You can't eat your cake and have it!. Huwezi kupenda utumbuaji majipu, lakini yakitumbuliwa majipu ya demokasia ndipo unapiga kelele!. Mtu akiwa ni dikiteta kote kote!, hivyo you just have to take the bitter with the sweet!, sio uchague vitamu tuu ndio umeze halafu vichungu uteme!, hiyo demokasia yenyewe nalo ni jipu tuu, lazima litumbuliwe!.
Baadhi ya hao wapigania demokrasia ndio madikiteta wakuu ndani ya vyama vyao, wengine wakifanya uchaguzi wa maigizo!, wengine wakinyofoa kinyemela, vipengele vya ukomo wa uongozi ili watawale milele!.
Mimi ni miongoni mwa tuliomshauri mkuu wa kaya aiweke katiba pembeni, ainyooshe nchi hii kwa mkono wa chuma!.
Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria
Pasco