Napendekeza tuanzishe JF Jogging Club ya mtandaoni

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
13,301
29,788
Wakuu sio siri kuwa ukivuka miaka 30 kuna mabadiliko ya kimwili lazima uyaone yakikujia kwa kasi ikiwemo kitambi. Kwa wale waliojaliwa riziki kidogo hali huwa mbaya zaidi ndo maana Mzee Janabi anazidi kutoa matamko. Wengi wetu tumekulia kwenye familia duni hivyo huku ukubwani baada ya mambo kuwa mazuri tunaanza kufakamia vyakula vya ndoto zetu. Sio mbaya ila lazima kuchukua tahadhari.

Sasa mimi nimekuja na hii hamasa ya members wa JF kujipa muda hata wa dakika 20 kufanya jogging ili kusaidia mwili kuwa fit. Kwa sababu humu hatutaki kujuana physically ninashauri tujiorodheshe tunaopenda mazoezi kisha kila siku tuji-committ kufanya mazoezi na kupeana updates kilichojiri huko uliko.

Binafsi sio mtaalamu wa mazoezi ila ningependa tuanze na 1KM CHALLENGE. Yaani kila siku members tupeane challenge ya kukimbia 1km.

Members watakaofanya hii challenge wanaweza tumia App ya jogging kama ile ya ADIDAS kwenye simu zao na kutupia matokeo yao kwa maana ya umbali waliokimbia, muda, calories burnes na pace. Ninaamini hii itahamasisha.

Ninakaribisha maoni.
Huu ni mfano wa report ya mazoezi niliofanya ya kutembea 5km na kukimbia 1km. Kama huna App fanya kupakua ADIDAS RUNNING.
IMG-20240322-WA0010.jpg
 
Mimi naenda Km 8 hadi 10 Kila siku jioni naenda kukimbia na Wakati wa kurudi natembea Huwa yanaambatana na mazoezi ya viungo,Kwa vile Niko Kisarawe huku nakutana na vilima viwili wakati wa kwenda na kurudi kimoja.Wakati huu wa Mvua na mwezi wa RAMADHANI Kwa wadau tumesimama.Ila Kila jioni pushups 10, Squatter series,mazoezi ya kukata tumbo pamoja na kunyosha mwili,haya nafanyia chumbani.Kwa Sasa Soda situmii kabisa,Nyama nimeacha kabisa.Niko na zaidi ya 40 lakini shemeji yenu anajua.
 
Kama hutumii soda umemuelewa dk. Janabi. Hongera
 
Jomba uko fit ile laana. Kwenda zaidi ya 2km kwa umri wako ni jambo jema hata ingekuwa kwa kutembea. Kuhusu soda huwa inafika tu wakati mwili unakataa ila sisi tunakuwa wabishi kuacha. Wewe ni mfano wa kuigwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom