Nashauri somo la physics liwe option kuanzia form one, mathematics liwe option pia

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,777
5,920
Au mwalimu mpwayungu village unasemaje?

Hii ni thathmini fupi ya masomo ya physics na mathematics kwenye matokeo ya form two yaliyotoka juzi.

1. PHYSICS
A - 0.4% (2,519)
B - 0.77% (4,874)
C - 4.73% (29,851)
D - 12.30% (77,586)
F - 81.79% (515,734)

2. MATHEMATICS
A - 1.96% (12,389)
B - 1.35% (8,532)
C - 4.84% (30,674)
D - 8.41% (53,246)
F - 83.44% (528,344)

Tatizo ni nini?
Je nani alaumiwe? Serikali? Wazazi? Walimu?..

Mwanafunzi anaingia form one huku uwezo wake ukiwa mdogo sometimes hata kusoma hajui, tukianza kuwashushia zigo walimu wa primary kwamba hawaandai watoto vizuri wanaweza kuja na hoja chanya nyingi tu juu ya kwanini watoto wanapandishwa wakiwa na uwezo mdogo.

Mtoto anapandishwa secondary baada ya kupiga chabo akifika anakuta mambo ni tofauti na magumu mnoo,

Nyie ni wazazi mnaweza kutoa ushuhuda humu, kwa waliomaliza form four before 2010, je ulianza kutumia simu lini? Sasa hivi wanafunzi wote wana simu tena wengine Kali kuliko walimu wao, suala la sex ndio usipime vijana wa siku hizi wameanza mapenzi primary ubongo umeshavurugika saana.

Turudi kwenye mada husika,

Kiukweli physics au Mathematics is not for everybody nitapinga saaana labda uje na hoja nzito sana inafaa mtu atulize akili aweze kuyamudu na kufaulu haya masomo.

Naiona juhudi ya serikali kuajiri walimu wa masomo hayo tena hao walimu wakiwa bora sana, lakini wanakuta nature ya watoto husika imeshabadilika mentality ya kusoma na kuyapenda hayo masomo hamna, ukisema uwachape serikali nayo inakuja juu.

O-level nimesoma tuition ya physcs na mathematics kwa mwalimu mmoja maarufu pale mwanza Michael mnyama pale ubungo secondary, jamaa alikua anapiga fimbo vibaya mno usipofanya kazi aliyoiacha ndio kilichonijenga nikaiva kidogo.

Nashauri serikali haya masomo mwanafunzi apewe choice ya kuchagua kuyasoma tokea akiwa form one, ili wale wanaojitambua wachache wapate fursa ya kuyaeelewa na kufanya vizuri, kuliko kujaza darasa wanafunzi 200 na wengine wakiyakataa kabisa hayo masomo wanasubiri form three wayakimbie. Kwanini yasiwe option kuanzia form one?
Imagine mwalimu wa mathematics au physcs akichukua wanafunzi wake 30 form one mpaka form four hakika hutokuja kuona matokeo mabovu ya Mathematics au Physics.

Ndio maana walimu wa chemistry na physics form four wanafaulisha sana kwa sababu form two wameshajichuja.

Nilikua naona matokeo ya st Francis waliofanya mtihani ni 92, miaka yote wako hivyo hivyo hawapungui wala hawaongezeki unadhani kwanini? Pale interview wanafanya hata 1500 but wanataka cream yao 92 tu, hakuna slow learner anaesoma pale.

mpwayungu village unaonaje wewe? Au wewe ni mwalimu wa history na language? 😁😁
 
Ninakuelewa sana hoja yako. Kuna kila sababu ya kutafuta ufumbuzi wa hili tatizo. Masomo hayo yaani Physics na Hesabu ni masomo muhimu. Siri na ufahamu wa ulimwengu umejificha kwenye masomo hayo.

Tutakuwa taifa la watu wajinga sana kama tutapuuzia masomo hayo. Ulimwengu unatawaliwa na Physics kuanzia enzi za Classical Physics ya akina Isaac Newton na wenzake hadi kwenye Quantum Physics ya akina Albert Einstein.

Moyo wangu unauma sana ninapoona watoto wanashindwa kusoma physics.
 
Solution yako ni hipi kama mdau wa elimu? Zigo tumuangushie nani? Hali inazidi kua mbaya sana, watoto haswa shule hizi za kata uwezo ni mdogo sana.
 
Mada nzuri mno ila kama kawaida yetu inapewa majibu rahisi,tatizo lipo kwenye foundation ya elimu yetu !mtoto akifika darasa la kwanza aanze kujifunza programing n coding, hii itamfanya mtoto ajenge uwezo wa kufikiri na sio kukariri,waalimu bora watafutwe na kuandaliwa vema na bila shaka tutarudia kule tuliko potea, hivi record ya Professor Sarungi pale Tosa ilivunjwa?elewa hadi leo UK inachukua waalimu na Nurse's from Zimbabwe, unafikiri why?Rwanda pia kaenda Zimbabwe mbona hakuja kwetu kutafuta waalimu bora!
 
Waalimu tangu shule ya msingi, wawe wa viwango vya juu. Kwanza wenyewe wawe waliofaulu masomo yao.
Mishahara ya waalimu iboreshwe ili kuwavutia wanaofaulu sekondari kujiunga na ualimu.
Vyuo vya ualimu viboreshwe dhana za ufundishaji, na wawe na wakufunzi walioiva, ili wanafunzi watoke hapo na ujuzi wa walichosomea na uwezo wa kuwaelimisha wanaoenda kuwafundisha.
Mashule yawezeshwe kwa zana, vitabu na maabara ili ufundishaji uwe kamili na rahisi kueleweka. Mazingira ya shule na makazi yawe rafiki kwa wanafunzi na waalimu wao.
Huu ni uwekezaji, kama mwingine wowote, serikali iwe na nia ya dhati kama inavyoendekeza siasa na wanasiasa, inatakiwa sasa iigeukie sekta ya elimu!
 
