataliwa na mke wa mtu una laana.

Mimi nakanyaga wake za watu almost on weekly basis.

Mi simooooo! Ngoja wenye wake zao waje.
 
Kama ni kweli umeamua kuacha dhambi zako hizo na kukiri hadharani ni jambo jema. Ila kama unacheza na akili za watu hiyo ni dhambi pia. Siri yako na Mungu wako.

Toba ya kweli ni kukiri, kujutia na kuachana na hayo mabaya!

Mungu akurehem sana, kuu la madui.. lara.

Cc Illovo
 
kabla hujaacha kabisa fanya kuniuzia mmoja wa mwisho!!! kuna package ya ukweli mezani...
 
Hahahahahaha, leo unatibu kiwe kitubio cha kweli.Na amani ya kristu ikae kwa wingi moyoni mwako.Na hao wake za watu naomba wamrudie Mungu tu manake kuwadi wao kashaiona nuru.
 
Kinondoni kuna njemba alimkosa kumtengua rafiki wa mke wake kiuno na revolver alikuwa akitoka rafiki yake mkewe alikuwa ana urafiki na njemba fuulani mtaani pale sasa bwana akawa anamshawishi yule mwanamke atembee na hao njemba

wambea wakamwambia mwenye mali akawakuta jamaa kachomoa revolver kaifyatua ikamkosa kosa kiuno NINA UHAKIKA alijamba yule mwanamke
 
Ninachokupendea akanana ni unavyo jua kufunguka....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…