Nashauri madereva wa mabasi ya abiria wanaoendesha zaidi ya km 500 wawe na masaa 24 ya kupumzika

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,882
2,311
Salamu na pole majeruhi na ndugu walifikwa na ajali na wiki hii huko Newala na Singida.

Hawa madereva ukiacha hizi ligi za kijinga za kukimbizana na kuwahi kufika, pia huwa wanakuwa hawako sawa kutokana na 'go' and 'return' ya Kila siku ya safari zao.

Kifupi pale abiria tunakuwa tunaendeshwa na kama robot tu. Dereva anakuwa anatumia uzoefu tu.

Kichwani anakuwa hana muda wa kupumzika. Kinachosaidia ni kustuliwa mara kwa mara na wakaguzi wa njiani yaani traffic.

Nimeshasema juu hapo kuwa madereva was km zaidi ya 500 safari wawe na twenty 4 hours rest.

Asitoke tu asubuhi na kuanza safari kama anaenda shamba.

Huyu anabeba roho za watu jamani, sio kwamba anaenda kulinda ngedere shamba.

Sasa hao wa safari za usiku hata sijui utaratibu wao ukoje huko nadhani ndio kuna balaa..hakuna usimamizi wa uhakika.

😕 Asante.
 
Back
Top Bottom