Solution yako ni hipi kama mdau wa elimu? Zigo tumuangushie nani? Hali inazidi kua mbaya sana, watoto haswa shule hizi za kata uwezo ni mdogo sana.
Nazishauri mamlaka za nchi kuongeza uwekezaji kwenye masomo hayo mawili. Hauwezi kiyafanya option kufanya hivyo ni kuongeza tatizo.

Niko tayari kushirikiana na mamlaka hasa katika eneo la sera.
 
Au mwalimu mpwayungu village unasemaje?

Hii ni thathmini fupi ya masomo ya physics na mathematics kwenye matokeo ya form two yaliyotoka juzi.

1. PHYSICS
A - 0.4% (2,519)
B - 0.77% (4,874)
C - 4.73% (29,851)
D - 12.30% (77,586)
F - 81.79% (515,734)

2. MATHEMATICS
A - 1.96% (12,389)
B - 1.35% (8,532)
C - 4.84% (30,674)
D - 8.41% (53,246)
F - 83.44% (528,344)

Tatizo ni nini?
Je nani alaumiwe? Serikali? Wazazi? Walimu?..

Mwanafunzi anaingia form one huku uwezo wake ukiwa mdogo sometimes hata kusoma hajui, tukianza kuwashushia zigo walimu wa primary kwamba hawaandai watoto vizuri wanaweza kuja na hoja chanya nyingi tu juu ya kwanini watoto wanapandishwa wakiwa na uwezo mdogo.

Mtoto anapandishwa secondary baada ya kupiga chabo akifika anakuta mambo ni tofauti na magumu mnoo,

Nyie ni wazazi mnaweza kutoa ushuhuda humu, kwa waliomaliza form four before 2010, je ulianza kutumia simu lini? Sasa hivi wanafunzi wote wana simu tena wengine Kali kuliko walimu wao, suala la sex ndio usipime vijana wa siku hizi wameanza mapenzi primary ubongo umeshavurugika saana.

Turudi kwenye mada husika,

Kiukweli physics au Mathematics is not for everybody nitapinga saaana labda uje na hoja nzito sana inafaa mtu atulize akili aweze kuyamudu na kufaulu haya masomo.

Naiona juhudi ya serikali kuajiri walimu wa masomo hayo tena hao walimu wakiwa bora sana, lakini wanakuta nature ya watoto husika imeshabadilika mentality ya kusoma na kuyapenda hayo masomo hamna, ukisema uwachape serikali nayo inakuja juu.

O-level nimesoma tuition ya physcs na mathematics kwa mwalimu mmoja maarufu pale mwanza Michael mnyama pale ubungo secondary, jamaa alikua anapiga fimbo vibaya mno usipofanya kazi aliyoiacha ndio kilichonijenga nikaiva kidogo.

Nashauri serikali haya masomo mwanafunzi apewe choice ya kuchagua kuyasoma tokea akiwa form one, ili wale wanaojitambua wachache wapate fursa ya kuyaeelewa na kufanya vizuri, kuliko kujaza darasa wanafunzi 200 na wengine wakiyakataa kabisa hayo masomo wanasubiri form three wayakimbie. Kwanini yasiwe option kuanzia form one?
Imagine mwalimu wa mathematics au physcs akichukua wanafunzi wake 30 form one mpaka form four hakika hutokuja kuona matokeo mabovu ya Mathematics au Physics.

Ndio maana walimu wa chemistry na physics form four wanafaulisha sana kwa sababu form two wameshajichuja.

Nilikua naona matokeo ya st Francis waliofanya mtihani ni 92, miaka yote wako hivyo hivyo hawapungui wala hawaongezeki unadhani kwanini? Pale interview wanafanya hata 1500 but wanataka cream yao 92 tu, hakuna slow learner anaesoma pale.

mpwayungu village unaonaje wewe? Au wewe ni mwalimu wa history na language? 😁😁
Kwa nchi zinazojitambua, Maths ni lazima upate angalau C ndipo usajiliwe kuchukua degree. Mfano Ireland na India. Wewe unadai iwe option, hapo tukueleweje
 
Waalimu tangu shule ya msingi, wawe wa viwango vya juu. Kwanza wenyewe wawe waliofaulu masomo yao.
Mishahara ya waalimu iboreshwe ili kuwavutia wanaofaulu sekondari kujiunga na ualimu.
Vyuo vya ualimu viboreshwe dhana za ufundishaji, na wawe na wakufunzi walioiva, ili wanafunzi watoke hapo na ujuzi wa walichosomea na uwezo wa kuwaelimisha wanaoenda kuwafundisha.
Mashule yawezeshwe kwa zana, vitabu na maabara ili ufundishaji uwe kamili na rahisi kueleweka. Mazingira ya shule na makazi yawe rafiki kwa wanafunzi na waalimu wao.
Huu ni uwekezaji, kama mwingine wowote, serikali iwe na nia ya dhati kama inavyoendekeza siasa na wanasiasa, inatakiwa sasa iigeukie sekta ya elimu!
Comment bora sana, tatizo wenye mamlaka nadhani elimu sio kipaumbele saaana kuweza kutengeneza na kutoa elimu bora.
 
Kwa nchi zinazojitambua, Maths ni lazima upate angalau C ndipo usajiliwe kuchukua degree. Mfano Ireland na India. Wewe unadai iwe option, hapo tukueleweje
Ni mawazo yangu tu, but kipi kifanyike unadhani kupunguza zero za Mathematics na physics? Unaonaje? Tunakwama wapi ku-implement system hiyo iliyoko India?
 
Back
Top Bottom