Sakascom
New Member
- Nov 26, 2018
- 3
- 1
Napenda kutoa ushauri Kwa taasisi za umma panapokuwa na changamoto au marekebisho ya kimfumo iwe inatolewa taarifa kuwa kuanzia saa Fulani Hadi Fulani kutakuwa na jambo Fulani kwahiyo hamtakuwa hai wakati huo.
Lakini Kwa sasa asilimia kubwa ya mifumo mingi ya taasisi za Umma kukiwa na marekebisho yoyote yanafanyika hakuna taarifa zozote unazopewa zaidi tu ukiingia katika mfumo husika unakuta unazunguka tu.
Embu tuige Kwa makampuni kama vile makampuni ya mawasiliano na kifedha yalivyo. Taarifa ni muhimu sana.
Tunatambua fika taasisi nyingi za Umma zimeanza kutoa huduma kwenye mifumo hivi karibuni hivyo hata uimara wa Moja Kwa Moja Kwa baadhi utakuwa mdogo. Kwa hiyo marekebisho lazima yanatakiwa kufanyika mara Kwa mara.
Sote wananchi tunatamani ifikie wakati mteja aliyeko Kigoma hata kama Ofisi husika ipo tu Dar es Salaam huyu mteja ahudumiwe au ajihudumie kama yupo katika Ofisi husika.
Huu ni ulimwengu wa utandawazi unaopewa nguvu na sayansi na technolojia, ambapo uwazi wa taarifa ni muhimu sana Kwa Maendeleo ya taasisi au makampuni mbalimbali.
Sote Kwa pamoja tukiamua tutaing'arisha Tanzania kama barafu ya mlima Kilimanjaro.
Kazi iendelee