Napendekeza Pascal Mayalla apewe nafasi ya kujibu maswali mbalimbali ya wadau wa jukwaa hili

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
3,116
6,995
Uongozi wa jamii forum na Wanachamq wote

Nishauri kuwa uanzishwe utaratibu kuwa na Uzi maalumu ambao member mmoja mbobezi kwenye eneo fulani ajibu maswali mbalimbali ya kisasa, kiuchumi au kijamii kutoka kwa wanaJF.

Itakuwa vema Uzi huu upangiwe muda na siku maalumu ili mhusika aweze kujiandaa

Naomba kwa kuanzia fursa hii naomba apewe mwanahabari na mwanasheria mbobezi Paskal Mayalla

Aksanteni sana
 
Katika jambo gani unadhani wachangiaji wengine hawana uwezo wa kujibu hayo maswali isipokuwa yeye tu? Kwa maoni yangu, tungekuwa wachangiaji serious (intelligent/critical/smart thinkers) tungejifunza mengi kutoka kwa kila mmoja wetu. Lakini baadhi ya wachangiaji "ni ovyo to the highest standard". Unakuta mtu anatoa mchango mzuri wao wanaanza personal attack na kutumia lugha ya kuudhi. Kwa mtindo kama huu hata tufanyeje hatuwezi kusonga mbele. Sijui shida ni wivu au itikadi za vyama vya siasa au labda just ignorance? Sijui shida huwa ni nini au labda ya kutokuwa serious?
 
We mshauri afungue darasa hapo mtaani kwako uwe una hudhuria. Unataka afundishe jukwaa zima kwa vigezo gani?
 
Kwa hapa hapana, huyu jamaa ana mapenzi na mahaba ya dhati kwa chadema
 
Mkuu Uzalendo wa Kitanzania, kwanza asante asante sana kwa kunifikiria, nimefarijika sana kwasababu kumbe kuna watu wanautambua uwezo wangu kusaidia wengine.

Kiukweli jf ina msaada mkubwa kwa taifa hili, nikatoa wazo la tuanzishe jf online TV, mimi nikajitolea kusimamia, vifaa na watenda kazi, tuandae vipindi maalum vya michango ya jf kwenye TV zetu Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako! angalia nilichojibiwa!.

Japo binadamu wote ni sawa, lakini watu tunatofautiana sana uwezo, wa kufanya baadhi ya vitu, kuna wengine wana uwezo zaidi ya wengine.

Mimi siku zote ni mtu wa kujitolea kusaidia wengine, hapa nilipo ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea na sasa pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea, natoa huduma kupitia TV ya Channel Ten Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=PFJg9uwRByyxPw99P
 
Kwenye maswala ya mautamu niwekwe mimi ngaiwoye. Ni mtaalamu wa mautamu yote unayoyajua wewe yasio haramu...utaaaam
 
JF kila jukwaa lina watu mahiri kwa jukwaa husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…